Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all 9000 articles
Browse latest View live

Hiki ndicho unapaswa kufahamu baada ya timu 32 kuelekea kombe la dunia kukamilika

$
0
0

Peru limekuwa taifa la mwisho kukata tiketi kwenda kushiriki michuano ya kombe la dunia itakayopigwa mwakani nchini Urusi baada ya kuibuka kidedea kwa mabao 2 kwa 0 zidi ya New Zealand.

Nini kinafuata? Baada ya mataifa 32 kufudhu sasa kinachofuatia ni droo ya kupanga timu hizo 32 katika makundi kwa ajili ya fainali hizo, mchezo ambao utafanyika siku ya kesho Ijumaa mjini Moscow.

Wababe, Timu za Ubelgiji, Hispania na Uingereza ndio timu ambazo zimefudhu katika michuano hiyo bila kupoteza mchezo hata mmoja na ndio timu pekee ambazo zimeingia katika michuano hiyo kwa kishindo.

Timu ya taifa ya Brazil haikuanza vizuri kampeni za kufuzu kwani walishinda mchezo mmoja kati ya sita ya mwanzo lakini baada ya kuja kocha mpya Tite ndipo wakaanza kupata matokeo mazuri wakishinda mechi 10 na kusuluhu 2 kati ya 12.

Timu zitapangwa kutokana na viwango vya shirikisho la soka vilivyotangazwa mwezi uliopita, makundi hayo yanatangwazwa kutoka kwenye magroup 4 ambayo tayari yamepatikana baada ya michezo ya kufudhu.

Suprise, Wakati hao wakiwa na rekodi ya kufuzu kwa kishindo kuna mataifa ambayo hii itakuwa mara yao ya kwanza kushiriki michuano ya kombe la dunia, Iceland hii ni michuano yao ya yakwanza huku pia Panama wakienda kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

Mshtuko, kuna mshtuko pia kuelekea michuano hii haswa taifa la Italia kukosa michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu 1958, ukiacha Italia kuna Mexico, Ivory Coast, Ghana na Cameroon pia ni mataifa makubwa yaliyokosa michuano hii.

TIKETI, hadi sasa FIFA wanasema kuna maombi milioni 3.5 ya tiketi za kombe la dunia huku kati ya hizo kuna 300,000 tayari zimeshafanyiwa application kwa ajili ya mechi ya fainali . 57% ya walioomba tiketi hizo wanatokeoa Urusi huku tiketi ya bei rahisi ni £345.


Je hii itakuwa Madrid Derby ya mwisho wa Torres?

$
0
0

Endapo Fernando Torres atafanikiwa kucheza katika mchezo wa November 18 katika dimba la Metropolitano – itakuwa Derby yake ya 21 ya Madrid kwa mshambuliaji huyo, swali, Je itakuwa ya mwisho?

El Nino hivi sasa ana miaka 33 na ingawa amepewa mkataba wa nyongeza wa mwaka 1 katika kipindi cha usajili kilichopita, amekuwa akipata nafasi finyu sana ya kucheza chini ya Diego Simeone.

Huku December ikikaribia, Torres amecheza dakika 332 katika mechi 10 zilizopita za mashindano yote na ameanza mchezo mmoja wa ligi, dhidi ya Girona katika mchezo wa ufunguzi wa msimu wa 2017/18.

Katika mechi 3 zilizopita za Atletico katika La Liga, Torres hajacheza hata sekunde na hajafunga goli katika msimu huu. Baada ya kuanza kama mshambuliaji pacha na Griezmann katika mchezo wa Girona, Torres akashuka kwenye listi ya washambuliaji nyuma ya Ángel Correa, Luciano Vietto na Kevin Gameiro.

Torres amekuwa akicheza mchezo wa kusubiri tangu aliporudi Calderon mnamo January 2015. Mara chache amekuwa akipata nafasi ya moja kwa moja akisubiri wengine kuumia ili kupata nafasi.

Mpaka sasa Torres ana historia ya kufunga mara 3 katika Madrid Derby akiwa na uzi wa Atletico. Goli lake la kwanza alifunga msimu wa 2006-07, msimu wake wa mwisho kabla ya kwenda Liverpool. Mengine mawili aliyafunga katika mchezo wake wa kwanza baada ya kurudi akitokea Milan.

