Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all 9000 articles
Browse latest View live

Simba inahitaji ushindi kuliko kitu chochote kulinda heshima

$
0
0

Mchezo kati ya Mbeya City dhidi ya Simba unasubiriwa kwa shauku kubwa na wadau wa soka nchini kwa sababu ni mchezo utakaoamua kinara wa ligi kuu Tanzania bara baada ya mechi za mwisho wa juma hili.

Simba inahitaji ushindi kuliko kitu chochote kwenye mchezo huo ili kuendelea kuongoza ligi hasa baada ya matokeo ya mechi za jana (Jumamosi November 4, 2017) ambapo wapinzani wa Simba kwenye nafasi ya kwanza Yanga na Mtibwa zilibanwa na kulazimishwa sare huku Azam ikishinda na kuongoza ligi baada ya kufikisha pointi 19 pointi mbili zaidi ya Yanga na Mtibwa ambazo zilicheza jana.

Pointi tatu pekee ndio zitaifanya Simba kurejea kwenye nafasi yake, matokeo tofauti na hayo maana yake ‘Mnyama’ atapoteza uongozi wa ligi kwa kuiacha Azam itawale kileleni. Endapo Simba itashinda itafikisha pointi 19 sawa na Azam lakini wastani mzuri wa magoli utaipeleka kwenye nafasi ya kwanza, matokeo ya sare yoyote yataifanya ibaki nafasi ya pili kwa wastani wa magoli kwa sababu  italingana pointi na Mtibwa pamoja na Yanga. Ikipoteza mbele ya City itaendelea kusalia katika nafasi ya nne ambayo ipo sasa ikiwa na pointi 16.

Matokeo ya Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya

Wameshinda mechi tatu kati ya nne walizocheza kwenye uwanja wao wa nyumbani, hawajashinda mechi yoyote nje ya Mbeya matokeo yao ya ushindi yamepatikana kwenye uwanja wa Sokoine. Mbeya City tayari imecheza mechi nane, imeshinda michezo mitatu, sare mbili huku ikiwa imepoteza michezo mitatu.

‘Wana-koma kumwanya’ wamepoteza mchezo mmoja wakiwa uwanja wa Sokoine huku mechi nyingine mbili wakidondosha pointi sita kwenye viwanja vya ugenini.

  • Mbeya City 1-0 Majimaji
  • Mbeya City 0-1 Ndanda
  • Mbeya City 1-0 Njombe Mji
  • Mbeya City 2-0 Ruvu Shooting

Katika magoli tisa waliyofunga kwenye mechi zao nane, manne kati ya hayo wamefunga wakiwa kwenye uwanja wa Sokoine na magoli matano yakifungwa kwenye viwanja vya ugenini.

Matokeo ya mechi za Simba nje ya uwanja wa Uhuru

Simba hawana rekodi nzuri wanapocheza viwanja vya ugenini, wameshinda mechi mmoja kati ya tatu walizocheza nje ya uwanja wa Uhuru. Ushindi pekee wa Simba katika mechi walizocheza nje ya uwanja wa Uhuru ni dhidi ya Stand United ya Shinyanga. Mchezo wa Yanga vs Simba haujahesabiwa kama wa ugenini kwa sababu uwanja huo ni wa nyumbani kwa vilabu vyote viwili kinachobalika ni zamu ya timu ipi kuwa nyumbani na nyingine kuwa ugenini kwenye uwanja huohuo.

  • Azam 0-0 Simba
  • Mbao 2-2 Simba
  • Stand United 1-2 Simba

Simba imefunga magoli manne tu nje ya uwanja wa uhuru kati ya magoli 20 iliyofunga katika mechi nane zilizopita za ligi kuu.

Matokeo ya Mbeya City vs Simba uwanja wa Sokoine, Mbeya

Mbeya City imecheza mara nane (mechi zote nyumbani na ugenini) mechi za VPL dhidi ya Simba tangu timu hiyo ya jijini Mbeya ilipopanda kucheza ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2013/2014. Katika mechi nne ambazo Mbeya City imekutana na Simba kwenye uwanja wa Sokoine, Simba imeshinda mara mbili, imefungwa mara moja na kuambulia sare mara moja.

  • 12/10/2016 Mbeya City 0-2 Simba
  • 17/10/2015 Mbeya City 0-1 Simba
  • 18/04/2015 Mbeya City 2-0 Simba
  • 15/02/2014 Mbeya City 1-1 Simba

Brenden Rodgers aweka rekodi kubwa na Celtic, aipita rekodi ya Wenger

$
0
0

Kocha wa zamani wa Liverpool Brenden Rodgers ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kuifanya timu kutoka Uingereza kucheza michezo 63 ya ligi ya ndani bila kupoteza.

Kikosi cha Celtic kimeshinda michezo 56 na kusuluhu 7 wakiwa wamefunga mabao 183, wakifungwa 35 na kucheza michezo 36 bila nyavu zao kuguswa.

Lakini pamoja na Rodgers kuwapa Celtic rekodi hiyo tayari kuna vilabu ambavyo vimecheza mechi nyingi zaidi katika ligi zao bila kupoteza mchezo hata mmoja.

1.Steaua Bucharest. Hakuna klabu dunianj inayofikia rekodi ya timu hii kutoka Romania,mwaka 1986 wakati wakibeba kikombe cha European Cup walicheza michezo 119 ya ndani hadi mwaka 1989 ndipo wakapoteza mchezo.

