Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all 9000 articles
Browse latest View live

Ukame wa penati unaoitokea Real Madrid haujawahi kutokea kwa miaka 36, yatajwa kuwa sehemu ya anguko la Cr7

$
0
0

Kati ya sababu ambayo imeshaanza kuongelewa kama chanzo cha kutofanya vizuri kwa Real Madrid msimu huu ni ukosefu wa penati, michezo 11 ya ligi kuu La Liga Los Blancos hawajapewa penati.

Mara ya mwisho kwa Real Madrid kucheza michezo 11 bila kupewa penati ilikuwa msimu wa mwaka 1980/1981 na kuanzia hapo Real Madrid wamekuwa wakipewa penati nyingi kula msimu.

Kuanzia msimu wa mwaka 1982 Real Madrid hawajawahi kucheza mechi 11 bila penati ambapo msimu uliopita katika kipindi kama hiki tayari Real Madrid walikuwa wameshapewa pigo la penati mara mbili.

Msimu wa mwaka 2015/2016 Real Madrid almanusra wakose penati lakini walifanikiwa kupata penati moja katika michezo 11 lakini msimu wa 2014/2015 ndio waliweka rekodi kwani walipata penati 5 katika mechi 11.

Kuanzia msimu wa 2011/2012 hadi kufikia msimu wa mwaka 2014/2015 Real Madrid hawajawahi kupewa chini ya penati 4 ndani ya mechi 11 za mwanzo na wakipata penati 19 katika misimu minne mechi 11 za mwanzo.

Tangu Cristiano Ronaldo ajiunge na Real Madrid mwaka 2009 hawajawahi kukaa muda mrefu hivi bila kupata penati na sasa ukame wa mabao unaomuandama Cr7 unatajwa kusababishwa na ukame wa penati.


HOFU: Majeraha huenda yakamweka nje Farid hadi mwisho wa msimu

$
0
0

Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Farid Musa anayevheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Tenerufe nchini Hispania amepata majeraha ya goti (knee ligament).

Farid mwenyewe amethibitisha kuwa majeruhi huku kesho akitarajiwa kwenda jijini Madrid kukutana na madaktari bingwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

“Ni kweli nimepata majeraha ya goti, kesho nakwenda Madrid kukutana na doctor kwa ajili ya uchunguzi zaidi”-Farid.

Endapo itathibitika ni majeraha makubwa ya goti, basi huenda akakaa nje ya uwanja hadi mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa hii imekuja siku moja baada ya nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta kupata majeraha yatakayomuweka nje kwa kipindi cha miezi sita (6).

Ukame wa magoli La Liga: Messi anaokoa jahazi, CR7, Suarez, Griezmann chali

$
0
0

LaLiga wanapitia katika kipindi cha ukame miongoni mwa wafungaji magoli – lakini kuna mwanaume mmoja anabakia kuwa na katika kilele cha ufungaji katika msimu wa 2017/18: Lionel Messi.

Ukiangalia msimamo wa ufungaji baada ya michezo 11 utamuona La Purga akiongoza kwa kuwa na magoli 12, na baada ya Messi anafuatia Simeone Zaza akiwa na magoli 9 na Cedric Bakambu ana magoli 8, huku Rodrigo Moreno na Antonio Sanabria akifuatia na magoli 7.

Hawa ni wachezaji wazuri na wanavitumikia vilabu vyenye sifa kubwa, lakini hawapo katika daraja la juu kabisa duniani la wachezaji bora. Kama utahitaji kuwapata wachezaji wa daraja la dunia kwenye listi ya wafungaji wa La Liga, itakubidi urudi chini kwenye msimamo.

Cristiano Ronaldo, Karim Benzema na Kevin Gameiro wote wamefunga goli moja moja msimu hui, Antonie Griezmann, Bale na Wissam Ben Ydder wakiwa wamefunga magoli mawili kila mmoja – huku Suarez akiwa amefunga magoli 3 tu.

Hivyo wachezaji hao 7 kwa ujumla wamefunga magoli 12, namba sawa na ile ya magoli aliyofunga Lionel Messi pekee yake.

Msimu uliopita, CR7 alikuwa amefunga magoli 5 katika mechi 8 za mwanzo alizoitumikia Real Madrid, idadi ambayo kwa kiwango ilionekana kuwa ndogo.

Benzema alikuwa amefunga magoli 3, Griezmann alikuwa ameweka kambani magoli 6. Aliyeporomoka zaidi ni Luis Suarez ambaye msimu uliopita baada ya mechi 11 tayari alikuwa amefunga 8.

Chuji amefungiwa ligi daraja la kwanza

$
0
0

Mechi namba 19 Kundi B (Coastal Union 1 v Polisi Tanzania 1). Wachezaji Athuman Idd ‘Chuji’ wa Coastal Union na Shabani Stambuli wa Polisi Tanzania wamesimamishwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kila mmoja kwa kosa la kupigana uwanjani. Adhabu dhidi yao ni kwa mujibu wa Kanuni ya 37(3) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.

Mechi namba 16 Kundi A (Friends Rangers 1 v African Lyon 1). Klabu ya African Lyon imepewa Onyo Kali kwa timu yake kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi ikiwa na maofisa pungufu, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Mechi namba 20 Kundi A (Mgambo JKT 1 v Mshikamano 0). Klabu ya Mgambo JKT imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuingia uwanjani baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo kupulizwa. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.

Mechi namba 21 Kundi A (Kiluvya United 2 0 v Mshikamano 1). Klabu ya Kiluvya United imepigwa faini ya sh. 100,000 (laki moja) kwa kutohudhuria kikao cha maandalizi ya mechi, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Faini hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Mechi namba 24 Kundi A (Friends Rangers 0 v JKT Ruvu 3). Klabu ya Friends Rangers imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kusababisha mchezo kusimama kwa dakika tano baada ya kumpiga jiwe Mwamuzi Msaidizi. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.

Mechi namba 28 Kundi A (Mgambo JKT 2 v Ashanti United 1). Klabu ya Mgambo JKT imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika 13. Adhabu hiyo ni utekelezaji wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.

Mechi namba 15 Kundi B (KMC 1 v Mbeya Kwanza 0). Mchezaji Stephano Mwasika wa KMC amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa kumpiga kiwiko kwa makusudi mchezaji wa Mbeya Kwanza. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 37(3) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.