Mshambuliaji huyu aliupiga chini mkataba mnono wa kwenda kucheza soka China katika kipindi kilichopita cha usajili na kuamua kubaki Atletico wakati wakihama kutoka Calderon kwenda Metropolitano.

TFF yapangua tuhuma za kujiongezea posho

$
0
0

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao ametolea ufafanuzi ujumbe uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii ukiituhumu taasisi hiyo inayoongoza soka la Tanzania kuongeza posho kwa wajumbe wa kamati ya utendaji pamoja na kuanzisha malipo ya mishahara kwa Rais na makamu wake.

1. Viwango vya posho za vikao vya Kamati ya Utendaji havijawahi kujadiliwa wala kubadilishwa (kuongezwa). Bado vipo vilevile.

2. Wajumbe wa kamati ya utendaji wanawezeshwa kutekeleza majukumu yao kwenye kanda zao. Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni kazi ya kujitolea watakuwa wakipewa Tsh. 1.5 milioni kwa miezi mitatu kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao kwenye Kanda zao (Tsh. 1.5 milioni ni sawa na Tsh. 500,000 kwa mwezi).

3. Kuhusu mshahara wa Rais wa TFF na makamu wake jambo hilo halikufikiwa mwafaka na Kamati ya utendaji. Wajumbe wa kamati ya Utendaji walishauri ofisi ya Rais ihudumiwe na TFF kama ilivyo kwa ofisi za marais wa FIFA na CAF.

Rais wa TFF Wallace Karia alikataa kwa kusema, anaamini sio wakati mwafaka wa yeye kuchukua posho hadi taasisi itakapokaa vizuri na taratibu zote kufuatwa.

Hatua zilizochukuliwa

Kidao amwagiza mwanasheria wa TFF kufungua mashtaka (leo) kwa wale waliosambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii wenye lengo la kuichafua taasisi hiyo.

Griezman anaipenda Atletico lakini Simeone anajaribu kumsukuma kwa Manchester United na Barcelona

$
0
0

Katikati ya msimu uliopita jina la mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezman lilitawala sana vyombo vya habari, Griezman alitawala vichwa vingi vya habari akihusishwa na kutimkia Manchester United.

Baadae tetesi zilizimwa huku Antoine Griezman akibaki Atletico Madrid. Lakini miezi michache baada ya dirisha la usajili Griezman anaanza tena kutengeneza habari akitajwa kushindwa kuibeba timu kipindi inachomhitaji.

Atletico Madrid wamekuwa na msimu mbovu sana safari hii huku wakikabiliwa na michezo migumu ndani ya siku saba zijazo ikiwemo mchezo dhidi ya majirani zao Real Madrid na mchezo wa Champions League vs As Roma.

Hadi sasa Atletico Madrid wako nafasi ya katika ligi kuu nchini Hispania La Liga ikiwa ni alama 8 nyuma ya Barcelona na pia kipigo toka kwa As Roma katika mechi ya Champions League kitashuhudia wakiaga michuano hiyo.

Kati ya sababu zilizotajwa kumfanya Antoine Griezman asiondoke Atletico ni kutokana na mapenzi yake juu ya klabu hiyo kiasi cha kuona itakuwa usaliti kuondoka Atletico wakati wanamhitaji sana.

Katika mkataba wa Antoine Griezman na Atletico Madrid kipo kipengele ambacho kimeweka wazi bei ya mchezaji huyo ambapo ilitoka £100m hadi kufikia £200m na sasa itarudi tena £100m mwakani bei ambayo miamba mingi ya Ulaya itatamani kutoa.

Inatajwa kwamba kwa sasa Antoine hana furaha ndani ya Atletico na anatamani kucheza na mwanasoka nguli Lioneil Messi huku pia inatajwa kwamba amekuwa akitamani kujiunga na rafiki yake Paul Pogba katika klabu ya Manchester United.

Griezman amecheza dakika 596 bila goli lakini mashabiki wa klabu ya Atletico wamwkuwa na hamu kubwa kumuona Antoine akibaki tena ili mwakani aanze kucheza na Diego Costa aliyejiunga na Athletico msimu huu akitokea Chelsea.

Diego Simeone amekosa namna ya kumfanya Griezman atakate kwa kukosa kumtaftia pacha sahihi wa kucheza naye kama mshambuliaji hadi sasa huku mechi nyingi ikiwemo ijayo zidi ya Real Madrid akimuacha peke yake kama mshambuliaji wa mwisho mbele.

Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps anaona kinachomtokea Griezman kwa sasa (kiwango duni) kinatokana na namna ambavyo timu yake inacheza msimu huu ikiwemo mfumo wa timu na ili kumuokoa ni lazima icheze vyema katika mfumo sahihi.

Kama Atletico watashindwa kucheza vyema kama Dechamps anavyoona baasi hii itamaanisha moja kwa moja itambidi Griezman akatafute mahali ambapo timu itakuwa inacheza vizuri.

Kipigo toka kwa Real Madrid mwishoni mwa wiki kitawafanya kuwa na pengo la alama 11 na vinara wa ligi na kuanza kufuta ndoto zao za ubingwa na kipigo toka kwa As Roma pia kitawafanya kuaga katika makundi ya CL msimu huu.

Wapi atakwenda?Hakuna striker asiyetamani kucheza na Romelu Lukaku kwa sasa na aina ya mshambuliaji kama Griezman aliyejawa na skills ila hayuko vizuri Physically ni lazima atamani kucheza na mshambuliaji mwenye nguvu kama Lukaku na uwepo wa Pogba unawapa nafasi United.

Wakati huo huo kila mchezaji duniani anatamani siku moja acheze pembeni ya kati ya wachezaji hatari kwahi kutokea dunian Ii Lioneil Messi na Griezman naye anatamani hili litokee siku moja.

Real Madrid je? Hapana na siamini kama Griezman atakwenda Madrid kwa kuwa kama ameshaogopa kuwasaliti Atletico kwa timu ya mbali na Hispania ni ngumu akasaini kwa majirani wa Atletico na pia PSG nako tayari kuna utawala mpya itakuwa ngumu kwake kuwa na uhakika wa nafasi.

Manchester United hawakuwa wakimhitaji Di Maria bali waliitaka jezi yake tu

$
0
0

Kati ya usajili ambao Luis Van Gaal aliufanya na ukawa gumzo dunia nzima ilikuwa ni usajili wa Angel Di Maria kutoka Real Madrid ambaye baada ya msimu mmoja tu waliamua kuachana naye akaenda PSG.

Wakati Di Maria akiondoka kwenda PSG hakuna bosi wa United alihangaika kumbembeleza abaki katika timu yao na walionekana walikuwa tayari kumuacha mchezaji huyo aondoke ndani ya muda mfupi.

Imebainikwa kwamba Manchester United walikuwa wakihitaji zaidi mauzo ya jezi ya Di Maria kuliko walivyokuwa wakihitaji uwepo wake katika timu hiyo na hilo lilimkera Muargentina huyo.

Msemaji wa mchezaji huyo amethibitisha kwamba United hawakumhitaji Di Maria ili kushinda makombe na walikuwa wakiambiana kwamba wakimnunua atawasaidia sana katika mauzo ya jezi.

Debora Gomes amesema Di Maria hakuwa na furaha ndani ya United na mabosi hawakuwa na habari naye huku akisema baada ya Fergie kuondoka sasa United imekuwa klabu ambayo haiwazi kuhusu soka tena bali jinsi ya kuingiza pesa tu.

Mwaka 2014 ndio mwaka ambao United walitoa kiasi cha £59m kwa Real Madrid ili kumnunua na inasemekana hadi anaondoka United walishauza jezi za Di Maria ambazo ziliwaingizia zaidi ya £75m.

Utovu wa nidhamu wamgharimu Pierre Aubameyang ndani ya BvB

$
0
0

Klabu ya Borussia Dortmund imeamua kumuweka nje kwa muda usiojulikana mshambuliaji wao tegemezi kutoka Gabon Pierre Aubameyang kwa kile kilichotajwa kama utovu wa nidhamu.

Taarifa rasmi kutoka ndani ya klabu hiyo imethibitisha kwamba Aubameyang hatakuwepo katika mchezo wa kesho ambao Borussia Dortmund wataikabili Stuttgart kutokana na matatizo hayo.

Hii sio mara ya kwanza kwa Mgabon huyu kupewa adhabu kutokana na masuala ya utovu wa nidhamu ambapo mwaka jana mwezi wa 11 aliachwa katika kikosi cha Dortmund kilichocheza zidi ya Sporting katika Champions League.