2.Lincolin Red Imps. Mwaka 2009 mwezi May hadi September mwaka 2014 walicheza michezo 88 ya ligi ya kwao bila kupoteza mechi na pia wamewahi kuchukua makombe 14 mfululizo ya ligi nchini kwao Gibraltar.

3.Ac Millan. Kati ya mwaka 1991 na 1993 klabu soka ya Ac Millan ilichukua makombe matatu mfululizo, lakini si hivyo tu bali pia Millan walicheza michezo 58 ya ligi ya kwao bila kupoteza hata mmoja.

4.Ajax. Ajax iliyochukua ubingwa wa Champions League mwaka 1995 ilikuwa kati ya Ajax bora kuwahi kutokea,mwaka ambao wanachukua kombe hilo walicheza michezo 52 bila kupoteza mchezo hata mmoja.

5.Arsenal. Wengi wanaikumbuka Arsenal hii ya nwaka 2003 ambapo hadi inafima 2004 mwezi October walikuwa hawajapoteza mchezo na Manchester United ndio walikatisha safari yao ya michezo 49 bila ushindi

Kichuya kairudisha Simba kileleni

$
0
0

Goli pekee la Shiza Kichuya limeirudisha Simba kwenye nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi kuu Tanzania bara kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.

Kabla ya mchezo huo, Simba ilikuwa nafasi ya nne nyuma kwa pointi moja kwa Yanga na Mtibwa zilizotoka suluhu kwenye  mechi zao za jana lakini ilikuwa imezidiwa pointi tatu na Azam ambayo ilishinda dhidi ya Ruvu Shooting.

Uhindi wa Simba dhidi ya Mbeya City umeipa Simba pointi tatu na sasa imefikisha pointi 19 sawa na Azam lakini Simba inaonoza ligi wastani wa magoli dhidi ya Azam.

  • Kichuya amefikisha magoli matano (5) kwenye ligi sawa na Ibrahim Ajib wa Yanga huku akiwa anaziwa na Mohamed Rashid wa Tanzania Prisons mwenye magoli sita na Emanuel Okwi wa Simba anaeongoza akiwa na magoli nane.
  • Simba imeshinda mechi ya tatu kati ya tano ilizokutana na Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya. Kabla ya mchezo wa leo, Simba ilikuwa imeshinda mechi mbili kati nne, mchezo mmoja walitoka sare na mwingine walipoteza.
  • Mbeya City imepoteza mchezo wa pili kati ya mechi tano walizocheza kwenye uwanja wa Sokoine. Mchezo mwingine waliopoteza kwenye uwanja wa Sokoine ilikuwa dhidi ya Ndanda.
  • Simba imeshinda mechi yake ya pili nje ya uwanja wa Uhuru ambao ndio uwanja wao wa nyumbani.

Hivi ndivyo Arsene Wenger alivyoamgamia Etihad, City waendelea kuweka rekodi mpya

$
0
0

Mchezo wa pili kati ya michezo kumi iliyopita Pep Gurdiola anapata ushindi zidi ya Arsenal ushindi ambao unawafanya Manchester City kuendelea kutawala katika ligi ya Epl.

Alikuwa Kelvin De Bruyne dakika ya 19 ndio alizifungua nyavu za Arsenal baada ya kupiga shuti lililomshinda mlinga lango wa Arsenal Petr Cech.

Goli la leo la Kelvin De Bruyne zidi ya Arsenal linamfanya kuifunga Arsenal bao mbili na kutoa assist mbili katika michezo 5 ambayo Mbelgiji huyo amecheza zidi ya Arsenal.

Ushindi wa leo wa City ni muendelezo wa rekodi mbovu ya Arsenal ambao hawajawahi kushinda mchezo wowote Epl wa ugenini ambao walimaliza kipindi cha kwanza wakiwa wamefungwa ndani ya miaka 6.

Kun Aguero aliifungia Manchester City bao la pili kwa mkwaju wa penati bao ambalo linawafanya Arsenal kuwa timu inayoongozwa kwa kufungwa magoli ya penati tangia kuanza kwa msimu uliopita.

Lakini Alexandre Lacazette aliyeingia akitokea benchi aliipatia Arsenal bao la kufutia machozi dakika ya 65 na kuwafanya Arsenal kuwa timu ambayo yenye mabao mengi kutoka kwa wachezaji wa akiba kuliko timu yoyote Epl tangu msimu uliopita (mabao 13).

Dakika ya 74 Manchester City walifunga bao ambalo lilizua utata kutoka kwa Gabriel Jesus baada ya kuonekana kama wachezaji wa City walikuwa offside na mchezo kumalizika kwa City kushinda 3 kwa 1.

Mabao matatu waliyopata Manchester City hii leo yanawafanya kufikisha idadi ya mabao 57 katika mechi zao 17 msimu huu idadi ambayo mara ya mwisho kutokea Epl ilikuwa msimu wa mwaka 1992/1993.

Alvaro Morata apigilia msumari wa moto kwenye kidonda cha Manchester United

$
0
0

Manchester United wameendeleza rekodi mbovu dhidi ya timu kubwa baada ya hii leo Jose Mourinho kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya mabingwa watetezi.