Mechi namba 17 Kundi B (JKT Mlale 1 v Polisi Dar 1). Klabu ya JKT Mlale imepewa Onyo Kali kwa timu yake kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi ikiwa na maofisa pungufu, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Klabu ya Polisi Dar imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika 15. Adhabu hiyo ni utekelezaji wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.

Mechi namba 21 Kundi B (Mbeya Kwanza 0 v JKT Mlale 0). Klabu ya JKT Mlale imepigwa faini ya sh. 100,000 (laki moja) kutokana na timu yake kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi ikiwa na maofisa pungufu, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Mechi namba 23 Kundi B (Mawenzi Market 0 v Mufindi United 1). Klabu ya Mawenzi Market imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kusababisha mchezo kusimama kwa dakika nne baada ya kumpiga jiwe Mwamuzi Msaidizi Namba Mbili. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.

Mechi namba 13 Kundi C (JKT Oljoro 1 v Toto Africans 0). Klabu ya Toto Africans imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi ikiwa na maofisa pungufu, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Mechi namba 17 Kundi C (Dodoma FC 1 v JKT Oljoro 0). Mwamuzi Said Pambalelo amepewa Onyo Kali kwa kutochukua hatua dhidi ya wachezaji wa JKT Oljoro waliokuwa wakifanya vitendo ambavyo ni kinyume na kanuni za mpira wa miguu. Adhabu dhidi yake ni kwa mjuibu wa Kanuni ya 38(5) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.

Mechi namba 26 Kundi C (Transit Camp 1 v Biashara United Mara 0). Klabu za Transit Camp na Biashara United Mara kila moja imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na timu zao kuonesha vitendo vinavyoashiria imani za ushirikina katika mechi hiyo wakati zikiingiz uwanjani. Adhabu dhidi yao imezingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.

Klabu ya Transit Camp pia imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuingia uwanjani baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo kupulizwa kwa lengo la kutaka kumpiga Mwamuzi. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.

Mechi namba 27 Kundi C (Pamba SC 1 v Rhino Rangers 0). Klabu ya Pamba imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi ikiwa na maofisa pungufu, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Nayo klabu ya Rhino Rangers imepewa Onyo Kali kutokana na washabiki wa timu yake kutoa lugha za matusi wakati mchezo huo ukiendelea.

Kocha mpya Simba apewa onyo kali, mashabiki waiponza Yanga

$
0
0

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imepitia ripoti za michezo yote ya Ligi Kuu Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja Pili (SDL) na kufanya uamuzi ufuatao.

Mechi namba 54 (Simba 4 v Njombe Mji 0).

Klabu ya Simba imepewa Onyo Kali kutokana na Kocha wake Msaidizi Masoud Djuma kuanza kufundisha bila kuwa na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini. Uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 40(13) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha.

Pia klabu hiyo imetakiwa kufikia Novemba 10 iwe imewasilisha Bodi ya Ligi nakala ya vibali hivyo, na kukumbushwa kuwa mahitaji ya nyaraka hizo ni kwa mujibu wa Kanuni za Ligi, lakini pia sheria za nchi.

Vilevile klabu ya Simba imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa timu yake kuwasilisha orodha ya wachezaji wake (team match list) nje ya muda wa kikanuni. Kitendo cha timu hiyo ni kukiuka Kanuni ya 14(2k) ya Ligi Kuu. Adhabu dhidi yao imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu.

Klabu ya Njombe Mji imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kuonesha vitendo vinavyoashiria imani za ushirikina katika mechi hiyo wakati ikiwasili uwanjani. Adhabu dhidi ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.

Mechi namba 56 (Stand United 0 v Yanga 4). Klabu ya Stand United imetozwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kutokana na golikipa wao kuvaa jezi yenye namba tofauti na ile iliyosajiliwa, kitendo ambacho ni ukiukaji wa Kanuni ya 60(11) ya Ligi Kuu kuhusu Usajili. Adhabu dhidi yao imezingatia Kanuni ya 60(12) ya Ligi Kuu.

Mechi namba 57 (Azam FC 1 v Mbeya City 0). Mwamuzi Shakaile Ole Yanga Lai amefungiwa miezi mitatu kwa kutoripoti na kuchukua hatua dhidi ya kitendo cha Kipa Owen Chaima wa Mbeya City kumpiga kofi mshambuliaji wa Azam FC. Kitendo cha Mwamuzi huyo ni ukiukaji wa Kanuni ya 38(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi wakati adhabu dhidi yake imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 38(5) ya Ligi Kuu.

Naye Kamishna wa mechi hiyo, David Lugenge amefungiwa miezi mitatu kwa kushindwa kuripoti tukio hilo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 39 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Kamishna.

Mechi namba 58 (Yanga 1 v Simba 1). Klabu ya Yanga imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na mashabiki wake kurusha uwanjani chupa zinazosadikiwa kuwa na mikojo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 42(1) kuhusu Udhibiti wa Klabu.

Real Madrid wapiga hodi Manchester United na safari hii sio De Gea tena

$
0
0

Miamba ya nchini Hispania Real Madrid baada ya kumkosa golikipa wa Manchester United David De Gea sasa wamerudi tena katika klabu hiyo kwa ajili ya kujaribu kufanya usajili wa mchezaji mwingine.

Mkataba wa Juan Mata na Manchester United unakaribia kuisha hivyo ni wazi United wanaweza kuvutiwa na kiasi cha pesa ambacho kitatolewa na Madrid kama ada ya kumnunua Juan Mata.

Juan Mata pia anaweza kuvutiwa na dili la kurudi nchini Hispania kwani msimu huu amekuwa hapewi dakika 90 uwanjani huku akifanikiwa kuanza katika michezo 11 kati ya 12 msimu huu.

Toka Juan Mata acheze katika mchezo ambao Manchester United walifungwa bao 2 kwa 1 na Huddersfield amekuwa akikaa nje huku mchezo pekee aliocheza baada ya mchezo huo ni mechi ya Champions League dhidi ya Benfica.

Historia kati ya Jose Mourinho na Juan Mata sio nzuri kwani mwanzo Jose alimuuza akiwa Chelsea na sasa inaonekana haitakuwa ngumu kwa kocha huyo wa United kumuuza tena kiungo huyu wa Hispania.