Matatizo kati ya Dortmund na Aubameyang yanaweza kuwa ishara kwamba mwanasoka huyo yuko mbioni kuachana na klabu hiyo kwani kila dirisha la usajili amekuwa akihusishwa na kuikimbia Dortmund.

Tayari katika msimu huu Aubameyang amefunga jumla ya mabao 10 lakini hajawahi kufunga tangu alipofunga katika mchezo zidi ya RB Leizpg  mwezi October ambapo Borussia Dortmund walifungwa bao 3 kwa 2.

World Cup 2018: Anguko la Italia, walikosea wapi, hasara za kiuchumi kwa kuikosa safari ya Russia na Nini kifanyike.

$
0
0

Wakati Carlo Tavecchio, Rais wa shirikisho la soka la Italia, alipotangaza kupewa kazi kwa Giampiero Ventura kuwa mbadala wa Antonio Conte, alitoa ahadi ya kutengeneza historia ya pamoja.

Mwaka mmoja baadae, kweli wametengeneza historia lakini historia mbaya. Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958, mabingwa wa mara 4 wa dunia hawatocheza kombe la dunia.

Tavecchio mwenyewe amesema kushindwa kufuzu ingekuwa ni janga. Sasa, janga limetokea.

Siku 4 zilizopita zimekuwa siku ngumu kwa Azzurri. Kama kipindi kile Giorgio Chinaglia alipotukana kwenye camera wakati Italia walipotolewa kwenye kombe la dunia 1974, au walipoondoleaa kwenye hatua ya makundi mbele ya New Zealand mwaka 2010 na Costa Rica miaka 4 iliyopita katika michuano ya dunia.

Wapi walipokosea

Kuna taswira mbili ambazo hazitosahaulika haraka machoni mwa wapenzi wa Azzurri. Picha ya Gianluigi Buffon akilia machozi na picha za video zinazomuonesha mmoja wa wasaidizi wa kocha Ventura akibishana Daniele de Rossi – akimuamuru De Rossi kupasha.

“Kwanini niende kupasha?” Alionekana akiuliza De Rossi. “Hatuhitaji sare hapa. Tunahitaji kushinda.” De Rossi akaonekana akimuelekeza kocha wake kwa Lorenzo Insigne – akitoa ishara kwamba ndio anayepaswa kuingia.

Insigne ndio mchezaji fundi aliye kwenye kiwango cha juu kwa sasa katika safu ya ushambuliaji ya Italia. Amekuwa akiiongoza Napoli kuanza msimu wakiwa on fire msimu huu. Lakini Ventura alimuacha nje mshambuliaji wakati timu yake ikimhitaji kuliko wakati mwingine wowote.

Wachezaji wakubwa wa kikosi walikuwa na mkutano wa dharula baada ya sare dhidi ya Macedonia jijini Turin mwezi uliopita. Ripoti zilijitokeza tena wakati timu ilipokuwa ikirejea kutoka kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Sweden ambapo wachezaji wakubwa walimuomba kocha abadili mfumo na uchaguzi wa wachezaji. Inasemekana Ventura alitishia kujiuzulu kabla ya kuombwa kutofanya hivyo.

Mbinu zake zilishindwa kuzaa matunda Jumatatu iliyopita. Wakicheza mfumo wa 3-5-2 ilionekana wazi kwamba hakukuwa na nafasi ya Insigne katika kikosi na ilikuwa wazi baada ya filimbi ya kuanzisha mpira ilipopulizwa kwamba kuwaanzisha mabeki watatu wa kati halikuwa jambo la busara hasa kwa sababu timu pinzani ilikuwa imeweka kambi kwenye eneo lao la penati. Mabadiliko yalihitajika. Italy walikuwa wakipiga krosi kila mara, jambo ambalo halikuwasumbua Wasweden. Mabeki wao warefu walizuia kila krosi iliyopigwa.

Wachezaji ambao wamekuwa na viwango vizuri kwenye timu zao za vilabu, wamekuwa vivuli vyao wakiwa na timu ya taifa, Ventura amekuwa hana mipango na ilianza kujionesha vizuri tangu walipofungwa 3-0 dhidi ya Spain jijini Madrid.

Inatosha kuamini kwamba Italy wametumia mifumo mitatu tofauti katika mechi zao 4 zilizopita. Wachezaji ambao huko nyuma wakipewa nafasi kama Simone Verdi, Jorginho, na Manolo Gabbiadini walipewa nafasi kubwa. Ni Jorginho tu ambaye amekuwa akicheza vyema.