Alikuwa Alvaro Morata dakika ya 55 kufunga bao pekee katika mchezo wa leo huku likiwa bao lake la nne la kichwa kati ya mabao saba aliyofunga msimu huu wa ligi.

Bao la leo la Alvaro Morata linamfanya mchezaji ambaye amefunga mabao mengi ya kichwa (10) kuliko mchezaji yoyote katika ligi kubwa tano barani Ulaya.

Matokeo ya leo yanawafanya Manchester City kuongoza ligi kwa tofauti ya alama 8 huku Chelsea wakipunguza pengo la alama na United na sasa wanatofautiana kwa pointi moja.

Katika matokeo mengine Everton waliokuwa nyumbani walitoka nyuma ya mabao mawili na kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya Watford.

Watford  walitangulia kupata mabao mawili kupitia kwa Ricahrlison na Kabasele kabla ya Oumar Niesse na Lewin kuisawazishia Everton kisha Leighton Baines kufunga bao la ushindi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Everton kutoka nyuma kwa mabao mawili na kuibuka na ushindi tangu wafanye hivyo mara ya mwisho mwaka 1994 dhidi ya Wimblendon Memories.

Siku 176 zimepita tangu Ruvu Shooting ipate ushindi wa mwisho VPL

$
0
0

Ruvu Shooting ndio timu pekee ya ligi kuu Tanzania bara ambayo bado haijashinda hata mechi moja tangu kuanza kwa msimu huu (2017/2018) ikiwa tayari kila timu imecheza mechi tisa hadi sasa.

Kikosi hicho cha kocha Abdulmutik Haji akisaidiwa na Selemani Mtungwe kimepoteza mechi nne na kutoka sare katika mechi zake tano, imekusanya pointi tano sawa na idadi ya mechi zake ilizotoka sare.

Ruvu Shooting ndio timu iliyofungwa magoli mengi zaidi, imeshafungwa magoli 14 tangu ligi ilivyoanza msimu huu huku yenyewe ikiwa imefunga magoli matatu na kufanya wastani wake wa magoli kuwa -11.

Mara ya mwisho Ruvu Shooting kupata ushindi ilikuwa May 14, 2017 msimu uliopita (2016/17)  ilipoifunga African Lyon  1-0 kwenye uwanja wa Uhuru Dar baada ya hapo ilipoteza mchezo wake wa mwisho msimu uliopita kwa kufungwa na 2-1 na Stand United kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga. Tangu hapo matokeo ya vipigo na sare yamekuwa rafiki kwa Ruvu Shooting.

Matokeo ya Ruvu Shooting msimu huu 2017/2018

  • 26/08/2017 Simba 7-0 Ruvu Shooting
  • 10/09/2017 Kagera Sugar 1-1 Ruvu Shooting
  • 16/09/2017 Lipuli 0-0 Ruvu Shooting
  • 24/09/2017 Ruvu Shooting 1-1 Mtibwa Sugar
  • 30/09/2017 Ruvu Shooting 1-1 Njombe Mji
  • 14/10/2017 Ruvu Shooting 0-0 Singida United
  • 21/10/ 2017 Mbeya City 2-0 Ruvu Shooting
  • 30/10/2017 Tanzania Prisons 1-0 Ruvu Shooting
  • 04/11/2017 Azam 1-0 Ruvu Shooting

Baada ya kufungwa 7-0 na Simba kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi msimu huu, Ruvu Shooting ilitoka sare katika mechi tano mfululizo zilizofuata, baada ya hapo ikapoteza mechi tatu mfululizo.

Mkufunzi wa waamuzi CAF apata kigugumizi goli la Kichuya vs Mbeya City

$
0
0

Goli alilofunga Shiza Kichuya kwenye mchezo wa VPL kati ya Mbeya City dhidi ya Simba limezua mjada mkubwa kwa wadau wa soka wapo wanaosema kabla Kichuya hajapokea pasi kutoka kwa Jonas Mkude alikuwa ameotea (Offside) huku wengine wakisema hakuwa ameotea (alikuwa-Onside).  Kila mtu amekuwa akiamini kile anachokiamini kutokana na utata uliopo kabla ya goli hilo kufungwa.

Mkufunzi wa waamuzi anayetambuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Leslie Liunda kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa kitaalamu zaidi lakini katika maoni yake ameshindwa kusema moja kwa moja kama Kichuya alikuwa offside au onside kabla ya kufunga goli.

“Kamera hazikuonesha vyema, offside inaamuliwa wakati mpira unapigwa si wakati wa kupokea mpira. Picha haioneshi vizuri wakati mpira unapigwa nafasi ya Kichuya ilikuwaje, hivyo tunapaswa kukubaliana na maamuzi ya mwamuzi msaidizi (assistant referee)”- ) Leslie Liunda.

Ukiachana na mazingira ambayo Kichya alifunga goli (yanatajwa kuwa tata) mjadala mwingine unaoendelea ni kuhusu mpira ulioguswa kwa mkono na Jonas Mkudeakiwa kwenye eneo la penati, wapo wanaoamini kwamba mwamuzi alitakiwa kutoa adhabu ya mkwaju wa penati kutokana na kitendo cha Mkude kuushika mpira lakini wapo wengine wanasema mpira ulifuata mkono.