Samatta kufanyiwa upasuaji, hayupo kwenye mipango ya Stars

$
0
0

Sasa ni rasmi, nahodha wa Taifa Stars ya Tanzania inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, Mbwana Ally Samatta, atakosa mchezo kati Tanzania na Benin utakaofanyika Novemba 12, 2017 kwa sababu ya majeraha ya goti.

Taarifa kutoka kwa matatibu wa Genk ya Ubelgiji, zinasema kwamba Mbwana Samatta anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mdogo na mpaka kupona, madaktari wamesema itamchukua wiki nane ili kurejea uwanjani.

Kocha wa Taifa Stars, Salum Shabani Mayanga amepokea taarifa hiyo na kusema haijawa bahati kwa Stars, lakini atapanga kikosi chake vema kwa wachezaji atakaokuwa huko Benin akiwamo Abdi Banda na Farid Mussa.

Wachezaji watakaosafiri ni Aishi Manula, Peter Manyika, Gadiel Michael, Boniphas Maganga, Kelvin Yondani, Nurdin Chona, Himid Mao, Hamis Abdallah, Raphael Daudi, Mohamed Issa, Jonas Mkude, Mudathir Yahya, Simon Msuva, Shiza Kichuya, Faridi Mussa,  Ibrahim Ajib, Mbaraka Yusuph na Elias Maguli.

Lionel Messi azitaja timu tishio kombe la dunia lakini ataja timu anayoihofia zaidi

$
0
0

Pamoja na kuchelewa kufika lakini timu ya taifa ya Argentina ilifanikiwa kufudhu kwa fainali za kombe la dunia zitakazochezwa mwakani nchini Urusi na shukrani zimeuendee Lioneil Messi aliyewabeba katika mchezo wa mwisho.

Lakini wakati wakijiandaa kushiriki michuano hiyo ya kombe la dunia, mshambuliaji huyo hatari wa klabu ya Barcelona tayari kichwani ana orodha ya timu ambazo anaamini zitakuwa tishio kwenye michuano hiyo.

Messi anaamini timu ya taifa ya Ujerumani ambao ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo ni kati ya timu anazozipa nafasi kubwa bila kusahau Ufaransa, Brazil na timu ya taifa ya Hispania.

Lakini Lioneil Messi pamoja na kuzikubali timu hizo lakini kuna timu moja anayoiogopa zaidi nayo ni timu ya taifa ya Hispania ambayo amekiri kwamba hatamani kabisa kukutana nao katika michuano hiyo.

Lioneil Messi anaamini kwa sasa timu ya taifa ya Hispania ndio timu bora na wanacheza vizuri sana hivyo itakuwa ngumu kupambana nao haswa katika michuano mikubwa kama kombe la dunia.

Kuhusu kufudhu katika michuano hiyo kwa tabu sana Messi amesema aliamini watakwenda Urusi hata kama itachukua muda na ndio maana siku ya mchezo aliwaambia wachezaji wenzake watulie wanaelekea Urusi.


Sahau kuhusu PSG na Man City, hii ndio timu yenye safu kali ya ushambuliaji ulaya

$
0
0

Ilikuwa ikitegemewa kwamba klabu ya Paris Saint Germain ingekuwa moja ya timu ambayo ingekuwa kiwembe kwenye suala la ufungaji msimu huu, lakini hakuna aliyedhani Lyon FC ndio ingekuwa klabu ambayo ingekuwa na safu kali ya ushambuliaji kwenye ligi 5 kubwa barani ulaya.

Nabir Fekir, Mariano na Memphis Depay wamekuwa kwenye kiwango bora msimu huu, wamefunga jumla ya magoli 26 katika Ligue 1, idadi kubwa zaidi ya ile ya washambuliaji wa PSG – Kylian Mbappe, Edinson Cavani na mchezaji ghali zaidi duniani – Neymar ambao kwa ujumla wamefunga magoli 24 katika ligi.

Mariano amewasili kutoka Real Madrid na tayari ameweza kufiti vizuri ndani ya mfumo wa timu, uwezo wake wa kupangua ngome na kutengeneza mianya kwa Fekir kuitumia

Wafungaji bora wa Lyon msimu wa 2017/18

1 Fekir: 11 goals

2 Mariano: 9 goals

3 Depay: 6 goals

Manchester City wamekuwa wakisifiwa kuwa klabu inayocheza soka la kuvutia zaidi kwa sasa chini ya Pep Guardiola na timu yao imefunga zaidi ya magoli 50 kwenye mashindano yote msimu huu.

Hata hivyo Safu ya ushambuliaji ya City inayoundwa Sergio Aguero, Gabriel Jesus na Raheem Sterling wamefunga magoli 22 mpaka sasa katika Premier League pekee.

Ushindi wa Lyon wa 5-0 dhidi ya wapinzani wao Saint Etienne ulikuwa ni mjumuisho wa kiwango kizuri cha Lyon msimu huu.

Wakicheza katika uwanja wa ugenini, safu ya ushambuliaji ya Lyon ilionyesha wazi makali yao – wakifunga magoli 4 kati ya hayo matano.

Fekir alifunga magoli mawili, Mariano aliongeza moja, Memphis akafunga lingine na Oscar Garcia akaweka msumari wa 5.

Hata hivyo Lyon sio timu inayoongoza kwa kufunga magoli mengi nchini Ufaransa katika mashindano yote, wamefunga magoli 32 kwa ujumla – washambuliaji wake wakichangia 81.25% ya magoli hayo.

Utegemezi mkubwa wa wachezaji hawa watatu unaweza kuleta tatizo endapo mmoja wao atapata majeruhi, hata hivyo vijana hawa watatu kwa sasa wanaibeba timu yao mabegani na huenda wakaendelea kuweka rekodi msimu huu.

Muuaji wa Yanga kaitwa Zanzibar Heroes

$
0
0

Na Abubakar Khatib ‘Kisandu’, Zanzibar

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), Hemed Suleiman ‘Morocco’ amemuongeza kwenye kikosi Mshambuliaji wa Lipuli ya Iringa Seif Rashid Abdallah ‘Karihe’ ili kuzidi kuipa nguvu timu hiyo itakayokwenda Kenya katika Mashindano ya CECAFA Challenge Cup yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25 na kumalizika Disemba 9, 2017.

Karihe ndio mchezaji wa kwanza kufunga goli dhidi ya Yanga msimu huu kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara ambapo alifunga bao kwenye mechi yao ya ufunguzi wa msimu huu August 27, 2017 Yanga lipotoka sare ya kufungana 1-1 na Lipuli kwenye uwanja wa Uhuru, Dar.