Hasara za kukosa kombe la dunia

Inakadiriwa timu ya taifa ya Azzurri itakosa kiasi cha 100m Euros ambazo zingetokana na mapato ya kufuzu kucheza kombe la dunia. Bonasi kutoka kwa wadhamini, Fedha za mauzo ya haki za matangazo ya Tv na fedha za zawadi. Shirikisho la soka la Italia watapata wakati mgumu wa kujadili mikataba mipya na Luma na wadhamini wao wengine pindi watakapoanza kujadiliana upya.

Haki za matangazo ya TV kwa World Cup zimeshuka thamani kwa zaidi ya nusu ya thamani nchini Italia. Namba ya wateja ya kununua TV – ilipanda kwa 4% wakati wa Euro 2016 – hivi sasa huenda ikashuka.

Mkataba aliovunjiwa Ventura na FIGC unatakiwa pia kulipiwa fidia japokuwa kulikuwa na vipengele vya kuonyesha endapo timu itashindwa kufuzu malipo hayo yatapungua. Ventura aligoma kujiuzulu pamoja na shinikizo kubwa kutoka kwa waitaliano na inaelezwa aligoma kujiuzulu ili asipoteze haki zake za malipo.

Nini kinafuatia

Mara baada ya Ventura kuondolewa, kifuatacho sasa ni kumtafuta mrithi wake. Carlo Ancelotti yupo huru na inaonekana ni muda sahihi kwake kuchukua majukumu ya timu ya taifa.

Wachezaji watatu waliokuwepo wakati Italy iliposhinda taji la kombe la dunia mwaka 2006, Gianluigi Buffon, De Rossi na Andrea Barzagli, wote wameshatangaza kustaafu kuitumikia Azzurri.

Giorgio Chiellini amesema anahitaji muda ili aweze kuamua. Anaamini soka la Italia linahitaji kurudo nyuma kidogo ili liweze kusonga mbele – hapa anamaanisha ku-reset mfumo mzima na kuanza upya.

Haya pia yalisemwa wakati Italia walipotolewa kwenye hatua ya makundi kwenye kombe la dunia lilopita wakati Cesare Prandelli alipojiuzulu, akafuatia Giancarlo Abete. Hata hivyo bado hakukuwa na mabadiliko.

Tavecchio alitoa ahadi ya kufuata mfumo wa Wajerumani na kufungua vituo vya soka nchi nzima. Mpaka anaondoka madarakani vimefunguliwa vituo 30 tu, tofauti na vituo 200 vilivyopangwa mwanzoni.

Ahadi yake nyingine ilikuwa ni kuweka mpango wa kupunguza timu kwenye Serie A kutoka timu 20 mpaka kuwa 18, kuongeza ubora na kuondoa wingi, hili halijaweza kutokea.

Serie A imeanza kuonyesha mwanga wa maisha. Juventus wamefika hatua ya fainali za Champions League mara 2 katika misimu 3. Ukiangalia kwa mfano Premier League, hawajafanikiwa kupeleka timu fainali tangu 2012.

Serie A tayari imeshaipiku Bundesliga katika viwango vya UEFA. Roma waliinyanyasa Chelsea 3-0 katika Champions League, Atalanta waliinyodha Everton katika Europa League 3-0 na Pep Guardiola amesema Napoli ni Moja ya timu bora barani ulaya.

Kuna waitaliano wengi kama Waargentina na Wajerumani katika listi ya wachezaji wanaogombea Ballon d’Or na bado wana kizazi kipya kinachokuja vizuri japokuwa bado hawajafanikiwa kuwapata Totti, Del Piero au Maldini wapya.

Italy walifika nusu fainali ya Euro U21 na katika michuano ya kombe la dunia U20. Kuna mwanga mbele kwenye soka la Italia na kama ambavyo Massimo Gramellini alivyoandika katika Il Corriere della Sera: “Sio mwisho wa dunia, ni mwisho wa kombe la dunia moja”

Mwantika kucheza mechi ya kwanza VPL 2017/2018

$
0
0

Beki wa kati wa Azam David Mwantika hacheza mechi yoyote tangu kuanza kwa msimu huu (2017/2018) ikiwa tayari Aza imeshacheza mechi tisa (9) hadi sasa bila uwepo wake ndani ya uwanja.