Nipe maoni yako (unachokiamini wewe) kutokana na matukio hayo mawili yaliyotokea kwenye mchezo wa jana Jumapili November 5, 2017 mechi iliyomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine.

Exclusive: “Ngasa alihitaji uvumilivu wa Samatta kufanikiwa”-kaka yake kafunguka

$
0
0

Ally Khalfani Ngasa ambaye ni kaka wa mchezaji wa Mbeya City Mrisho Ngasa amesema mdogoake  alitakiwa kuvaa moyo wa uvumilivu kama Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ili afanikiwe katika soka la kimataifa.

Ally Ngasa amesema nafasi ambayo aliipata mdogoake kama angekuwa mvumilivu huenda angekuwa mbali badala ya uamuzi wake wa kuvunja mkataba na klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini.

“Hayakuwa maamuzi sahihi, hata Samatta alivyokwenda TP Mazembe hakuanza moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza, alivumilia badae akawa anaingia kipindi cha pili lakini badae akawa anategemewa na timu. Ngasa alitakiwa kuvumilia kama walivyovumilia Samatta na Ulimwengu.”

“Ngasa alivunja mkataba ili awe huru kwenda timu nyingine kwa sababu timu aliyokuwepo (Free State Stars) alikuwa hapati nafasi ya kucheza, hiyo ndio sababu aliyomwambia mzee.”

“Mpira siku zote ni mchezo wa uvumilivu kwa sababu uwezo wake ulikuwa ni mkubwa asingekosa timu nje. Sasa hivi yupo Mbeya City uwezo wake umepungua sio kama zamani halafu hasikiki kama alivyokuwa Yanga, Azam na Simba.”

Kaka yake Ngasa bado anaamini mdogoake anaweza kutoka tena kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi kwa sababu bado umri wake unamruhusu.

“Umri bado unamruhusu kwa sababu hata miaka 30 bado hajafikisha akijipanga vizuri akarudi kwenye kiwango chake cha zamani anaweza kutoka tena kucheza nje ya nchi.”


Mchezaji apigwa na kitu kinachodhaniwa ni bomu akiwa uwanjani kwenye ligi ya kina Mbwana Samatta

$
0
0

Ligi kuu nchini Ubelgiji iliendelea mwishoni mwa wiki lakini habari iliyotawala vyombo vya habari nchini Ubelgiji ni bomu la moshi lililotupwa uwanjani wakati wa mchezo kati ya Sporting Charlelois vs Royal Antwerp.

Shabiki wa klabu ya Royal Antwerp alirusha bomu hilo wakati wachezaji wa klabu ya Sporting Charleois wakishangilia bao lao la pili bomu ambalo lilimpiga mchezaji wa Charleois begani na kumjeruhi.

Christian Benavente kiungo raia wa Peru ndie mhanga wa tukio hili japokuwa kocha wa Royal Antwerp amemtupia lawama Benavente kwa kwenda kushangilia mbele ya mashabiki wa timu pinzani. 


Benavente amejitetea kwamba hakuwa na nia ya kumuudhi mtu yoyote na anashangazwa na kitendo cha mashabiki wa Royal kumrushia bomu hilo wakati kushangilia lilikuwa tukio la kawaida kwenye mchezo huo.

Ushindi wa Charleloi umeendelea kuwaweka katika nafasi ya pili ya ligi ya Ubelgiji wakiwa na alama 28 alama 9 zaidi ya Genk anayoichezea Mbwana Samata walioko katika nafasi ya kumi.

RASMI: Safari ya Ndemla Sweden imeiva

$
0
0

Taarifa rasmi kutoka Simba imethibitisha kiungo wao mshambuliaji Said Hamisi ‘Ndemla’ anaondoka kesho kwenda nchini Sweden kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.

Atafanya majaribio hayo kwenye klabu ya AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi kuu nchini Sweden. Majaribio hayo ni ya wiki mbili (siku 14).

Eskilstuna ndio klabu ambayo anakipiga mtanzania mwingine Thomas Ulimwengu ambaye kwa sasa anauguza jeraha la goti baada ya kufaniwa upasuaji.

Slaven Bilic atupiwa virago West Ham huku kocha wa zamani wa United akitajwa kuchukua nafasi yake

$
0
0

Baada ya kupokea kipigo kutoka kwa Liverpool huku wakiandamwa na matokeo mengi yasiyoridhisha siku za usoni hatimaye West Ham wameamua kumfukuza kazi kocha wao mkuu Slaven Bilic.

Katika kuonesha kwamba West Ham wameamua kufanya mabadiliko wameamua kumtimua Slaven Bilic pamoja na jopo la makocha wake wasaidizi akiwemo Nikola Jurcevic, Edin Terzic na Julian Dicks.

Msimu huu West Ham wamefanikiwa kushinda michezo miwili tu ya ligi kuu Uingereza huku wakipoteza michezo yao mitatu ya mwanzo ya ligi kuu nchini Uingereza.

Hadi sasa West Ham wanashikilia nafasi ya 18 katika msimamo wa ligi Epl na tayari kocha wa zamani wa klabu ya Everton ambaye pia amewahi kuifundisha Manchester United David Moyes anatajwa kuchukua mikoba ya Bilic.