Katika uteuzi wa awali wa wachezaji 30 Karihe hakuitwa lakini kocha Morocco amelazimika kumuongeza mshambuliaji huyo na atakuwa mchezaji wa 31 kuitwa katika kikosi cha awali huku Morocco akisema si kosa kwa timu ya Taifa kupunguza au kuongeza mchezaji wakati wowote tu ikiwa bado haijaenda katika Mashindano.

“Hii ni timu ya Taifa wakati wowote unamwita mchezaji au unamtoa kutokana na mahitaji yako, nimelazimika kumuongeza Karihe kwasasa ataungana na wenzake 30 wale wa awali”- Morocco.

Karihe ambae ni mchezaji wa zamani wa Azam FC ataungana na wenzake Ahmed Ali ‘Salula’ (Taifa ya Jang’ombe), Nassor Mrisho (Okapi), Mohammed Abdulrahman ‘Wawesha’ (JKU), Abdallah Haji ‘Ninja’ (Yanga), Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed ‘Sangula’ (Jang’ombe Boys), Adeyum Saleh ‘Machupa’ (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Abubakar Ame ‘Luiz’ (Mlandege), Issa Haidar ‘Mwalala’ (JKU),  Abdulla Kheir ‘Sebo’ (Azam) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang’ombe).

Wengine ni Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang’ombe), Mudathir Yahya (Singida United), Omar Juma ‘Zimbwe’ (Chipukizi), Mohd Issa ‘Banka’ (Mtibwa Sugar), Amour Suleiman ‘Pwina’ (JKU), Mbarouk Marshed (Super Falcon), Ali Yahya (Academy Spain), Hamad Mshamata (Chuoni), Suleiman Kassim ‘Selembe’ (Majimaji), Kassim Suleiman (Prisons), Matteo Anton (Yanga), Ali Badru (Taifa ya Jang’ombe), Feisal Salum (JKU), Salum Songoro (KVZ), Khamis Mussa ‘Rais’ (Jang’ombe boys), Mwalimu Mohd (Jamhuri) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).

Manchester City ndio kikosi ghali zaidi ulimwenguni, angalia nafasi timu yako ilipo

$
0
0

Utafiti uliofanya na shirika la CIES Football Obsevatory unaonesha vilabu vya nchini Uingereza Manchester City na Tottenham ndio vilabu vinavyoongoza kuwa na kikosi chenye thamani kubwa ulimwenguni.

Ripoti ya utafiti huo inasema Man City kikosi chao cha kwanza kuna wachezaji wanne ambao kwa sasa kama wataamua kuwauza baasi thamani yao lazima itakuwa ni kuanzia kiasi cha €100m.

Mchezaji wa Manchester City ambaye kwa sasa ukimuweka sokoni ana thamani kubwa zaidi ni Kelvin De Bruyne ambaye mauzo yake sokoni yanaweza kuwa €145m akifuatiwa na Leroy Sane €119.5m.

Raheem Sterling thamani yake imepanda hadi kufikia €118.2m huku kuna Gabriel Jesus ambaye thamani yake sokoni ni €107m ambalo kwa ujumla pamoja na wachezaji wengine Manchester City wana thamani ya €1.19b.

Tottenham Hotspur  kikosi chao thamani yake ni €1.17bn huku Harry Kane pekee thamani yake ni €185.6m, Delle Ali €181.7m na hii inamaanisha kwenye 3 bora ya wachezaji wenye thamani duniani Tottenham ina wachezaji wawili.

Ukimuacha Ali na Kane yupo Eriksen €104.9m yupo Heung Son Min €67.5m. Barcelona wanafuatia katika nafasi ya 3 wana Lioneil Messi €117.3m wana Luis Suarez 133.6m na kwa ujumla kikosi chao kina thamani ya €1.13bn.

Chelsea wapo katika nafasi ya nne ambapo kikosi chao kina thamani ya €1.04bn huku Manchester United wakiwa ya 5 na £812.9bn lakini Romelu Lukaku(€165m) ametajwa kuwa na thamani kubwa kuliko Messi, Ronaldo na Hazard.

Real Madrid wako nafasi ya 6 huku bei ya Cr7 ikishuka hadi kufikia €96m akipitwa hadi na Mohamed Salah ambaye yeye na Liverpool wako nafasi ya 7 lakini Mo Salah mwenyewe ana thamani ya €101m.

Ripoti hii ya CIES mara nyingi huwa inaangalia viwango vya wachezaji wanapokuwa uwanjani lakini vile vile umri huwa ni kigezo kikubwa na kile wanachofanya uwanjani katika kipindi ambacho ripoti inaandikwa.

Ripoti hiyo hapo juu inaonesha wachezaji 10 ghali kutoka katika kila klabu ambayo ipo 10 bora ya ripoti ya CEIS huku Luis Suarez akiiwakilisha Barcelona kutokana na thamani yake kuwa kubwa kwa sasa kuliko Lioneil Messi.

Wachezaji 10 walioenda EPL kwa mbwembwe wakafeli

$
0
0

10.George Weah. Wakati anatoka Ac Milan kuja Chelsea mwaka 2000 kila mtu aliamini wapinzani wa Chelsea wanakwenda kuumia kwani Weah alishakuwa mchezaji bora wa dunia, lakini ndani ya miezi mitano alifunga mabao mawili tu Epl akapelekwa Man City.

9.Mario Jadel. Wanasema huyu alikuwa akionekana kama Pele mpya kwani akiwa Gremio alifunga mabao 67 katika mechi 73 lakimi alipofika Bolton alifunga mara 3 tu katika mechi 12.

8.Radamel Falcao. Mashabiki wa United walitamba sana wakati akienda United kwa ada ya £46m lakini alichokifanya walishangaa alofunga mabao 4 katika mechi 29 kabla kwenda Chelsea alikofunga 1 katika mechi 12 lakini alipokuwa Porto alifunga mabao 72 katika michezo 87, Monaco 13 katika michezo 20.

7.Paulo Futre. Hii ilikuwa 1996 huyu alianza cheza timu ya taifa Ureno akiwa na miaka 17 tu, mwaka 1987 hadi 1989 alishinda kombe la Ureno mara mbili lakini aliposajiliwa West Ham alicheza michezo 9 tu na kiwango alichoonesha kilitosha kukatisha mkataba wake.