Chelsea wapata pigo kubwa linalozua mashaka nafasi ya Conte

$
0
0

Michael Emenalo linaweza kuwa jina jipya kwa mashabiki wa soka lakini sura ya Emenalo inaweza isiwe sura ngeni kwa mashabiki wa soka Epl haswa wanaoangalia michezo ya mabingwa watetezi Uingereza Chelsea.

Michael Emenalo alikuwa moja ya wakurugenzi wa masuala ya ufundi ndani ya klabu ya Chelsea ambaye pamoja na uwezo wake lakini anaijua vyema Chelsea kwani amekaa klabuni hapo kwa miaka kumi sasa.

Tangu Emenalo awe katika bodi ya ufundi ya Chelsea wamefanikiwa kushinda makombe ya Epl mara tatu, Europa mara moja na pia wamefanikiwa kombe moja la Champions League katika kipindi chake.

Lakini sasa baada ya miaka hiyo 10 hii leo Michael Emenalo ameamua kuachana na klabu ya Chelsea huku habari za ndani zikisema kwamba Michael Emenalo anaelekea kujiunga na klabu ya Monaco. 

Habari ya Emenalo kuachana na Chelsea inazidi kukuza tetesi ya maelewano mabovu yanayotajwa kuwepo kati ya kocha wa sasa wa Chelsea Antonio Conte na baadhi ya viongozi wa klabu ya Chelsea.

Habari nyingine toka darajani inasemekana kocha Antonio Conte amejikuta akiingia kwenye ugomvi mpya na beki wa klabu hiyo David Luiz jambo lililopelekea kumuweka nje katika mpambano zidi ya United.

“Ukizoea kuzika, na wewe utazikwa”-Julio

$
0
0

Na Yohan Gwangway

Vinara wa kundi C ligi daraja la kwanza nchini Tanzania Dodoma Fc leo wameshindwa kuwika katika mchezo wao uliopigwa katika uwanja wa Nyamagana baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 mbele ya Pamba

Mara baada ya mchezo wa leo kocha mkuu wa Dodoma Fc Jamhuri Kiwelu ‘Julio’ amesema imekuwa mazoea wao kuwafunga wenzao lakini leo msiba umekuwa kwao na wameshindwa kihalali

“Siku zote sisi tumekuwa tukishinda, ukizoea kuzika ipo siku na wewe utazikwa”, alisema Julio mara baada ya mchezo wa leo

Wakicheza kandanda safi mbele ya mashabiki wao Pamba walicheza bila mafanikio ya goli katika kipindi cha kwanza licha ya kuwadhibiti wachezaji wa Dodoma Fc katika idara zote

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku ikichukua dakika 4 pekee ambapo Amosi Mnyapi aliwainua mashabiki wa Pamba

Mabingwa hawa mara mbili wa Tanzania walicheza mchezo wa kulinda goli lao hilo kwani walicheza kwa tahadhari kubwa huku mpira ukichezwa katikati ya uwanja muda mwingi. Pamba ambao waliingia katika mchezo wa leo wakiwa na alama 6 sasa wamefikisha alama 9 mara baada ya michezo 8 katika kundi C

Kwa matokeo haya sasa kundi hili linaonekana kuwa gumu zaidi kwani Dodoma Fc wana alama 18, Pamba alama 16 na Biashara wanasogea kwa karibu wakiwa na alama 14

Katika michezo yote 14 ambayo kila timu itacheza katika makundi yote matatu zitatoka timu 6 ambazo zitapanda ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu ujao.

Andrea Pirlo atundika daluga rasmi

$
0
0

Miaka 38 inaonekana imetosha kwa Andrea Pirlo kucheza soka na sasa kiungo huyo Muitaliano ametundika daluga rasmi na hatocheza tena soka katika timu yoyote ile.

Pirlo ambaye amewahi kuvichezea vilabu vya Inter Milan, Ac Milan na Juventus  alianza kucheza soka katika klabu ya Brescia huku pia akiishinda michezo 116 ya timu ya taifa ya Italia.

Andrea Pirlo alishinda kombe la Serie A mara mbili, champions league mara mbili na kikombe cha klabu bingwa dunia akiwa na Ac Milan huku akiwepo katika timu ya taifa Italia iliyobeba kombe la dunia 2006.

Andrea Pirlo pia alikuwa nguzo muhimu wakati Juventus ikishinda kombe la Italia mwaka 2012 hadi 2015 kabla ya kuachana na Juventus nakwenda kucheza ligi kuu ya Marekani MLS mwaka 2015.

Tangu aanze kucheza soka Pirlo amebeba kombe la Italia Serie mara 6, kombe la Copa Italia mara 2, kombe la champions league mara 2 na kbe la dunia mara 1 katika jumla ya michezo 872 aliyocheza.

Cazorla: Hivi ndivyo majeruhi yalivyotishia ndoto yangu, upasuaji mara 8, almanusra kukatwa mguu

$
0
0

Ukubwa wa majeruhi ya muda ya Santi Cazorla unaelezewa na mchezaji mwenyewe ambaye aliambiwa na madaktari kwamba akiweza tu kutembea na mwanae kwenye bustani basi yangekuwa ni mafanikio makubwa.

Ilikuwa mnamo September 10, 2013 jijini Geneva wakati Spain wakicheza mechi ya kirafiki na Chile, Cazorla akashindwa kumaliza mchezo baada ya kutokana na kuumia enka, jeraha ambalo liliacha mpasuko kwenye mfupa. Tangu wakati huo, alijifunza kuishi na kucheza na maumivu katika mguu wake wa kulia.

Picha inayoonyesha namna mguu wake wa kulia ulivyorika baada ya upasuaji

“Mara ya kwanza nilikuwa naweza kuvumilia maumivu kiasi kidogo. Nilikuwa nikipata joto kidogo nilikuwa naweza kucheza, lakini ilipofika wakati wa mapumziko na mwili ukishapoa nilikuwa napata maumivu ambayo nilikuwa naishia kutoa machozi.”

December 5, 2015, alifanyiwa upasuaji kutoka na kuumia goti la kushoto, lakini tatizo la kwenye enka liliendelea kukua.

Lakini kutokana na matamanio yake ya mchezaji muhimu katika kikosi cha Arsenal, aliendelea kujaribu kuvumilia kadri alivyoweza lakini hakukuwa na namna zaidi kupata matibabu.

Mpaka kufikia hatua hiyo, Cazorla hakuweza kufikiria kwamba njia yake ya matibabu ingekuwa ndefu na nyeusi, kwa kufanyiwa upasuaji mmoja baada ya mwingine.

Madaktari nchini Uingereza hawakuwa wakimpa imani vya kutosha.

“Ikitokea umeweza kutembea tena hata mwanao kwenye bustani, basi ridhik, walianiambia hivyo madaktari.” – anasema Cazorla.

Hivyo soka Ilibidi lilirudi siti ya nyuma na kuweka umakini wote kwenye kupona majeraha na angalau aweze hata kutembe tena.

Mwaka mmoja baada ya upasuaji kwenye goti, akahitaji upasuaji mwingine kwene msuli wa paja wa mguu wa kulia.

Picha inaonyesha jeraha la enka kwenye mfupa wa ndani kabisa

Kile kilichoonekana kitamuweka nje kwa wiki 3, kilitishia kumaliza maisha yako soka ya Cazorla.

Baada ya mwezi upasuaji wa enka, nyuzi zikaondolewa, lakini kidonda kikawa kinafunguka kila kukicha, ilifikia hatua ikabidi afanyiwe upasuaji mara 8 zaidi ndani ya mwaka.

Kuna wakati kipindi hicho bado nilikuwa nacheza. Wataalam waliniambia haikuwa na shida, tatizo lilikuwa kwamba kidonda hakikupona na kikawa kinafunguka mara kwa mara, kilipata maambuziki.”

Hakuweza kufikiria ambacho alikuja kuambiwa na Dr. Mikel Sanchez alipokutana nae huko Vitoria mnamo May 2017.

Cazorla alikutana na daktari huyo baada ya kukosa tiba nchini England.

Akiwa chumba cha upasuaji Dr Sanchez alimwambia maneno ambayo yalimfanya ashike kichwa.

Aliona jinsi maambukizi yalivyo makubwa, na jinsi mifupa ilivyorika.” Cazorla anaelezea.

“Kulikuwa na shimo kubwa, angalau sentimenta 8 za mfupa zilikuwa zimepotea kuingia ndani.”

Wakati huo ndio waligundua wadudu wengine wa bacteria ambao walikuwa wanashambulia kwa kasi mfupa, na kuzidisha maambukizi..

Cazorla alifanyiwa matibabu kadhaa yaliyofanikiwa ya antibiotic lakini kulikuwa na tishio kwamba maambukizi ya damu yangeweza kukatwa kwa mguu.

Dr. Sanchez mwenyewe, ambaye alikiri kwamba hakuwahi kuona tatizo la namna hiyo, alimfanyoa upasuaji wa mwisho mnamo May 29.

Wakati wa kiangazi uliopita Cazorla akaanza program ya rehabilitation na amekuwa akiendelea vizuri.

Hivi sasa ute ute wa mifupa umepunguza kasi ya uponaji, lakini pia mpai sasa haijafahamika atarudi lini uwanjani.

Arsenal wameshaongeza mkataba mnamo November 2017 mpaka June 2018, na anataka kurudi uwanjani kucheza tena soka.

“Sina ruhusa ya kucheza mpaka January, lakini nitarudi wakati huo ukifika.”

Mwezi mmoja uliopita alikuwa akikimbia kwenye uwanja wa Estadio Helmantico na kaka yake alipomuona alianza kutokwa na machozi.

Tangu July, Cazorla amekuwa akiishi hotelini katik jiji la Salamanca akipatiwa matibabu.

“Familia yangu ipo London kwa sababu watoto wangu walianza shule kule. Kuwa hapa mwenyewe bila uwepo wao ni kitu kigumu sana kwangu.”

Kila asubuhi anaamka mapema na kuanza mazoezi kwenye swimming, anatumia lisaa limoja kwenye baiskeli kila siku kwenye mazoezi yake.

“Mara nyingi sana anapokea message za kunitakia kheri kutoka Iniesta, Silva, Villa… ,” anasema, huku akikumbuka mafanikio ya kushinda ubingwa wa ulaya mara mbili.

Anasema hakujitaji kupata mwanasaikolojia kwa ajili ya kumuongoza katika kipindi hiki kigumu alichopopitia.

“Namshukuru Mungu kwa kila kitu, yote niliyopitia hayakuwa rahisi – halikuwa tu jeraha la kawaida kama watu walivyoamini. ‘Hakuna aliyeamini nitarudi uwanjani, ila nashukuru sasa naendelea vyema sana, NITAREJEA tena uwanjani.”