6.Branco. Mwaka 1994 alikuwa na kikosi cha Brazil kilichoshinda kombe la dunia na mwaka 1996 klabu ya Middlesbrough walimsaini, alipokuwa Middlesbrough alipwaya sana kiasi kwamba baada ya michezo 11 tu mwaka 1997 waliamua kuachana naye.

5.Juan Sebastian Veron. Kama ilivyo kwa Falcao, Manchester United wanawapa Chelsea mzigo mwingine, wakati Veron anakuja United alianza vyema sana lakini baada ya mda alianza kuwa flop na inatajwa ugomvi wake na SAF ndio ulichangia akauzwa Chelsea 2003 ambapo ndiko aliboronga zaidi.

4.Andriy Shevchenko. Hakuna kitu mashabiki wa United, Arsenal na Liverpool waliogopa kama usajili wa Chenko kwenda Chelsea, wataachaje ogopa wakati mshambuliaji huyu alifunga mabao 173 alikotoka? Lakini huwezi amini akiwa na Chelsea alizima kwani michezo 76 alifunga mabao 22.

3.Davor Suker. Kombe la dunia 1998 alichukua kiatu cha dhahabu na alishinda La Liga 1997 na Champions League 1998, ilipofika mwaka 1999 Madrid walimchukua Anelka na wakawapa Arsenal Davor Suker lakini akafunga mabao 11 katika mechi 40 kabla ya Arsenal hawahampeleka West Ham mwaka 2000 alikofunga mabao 3 tu.

2.Angel Di Maria. Usajili mwingine uliojaa mbwembwe sana ni huu, wakati anakuja Manchester United mwaka 2014 kila mtu aliamini moto utawaka, lakini mwaka uliofuta Van Gaal hakuona tabu kumuacha aondoke kwani michezo yake 31 alifunga jumla ya mabao 4 tu.

1.Fernando Morientes. Liverpool walimnunua mwaka 2005 akitokea Madrid alikoshinda Champions League mara 3, mashabiki wa Liverpool walitegemea makubwa kutoka kwake lakini katika michezo 61 aliyoichezea Liverpool alifunga mabao 12 tu.

Chirwa kawamwaga Ajib, Nyoni

$
0
0

Mshambuliaji wa Young Africans ya Dar es Salaam, Obrey Chirwa amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Oktoba wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2017/2018.

Chirwa raia wa Zambia alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, beki Erasto Nyoni wa Simba na mshambuliaji Ibrahim Ajibu pia wa Young Africans alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za VPL zinazotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha waliopo viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa msimu huu.

Mshambuliaji huyo alitoa mchango mkubwa kwa Young Africans mwezi huo ikipata pointi saba katika michezo mitatu iliyocheza na kupanda katika msimamo wa ligi kutoka nafasi ya sita iliyokuwepo mwezi Septemba hadi ya pili mwishoni mwa Oktoba.

Young Africans iliifunga Kagera Sugar mabao 2-1 Uwanja wa Kaitaba, Bukoba,  ambapo Chirwa alifunga bao moja na kutoa pasi ya mwisho ya bao moja, pia Yanga iliifunga Stand United mabao 4-0 Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, ambapo Chirwa alifunga bao moja na kutoa pasi ya mwisho ya bao moja.

Kiwango cha mchezaji huyo kilionekana pia katika mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba uliofanyika Oktoba 28, 2017 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1. Bao la Yanga lilifungwa na Chirwa, hivyo kwa mwezi huo alifanikiwa kuwa na kiwango cha juu katika kila mchezo ikiwa ni pamoja na kufunga.

Kwa upande wa Erasto naye alitoa mchango mkubwa kwa Simba uliowezesha timu hiyo kupata pointi nane katika michezo minne iliyocheza, akitoa pasi za mwisho za mabao nne, ambapo Simba ilishinda michezo miwili na kutoka sare miwili, huku Ajibu akitoa mchango mkubwa kwa Yanga ikiwa ni pamoja na kufunga mabao matatu na kutoa pasi ya mwisho ya bao moja.

Wachezaji wengine ambao tayari wameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa VPL msimu huu ni mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze (Septemba).

Kampuni ya Vodacom, ambao ndiyo wadhamini wa ligi hiyo ina utaratibu wa kuwazadiwa wachezaji bora wa kila mwezi, huku pia mwisho wa msimu kukiwa na tuzo mbalimbali zinazohusu ligi hiyo, ambapo msimu wa mwaka 2016/2017 kulikuwa tuzo 16 zilitolewa kwa washindi wa kada mbalimbali. Chirwa atazawadiwa Sh milioni moja kwa kuibuka Mchezaji Bora wa Oktoba.

Kuelekea Urusi 2018 bado nafasi 4 Ulaya, 3 Afrika, 2 Amerika/Asia, nani kuzichukua?

$
0
0

Katika bara la Ulaya zimebaki timu 4 tu ambazo zitacheza michezo yao wiki hii ili kupata timu itakayoenda kombe la dunia, bara la Afrika bado tatu na mbili kutoka  bara la Amerika na Asia, na hii ndio michezo itakayoamua timu hizo 9.

Crotia vs Ugiriki. Sio mchezo rahisi kwa Luka Modric na wenzake kwani Ugiriki wameshafudhu kwenye michuano hii mara 5 na wana uzoefu, Alhamisi utapigwa mchezo wa kwanza kabla ya kurudiana siku ya Jumapili.

N.Ireland vs Switzerland. Northern Ireland kama wakafanikiwa kuwafunga Switzerland katika mchezo huu, watakuwa wamefudhu kwa mara ya kwanza katika michuano hii tangu wafanye hivyo mwaka 1986.

Sweden vs Italy. Itakuwa aibu kwa taifa bingwa mara 4 wa michuano hii timu ya taifa Italia kama watashindwa katika hatua hii ya mtoano, Alhamisi Italia watasafiri hadi Sweden kabla ya kurudi Millan siku ya Jumapili kuamua hatma yao.

Dermanrk vs Ireland. Mechi ya kutafuta heshima kwa pande zote mbili lakini tofauti na wengine nu kwamba hawa wataanza mchezo wao wa kwanza siku ya Jumamosi November 11 kabla ya kurudiana siku ya Jumanne November 13.

New Zealand Vs Peru. Toka mwaka 1982 timu ya taifa ya Peru hawajawahi kwenda kombe la dunia na Jumamosi hii wanakwenda kukabiliana na New Zealand huku nahodha wao Paolo Guerrero akiwa hayupo.

Hondurus vs Australia, Australia watakuwa na kibarua kigumu kwani timu ya taifa ya Hondurus wana rekodi nzuri katika kwenda kombe la dunia ambapo mara mbili mfululizo wamefudhu, na Jumamosi Hondurus wakiwa nyumbani watajaribu kufudhu kwa mara ya tatu.

AFRICA, Katika bara la Africa tayari timu mbili Nigeria na Misri wameshatangulia katika michuano hiyo itakayopigwa mwakani nchini Urusi na sasa kumebaki timu tatu ili kukamilisha idadi ya timu tano.

Group A. Tunisia wanaongoza kundi kwa tofauti ya alama 3 na wanahitaji suluhu  vs Libya kwenda Urusi lakini wakipoteza mechi yao huku DR Congo wakimfunga Guinea baasi mshindi ataamuliwa kwa tofauti ya mabao.

Group B. Morocco wanaongoza kundi wakifuatiwa na Ivory Coast, lakini Morocco wanakwenda Abidjan kuwakabili Ivory Coast huku Ivory Coast wakihitaji alama zote tatu ili kwenda katika michuano ya kombe la dunia.

Group D. Kimbembe kimo hapa kwani timu zote nne zinaweza kufudhu kombe la dunia, Novemeber 10 Senegal wataikaribisha Bafanabafana na Senegal anahitaji ushindi ili kwenda kombe la dunia.
Lakini endapo Senegal na Bafanabafana watasuluhi mechi moja na Senegal akapoteza nyingine baasi mshindi katika mechi kati ya Cape Verde na Burkina Faso anaweza kwenda hadi nafaso ya kwanza kwa tofauti ya mabao huku Burkina Faso wakiwa katika nafasi nzuri kweny hili.

Mikel Obi aelezea jinsi Chelsea walivyomnyakua toka katika mikono ya Alex Ferguson

$
0
0

Mwaka 2005 wakati John Obi Mikel akijiunga na klabu ya Chelsea kulikuwa na mambo mengi yanayozunguka usajili huo, kubwa ikiwemo taarifa ya Obi kusaini vilabu viwili vya Manchester United na Chelsea.

Lakini Obi Mikel mwenyewe amekiri kwamba nguvu kubwa walioionesha Chelsea ikiongozwa na kocha Jose Mourinho pamoja na boss wa klabu hiyo Roman Abromovich vilimfanya kusema hapana kwa SAF.

Haikuwa rahisi kwa Obi kumtolea nje SAF kwani walikuwa na mahusiano ya karibu sana huku Fergie akimtambulisha Obi kwa manguli akiwemo Roy Keane na kumuahidi kuwa tajiri akianza kuichezea Manchester United.

Wakati Ferguson akimpa makaratasi ya awali Obi na akasaini kumbe kulikuwa na mpango wa siri wa kumnunua Obi uliokuwa ukifanywa na Chelsea huku tayari wakijua Obi anakaribia kumalizana na Chelsea.

Inasemekana wakati Obi akijiandaa kwenda Carington kumalizana na United, Chelsea walituma msafara wa magari 6 kwenda tu kumshawishi Mnigeria huyo aachane na United na asaini kwao.

Obi anakiri kwamba msafara huo ulikuwa kama wa kijeshi kwani alikuwa akipakizwa kwenye gari moja anamsikia dereva anawasiliana na walioko gari lingine kupoekea maelezo ya nini kifanyike.

Na ndipo alikutana na Jose Mourinho kwa mara ya kwanza na Jose alimuambia Obi kwamba bosi wa Chelsea anamhitaji sana kwenye timu yake na akapewa uhakika wa kupata namba katia timu ya Chelsea.

Obi anasema alivutiwa sana na Chelsea na akabadili mawazo akaamua kumtosa Ferguson jambo ambalo Obi anakiri kwamba lilimkera sana SAF kwani aliamini hakuna mchezaji ambaye angeweza kumpiga chini.

Obi anasema sio tu Chelsea waliojaribu kumuiba toka United lakini pia Barca, huku pia kuna wakala alikwenda kwake na Briefcase lenye usd 70,000 kisha akamuonesha Obi ili asaini katika klabu yake (Obi hakumbuki jina la klabu).

Obi ameitumikia Chelsea kwa misimu 11 ya ligi na kufanikiwa kushinda Champions League, Europa League, Epl mara mbili, FA Cup mara nne na kombe la ligi mara mbili na kwa sasa anakipiga Tianjin Teda ya nchini China.


Rekodi 8 ambazo Messi bado hajavunja: CR7 kizingiti kwenye rekodi 3

$
0
0

Lionel Messi ametimiza mechi 600 akiwa na FC Barcelona Jumamosi iliyopita wakati Barca walipoifunga Barcelona 2-1 katika La Liga. Tayari ameshavunja na kuweka rekodi kadhaa, lakini bado hizi hapa rekodi 8 hajafanikiwa kuzivunja au kuziweka…..

All time Top goalscorer katika Champions League: Mpaka sasa Cristiano Ronaldo mwenye magoli 110 anaongoza, Messi akifuatia na magoli 97. Hata hivyo CR7 amemzidi Messi mika miwili na huenda La Purga akafanikiwa kuivunja rekodi hii misimu kadhaa ijayo wakati CR7 akiwa tayari muda umemtupa mkono.

Mchezaji mwenye makombe mengi katika historia ya soka: Messi tayari ameshashinda makombe 30, idadi sawa na Gerard Pique. Ryan Giggs ameshinda makombe 36 na United, Victor Baia alishinda vikombe 35, Andres Iniesta makombe 32, Gary Neville akiwa na United, Dani Alves (PSG, ex Barca), wote walishinda makombe 31.

Mchezaji mwenye vikombe vingi vya ulaya (UCL/EuropeanCups): Paco Gento wa Madrid alishinda vikombe 6, Di Stefano, Jose Maria Zarraga (wote Real Madrid) na Paolo Maldini (AC Milan) wote wana rekodi ya kushinda makombe 5, wakati Messi, Ronaldo, Iniesta na Pique wote wakiwa wameshinda mara 4.