Kichuya kamkamata Ibrahim Ajib

$
0
0

Goli alilofunga Shiza Kichuya dhidi ya Mbeya City limemfanya afikishe magoli matano na kumfikia kiungo mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajib mwenye idadi hiyo ya magoli. Ajib na Kichuya wapo nyuma ya Mohamed Rashid mwenye magoli sita na mkongwe Emanuel Okwi mwenye magoli nane akiongoza chati ya wafungaji wa VPL hadi sasa baada ya mechi tisa kuchezwa.

Kichuya amefunga katika mechi mbili mfululizo zilizopita alifunga goli la kuongoza dhidi ya Yanga mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya 1-1, akafunga bao pekee la Simba kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City. Ajib hajafunga katika mechi mbili za Yanga zilizopita (Yanga 1-1 Simba na Singida United 0-0 Yanga) mara ya mwisho kufunga ilikuwa mechi ambayo Yanga ilishinda 4-0 dhidi ya Stand (alifunga mawili).

Magoli matano ya Shiza Kichuya msimu huu

  • Simba 7-0 Ruvu Shooting (alifunga goli lake la kwanza msimu huu, Okwi alifunga (4), Liuzio (1) na Nyoni (1)
  • Mbao 2-2 Simba (alifunga goli moja goli jingine lilifungwa na James Kotei)
  • Stand United 1-2 Simba (alifunga goli moja, Laudit Mavugo alifunga goli jingine)
  • Yanga 1-1 Simba (alifunga goli la kuongoza kabla ya Yanga kusawazisha)
  • Mbeya City 0-1 Simba (alifunga goli pekee la ushindi)

Magoli matano ya Ajib VPL tangu amehamia Yanga

  • Njombe Mji 0-1 Yanga (alifunga kwa mkwaju wa free kick)
  • Yanga 1-0 Ndanda (bao lake pekee liliipa Yanga ushindi wa kwanza uwanja wa Uhuru msimu huu)
  • Kagera Sugar 1-2 Yanga (alifunga goli la moja jingine lilifungwa na Obrey Chirwa)
  • Stand United 0-4 Yanga (alifunga magoli mawili Pius Buswita na Obrey Chirwa wakafunga moja kila mmoja).

Samatta kuiibukia Stars Benin

$
0
0

Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta na Farid Musa hawatakuja nchini badala yake wataungana na timu na wachezaji wengine huko Benin kwa ajili ya mchezo wa kirafiki.

“Mbwana Samatta na Farid Musa hawatokuja hapa (Tanzania) wataungana na timu nchini Benin, wanatarajia kufika huko November 7 ambapo tayari TFF imeshaandaa watu wa kwenda kuwapokea huko”-Alfred Lucas, afisa habari TFF.

Stars inatarajia kucheza ugenini dhidi ya Benin mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kalenda ya FIFA ambao unatarajiwa kuchezwa November 12, 2017.

Antonio Conte kwenye kivuli cha Sir Alex Ferguson

$
0
0

Dimitri Berbatov aliwahi kukiri kwamba wakiwa mazoezini huwa kunatawala ukimya mkubwa kuanzia kwa wachezaji hadi makocha wengine wa benchi la ufundi pale kocha mkuu Sir Alex Ferguson anapofika Carrington.

Watu walikuwa wakimuogopa sana SAF japokuwa alikuwa anapenda kuwaweka wachezaji karibu na yeye, hakuna aliyekuwa juu ya Ferguson na ndio maana haikuwa jambo gumu mtu maarufu kama Beckham kuondoka United kwa style ya aibu.

Nimemkumbuka Alex Ferguson baada ya kumuona Antonio Conte anachowafanya Chelsea kwa sasa, bila uoga wala hofu yoyote anaingia katika msuguano na mchezaji mkubwa mwingine wa Chelsea tena ikiwa katika misimu miwili mfululizo.

Msimu uliopita Muitaliano huyu pamoja na msaada wote ambao Diego Costa aliutoa hadi Chelsea wakabeba ubingwa lakini Conte alimchana tena kwa message na kumuambia wazi hana mpango naye msimu huu.

Kila mtu alishtushwa na habari za Diego Costa lakini wakati watu wakiwa wameanza kusahau ya Diego Costa sasa Antonio Conte huyu huyu anaingia kwenye mzozo na mchezaji ambaye ni kipenzi cha mmiliki wa Chelsea Roman Abromovich.

Antonio Conte anajua wazi kwamba Roman ndio aling’ang’aniza David Luiz arudi Chelsea lakini Antonio anaziba macho na masikio anamuweka nje Luiz katika mechi kubwa na sababu ikitajwa kwamba ni kutokuelewana kati ya wawili hao.

Siku ya Alhamisi iliyopita Antonio Conte aliwaita wachezaji wote katika vyumba vya kubadilishia nguo na inadaiwa aliwapiha mkwara kuhusiana na masuala ya kufanya vitu asivyotaka na inadaiwa kwamba alimtumia Luiz kuonesha mfano kitakachowapata wengine.

Inasemekana katika mazoezi ya mwisho ya Chelsea kuelekea mchezo zidi ya Manchester United Conte alimuweka Luiz kama muokota mipira akishuhudia wenzie wakicheza mazoezi kati ya timu ya kwanza na ya akiba.

Wakati Antonio Conte huyu huyu anamtema Branislav Ivanovic kila mtu alijiuliza kuhusu akili za Conte lakini akambwaga bila kusikiliza ni ni watu au mashabiki wa Chelsea watasema.

Huyu ndio Conte mwenye roho ya Fergie hajali kuhusu bosi, hajali kuhusu umaarufu wako na jina lako anachotaka yeye kila mtu ajue kwamba yeye ndio kiongozi wa timu na usipomsikiliza utaokota mipira mazoezini kama David Luiz.

Taarifa mpya kuhusu Ndemla kwenda Sweden

$
0
0

Taarifa kutoka uongozi wa Simba zinaeleza kwamba, kiungo wao Said Hamisi ‘Ndemla’ safari yake ya kwenda nchini Sweden kufanya majaribio kwenye klabu ya AFC Eskilstuna imesogezwa mbele hadi Alhamisi November 9, 2017.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana, ilieleza Ndemla ataondoka leo jioni kuelekea Sweden kufanya majaribio ya siku 14 kwenye klabu ya AFC Eskilstuna  lakini hadi sasa hazitajwa sababu za mabadiliko hayo.

“Tunapenda kuwafahamisha kuwa  safari ya mchezaji wetu Hamis Said Juma Ndemla iliyokuwa ifanyike leo Jumanne imesogezwa mbele”-Haji Manara, Afisa Habari Simba.

“Ndemla ambaye amepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio katika klabu ya AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi kuu nchini Sweden ,sasa ataondoka nchini siku ya Alhamis ya tarehe 9 ya mwezi huu.”

“Mabadiliko haya ya safari hayataathiri muda wake wa majaribio katika klabu hiyo,ambapo atakuwa huko kwa siku 14.”

Acheni kumuonea Lukaku, huyu ndiye mchezaji anayewaangusha Manchester United katika mechi kubwa

$
0
0

Wakati mchezo wa Chelsea vs Manchester United ukiendelea mchambuzi mmoja wa kituo cha Sky Sports Jamie Caragher alisikika akisema Eden Hazard alikuwa bora kiasi cha kumfanya namba 10 wa timu pinzani asieleweke nini anafanya.

Caragher alimlenga Henrikh Mkhitaryan ambae wakati wote wa mchezo dhidi ya Chelsea alionekana kama mzurulaji uwanjani kwani alikuwa akitembea tu huku na huku na kazi aliyokuwa akifanya uwanjani haikujulikana.

Dakika ya 86 ya mchezo takwimu zinasoma kwamba Hazard amegusa mpira mara 72, amedrible mara 4 zilizofanikiwa, ametengeneza nafasi moja na huku akiwa amefanikiwa kupiga mashuti mawili.

Lakini wakati takwimu hizo zikitoka inaonesha pia kwamba Mkhitaryan dakika zake 63 aligusa mpira mara 28 tu, akidrible mpira mara moja lakini akiwa hajatengeneza nafasi hata moja wala kupiga shuti golini.

Tatizo kubwa kwa Mkhitaryan inaonekana ana tatizo linaloendana na la Romelu Lukaku kwani katika michezo yote mikubwa ambayo United wamecheza Mkhitaryan ameonekana kupwaya sana.

Mchezo wao dhidi ya Liverpool wakati Phellipe Coutinho akigusa mpira mara 68, Mkhitaryan aligusa mpira mara 44, tatizo likajotokeza tena kwa Chelsea wakati Eirikssn akigusa mpira mara 88, Mkhitaryan aligusa mara 44.

Kiujumla Henrikh Mkhitaryan katika michezo ambayo United wamecheza na timu zilizoko top 6 Mualmernia huyo amecheza dakika 795 na katika dakika hizo Mualmernia huyo amegusa mpira mara 614.

Lakini Kelvin De Bruyne (KDB) katika dakika hizo dhidi ya timu za top 6 amegusa mpira mara 1049, David Silva amegusa mara 1065, Erikssen amegusa mara 840 na Mkhitaryan anaonekana amepoteza na namba 10 wa timu pinzani.

Tofauti na alivyokuwa Dortmund na tofauti na namba 10 wenzake Mkhitaryan anaonekana pamoja na kasi aliyonayo lakini anashindwa kufika kwa muda mipira inapofika na ndio maana hata nafasi kwa mshambuliaji wa mwisho anashindwa kutengeneza.

Rekodi zinaonesha msimu huu Kelvin De Bruyne ametengeneza nafasi nyingi 32 na mashuti 26 idadi ya mashuti ambayo ni mara mbili ya Henrinkh Mkhitaryan ambaye amepiga mashuti 13 tu.

Msimu huu Mkhitaryan ana assists tano ambazo zimepatikana katika mechi tatu za mwanzo za Manchester United huku mechi mechi mbili kati ya hizo zikiwa dhidi ya klabu ambazo ziko tatu ya mwisho wa msimamo Epl.

Inaonekana ni muda sasa kwa Mourinho kumpa nafasi Juan Mata na kumuamini kwani wakati United wakiwaza jinsi ya kuwazuia namba 10 wa timu pinzani kubwa, wenzao hawana uwoga hata kidogo na namba 10 wa United.

Viewing all 9000 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>