Mchezaji mwenye vikombe vingi vya ulaya (UCL/SuperCups): Dani Alves, Paulo Maldini na Arie Haan (Ajax) wote wameshinda kwa ujumla makombe 9 kila mmoja. Kwa sasa Messi tayari ameshinda 7, manne ya Champions League na matatu ya Super Cups, idadi sawa na Pique, Iniesta na Cristiano.

Mfungaji bora wa klabu moja: Messi tayari amefunga magoli 523 katika mechi 600, Gerd Muller alifunga magoli 525 katika mechi 563 alizoitumikia Bayern. Anayeshikilia rekodi mpaka sasa Josef Bican, ambaye kati ya mwaka 1937 na 1948 alifunga magoli 534 katika mechi 274 na klabu ya Slavia Prague. Pele alifunga magoli 643 katika mechi 659 akiwa na Santos kutoka 1956 mpaka 1974.

Mchezaji aliyeitumikia Barcelona mechi nyingi: Xavi Hernandez ndio anashikilia rekodi hii akiwa amecheza mechi 767. Anayemfuatia ni Iniesta 642 halafu Messi, 600.

Mchezaji aliyeshinda mechi nyingi nchini Spain: Iker Casillas ana rekodi ya kushinda mechi 334 akiwa na Real Madrid kabla ya kwenda Porto. Andoni Zubizarreta (Athletic, Barcelona, Valencia) alimaliza kucheza soka na ushindi katika mechi 333. Raul Gonzalez 327, Xavi 322 na Manolo Sanchis 312 wa Madrid nae yupo mbele ya Messi, ambaye mpaka sasa ameshashinda mechi 298 za La Liga.

Mchezaji mwenye viatu vingi vya dhahabu: Leo Messi alishinda tuzo hii (2009/10, 2011/12, 2012/13 na 2016/17) na Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo hii (2007/08, 2010/11, 2013/14 and 2014/15)  – sasa wote wanaipigania rekodi hii. Msimu huu tayari Messi amefunga magoli 12 kwenye La Liga, CR7 amefunga moja tu.

Mchezaji mwenye Ballon D’or nyingi:  Hii ni vita nyingine ya Ronaldo vs Messi. La Purga alishinda tuzo hii mara 5 tayari 2009, 2010, 2011, 2012 na 2015, wakati Cristiano alishinda 2008, 2013, 2014 na 2016, na mwaka huu pia anapewa nafasi kubwa zaidi ya kushinda pamoja na kuanza msimu vibaya.

Hofu yatanda Manchester United kuhusu Jose Mourinho, yadaiwa anaogopa moto aliowasha Pep Gurdiola

$
0
0

Ripoti kutoka nchini Uingereza hii leo zinasema klabu ya Manchester United imenza kuwa na hofu juu ya kocha Jose Mourinho kwani anahisiwa kuikimbia ligi ya Epl kutokana na ushindani mkubwa.

Pep Gurdiola anatajwa kama sababu ya kumkimbiza Jose Mourinho kwani inaonekana Mourinho anaamini kwa sasa hawezi kushindana na Pep Gurdiola anayeonekana kuwa tishio kubwa hivi sasa.

Jose Mourinho anahusishwa na kutua katika klabu ya PSG tetesi ambazo zilishawahi kuibuka mara ya kwanza lakini baadae zikazima lakini hivi sasa inasemekana kuna ukweli kuhusina na jambo hilo.

Inadaiwa kwamba kutokana na umaarufu na upinzani wa muda mrefu kati ya Jose Mourinho na Pep Gurdiola inamfanya Mreno huyo kujisikia vibaya pale anapoona Pep ana kikosi kinachoonekana kutozuilika.

Pamoja na kiasi cha £300m ambacho United walitumia katika usajili uliopita lakini Mourinho anadaiwa kuhitaji tena kufanya usajili mwingine suala ambalo mabosi wa United ni ngumu kulitekeleza.

Mourinho ndio kwanza yuko nusu ya mkataba wake ambapo aliahidi msimu huu anaweza kufanya makubwa, japo hadi sasa hawako katika nafasi mbaya lakini tayari ameshawahi kuongelea kutamani kwenda Ufaransa.

Katika moja ya mahojiano yake Mourinho alisema hatamaliza kazi yake ya ukocha katika United na akisema Paris kuna jambo maalum huku akikiri hata mwanae alifurahi alipoekwenda Paris akaona mechi ya PSG.

Hadi sasa Manchester United wako nafasi ya pili Epl wakiwa na alama 23 ikiwa ni nane nyuma ya City walioko kileleni na alama 31 huku timu yao ikiwa imefunga mabao 50 katika mashindano yote tangu kuanza kwa msimu.

Doctor amethibitisha matibabu ya Farid Mussa hayahitaji upasuaji

$
0
0

Baad ya kufanyiwa vipimo na uchunguzi kwakina, imegundulika  Farid Mussa hakupata maumivu makubwa ya goti kama ilivyokuwa ikidhaniwa awali.

Farid Mussa amesema, daktari bingwa amemweleza kuwa, kuna baadhi ya mishipa inayounganisha tishu za kwenye goti ilipishana ndio maana alipata maumivu.

Daktari amethibitisha kwamba, matibabu yake hayahitaji upasuaji, amepewa wiki tatu za kufanya mazoezi chini ya physiotherapist halafu baada ya hapo anaweza kuanza mazoezi ya kawaida.

“Daktari amesema sijaumia sana kiasi cha kufanyiwa upasuaji, ni mishipa tu ilipishana, kwa hiyo amenipa wiki tatu za kufanya mazoezi chini ya uangalizi wa physiotherapist wa klabu, baada ya hapo naweza kuanza mazoezi ya kawaida”-Farid Musa.

Ukweli kuhusu tetesi za Lwandamina kurejea Zesco United

$
0
0

Baada ya taarifa kuenea kwenye mitandao ya kijaamii kwambakocha wa Yanga George Lwandamina anakaribia kujiunga na kabu yake ya zamani Zesco United ya Zambia, afisa habari wa Yanga Dismas Ten amesema kocha huyo amekwenda Zambia kwa ajili ya matatizo ya msiba.

Dismas amesema Lwandamina anatarajia kurejea nchini siku ya Jumatatu kwa ajili ya kuendelea na maandalizi kwa mechi za ligi zinazofuata.

“Taarifa pekee kutoka Yanga ni kwamba mwalimu amekwenda Zambia kwenye msiba na anarejea jumatatu, msiba ni jambo ambalo linamkuta kila mtu na huwezi kuliepuka na linapokufika huna budi kushiriki kwa yoyote ile. Hilo la Zesco siwezi kuzungumza kwa sababu mimi sipo Zesco na kama inazungumzwa kwenye mitandao huwezi kuzuia watu kwenye mitandao ndio sehemu yao kuzungumza.”

“Lwandamina bado ni mwajiriwa wa Yanga ndio maana nimesema kwamba amekwenda Zambia kwenye msiba na atarejea Jumatatu kwa ajaili ya matayarisho ya michezo ya ligi inayofuata.”

Carzola anaamini sukari ni tamu kuliko pilipili

$
0
0

Na Privaldinho ABIUD

Hivi unadhani Carzola anajisikiaje pale India Ursula akimuuliza baba mbona huendi kazini? Katikati mwa msimu jibu rahisi la Carzola Kwa Mwanae lilikuwa “mwanangi nitarudi kazini mwezi wa kumi” 

Mwezi wa kumi umefika na Carzola bado hajarudi kazini. Swali gumu zaidi kwa mwanae ni “baba mbona kwenye picha ya pamoja ya Arsenal ya Msimu hu haupo? Carzola itabidi amwambie nitarudi kazin mwakani. 

Michael Owen aliteseka na Majeruhi maisha yake yote ya soka. Alipofika mwaka 2013 aliona bora awe Dr Leakey wa England ili acheze mpira wa mdomoni kwenye vituo vya Tv baada ya Mateso ya misuli kwa kipindi kirefu. Mwaka 2007 Dr Richard Steadman alimweleza Ji sung Park kuwa opereshen yake ya goti itamweka benchi mwaka mmoja, haikuwa taarifa nzuri. 

Huyu Dr maarufu aliwahi kuwatibu akina Ronaldo, Ruud van Nistelrooy, Michael Owen na Alan Sheare na kuwaeleza wazi kuwa matatizo yao ya misuli yatahitimisha soka lao.Carzola nae tokea mwezi wa 10 mwaka jana hayupo uwanjani. Dr wake ndugu Roman Cugat huenda ndiye mwenye majibu sahihi kwa mtoto wa Carzola ambaye anamuuliza baba kwanini huendi kazini. Jibu la Cugat kwa mtoto wa Carzola ni moja tu. Amweke wazi kama Steadman alivyofanya kwa akina Delima. Amweleze ukweli kuwa baba hawezi kurudi uwanjani mapema hivyo atarudi Lugo de Llanera in Oviedo (nyumbani kwao).

Michael Owen aliumia mnamo tar 12 mwezi wa 4 mwaka 1992 akiwa na Liverpool kule Leeds. Mwaka 2007 alikaa nje ya uwanja takriban siku 315. Achana na 2012 ambapo alikaa nje kwa siki 129. Maisha haya ya Owen kushindwa kuishi kwa amani ndiyo yanamrudisha Carzola Llanera. Wakazi wa Asturias walizoea kumuona Carzola akikatiza misitu ya akina Vidic, Terry na Cahil. Wamemisi kumuona Carzola akimpa Furaha Wenger. 

Dr wake Roman Cugat ameshauri Carzola aachane na soka. Huu ni uamuzi mgumu sana kwake. Tokea mwezi wa 10 mwaka jana ilisemekana Carzola atatumia siku 346 akiwa benchi. Lakini kutokuwepo kwa Carzola kwenge picha ya pamoja ya Arsenal msimu huu basi huenda asiwepo mpaka mwakani. 

Ana umri wa miaka 32 kwa sasa, unategemea nini?

Ingawa Carzola Bado anaamini kuwa pilipili ni tamu kuliko sukari, ana Imani na misuli yake kuwa ina uwezo wakupambana majira yote.

Ndani ya miaka 8, Carzola amelitumikia benchi siku 608. Takribani miaka miwili amekuwa akitembea na magongo. Bila shaka  uhakika wa namba nane kwa Carzola itakuwa uwongo, misuli ya Carzola itaanza ushindani na Granit Xhaka. Nje yupo Ramsey, pia yupo Elneny. Usisahau kuwa Ozil atasimama kama namba 10.

Chumba cha Carzola ni kama kimeshanunuliwa. 

Mashabiki wa Arsenal watatamani kunirushia mawe, lakini niwaambieni tu ukweli, tafuteni video za Falcao aliyetokea benchi baada ya kukaa miezi 8 alikuwa na hali gani.

Labda tu tujiulize unafikiri swali la Enzo (mtoto wa Carzola) linampa hisia gani?

Kwa upande wangu huu ni wakati wa yeye kupunguza ruti za hospitali kila siku. Kiasi cha pesa alichokitumia kwenye upasuaji nadhani ni vyema arudi Cimavilla na fukwe za Abba Kaya kule Gijon akapunge upepo na mke wake Ursula. Aliyoyafanya ni makubwa. Asijikute Fransesco Totti. Misuli yake na akili vinaandamwa kama ishu ya makinikia.

Carzola amewekeza sehemu nyingi mno. Mwaka 2014 aliwekeza kwenye kampuni ya ardhi na makazi yenye ofisi zake Liverpool na Man United ijulikanayo kama Capital Centric Investments LLP. Ambapo yeye na Luis Suarez, Mikel Arteta na Jose Henrique waliwekeza zaidi ya Euro milioni 50 na wanategemea kupata faida ya sio chini ya Euro 250 milioni kwa mwaka. Wote walikuwa wakurugenzi kwenye kampuni moja licha ya uhasama wao wa kitimu wakiwa pamoja na akina Higgins. 

Nadhani huu ni wakati wa yeye kusimamia mambo yake Mengine ya kibiashara pamoja na wa ubavu wake. Amebarikiwa kuwa na mwanamke msomi waliyetokea nae kijiji kimoja. Mke wake huyu ni msomi mkubwa tu. Ana Degree ya   sayansi ya elimu ya viungo. Ni muda muafaka wa yeye kuwekeza zaidi na kufanya mambo mengine.. ni ngumu kukubali lakini sijui kama kuna namna ya Carzola ambaye muda sio mrefu atafikisha miaka 34 kurudi katika ubora wake. Kila la kheri kwake na nampa pole pia…

Viewing all 9000 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>