Kukosekana kwa Mwantika kwenye kikosi cha kwanza cha Azam kunatokana na ushindani mkubwa wa nafasi katika eneo lake huku wapinzani wake wengi wakiwa ni raia wa kigeni. Kufanya vizuri kwa mabeki raia wa Ghana Yakubu Mohammed na Daniel Amoah ndani ya kikosi cha kocha Aristika Ciaobandiko kunamfanya Mwantika achezee benchi.

Kushindwa kufurukuta kwa Mwantika ndani ya klabu yake, beki huyo wa zamani wa Tanzania Prisons amepoteza nafasi katika timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ambapo mara ya mwisho alicheza wakati Stars ilipocheza ugenini dhidi ya Nigeria (September 2016) kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika (Africa Cup of Nations). Baada ya hapo Mwantika aliungana na kikosi cha Azam mkoani Mbeya kwa ajili yamechi za VPL dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City (mechi zote Azam ilishinda uwanja wa Sokoine).

Habari njema ni kwamba, Mwantika huenda akarejea kwenye kikosi cha kwanza kutokana na kukosekana kwa Yakubu. Meneja wa Azam FC Philip Alando amethibitisha Azam itawakosa wachezaji wake watatu wa kikosi cha kwanza (Himid Mao, Yakubu Mohammed na Daniel Amoah) kukosekana kwa Yakubu na Amoah kwa wakati mmoja kutatoa fursa kwa Mwantika kurejea kwenye kikosi cha Azam itakapokuwa ikicheza dhidi ya Njombe Mji siku ya Jumapili kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.

Mwantika anatarajiwa kuanza kwenye kikosi cha kwanza sambamba na  Aggrey  Morris Ambrosi katika beki ya kati, tangu kuanza kwa msimu huu Aggrey amekuwa akicheza na Yakubu, huku walinzi wa pembeni wakiwa ni Daniel Amoah (kulia) na Bruce Kangwa (kushoto).


Pius Buswita Jogoo la shamba linalowika mjini, Hoza, Haule, Mseja, Mwambeleko, chali  

$
0
0

Pius Buswita ameukataa  ule msemo wa ‘wahenga’ “Jogoo la shamba haliwiki mjini”, wakati wenzake wanne wamedhihirisha wahenga hawakukosea katika kauli hiyo.

Baada ya kumalizika ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2016/2017 huku kikosi cha Mbao kutoka mkoani Mwanza kikinusurika kushuka daraja siku ya mwisho (May 20, 2017) baada ya kuifunga Yanga 1-0 kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza wakati Mbao wakifanya sherehe za kunusurika kushuka daraja katika msimu wao wa kwanza VPL, Yanga walikuwa wanasherekea ubingwa wao wa tatu mfululizo katika msimu huo.

Wiki moja baadaye (May 27, 2017) Kikosi cha Mbao kilikuwa kinacheza fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Simba mchezo ambao walipoteza kwa kufunga 2-1 kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Timu zenye majina makubwa za jijini Dar es Salaam (Simba, Yanga na Azam) zikaanza kukimbizana kutafuta wachezaji kwenye chaka la Mbao. Kila timu ikafanikiwa kunyakuwa wachezaji kutoka katika timu hiyo iliyopanda kucheza VPL kwa staili ya aina yake msimu uliopita.

Simba wakawasajili mlinzi wa kushoto Jamal Mwambeleko na golikipa Emanuel Mseja, Yanga wakamchukua kiaina Pius Buswita, huku Azam wakifanikisha usajili wa Salmin Hoza na golikipa Benedict Haule.

Kati ya wachezaji hao watano waliosajiliwa na vilabu vyenye majina makubwa bongo kutokea Mbao, Pius Buswita ndiyo mchezaji pekee ambaye ameshacheza mechi za VPL msimu huu akiwa na klabu yake mpya (Yanga) huku wenzake wakiishia benchi na wakati mwingine hawakai kabisa hata benchi hivyo kutazama mechi wakiwa kwenye majukwaa.

Usajili wa Buswita

Inaelezwa Buswita alishakubaliana kila kitu na klabu ya Simba ambayo ilimtumia tiketi ya ndege atoke mwanza kwenda Dar kwa ajili ya kumalizana kuhusu usajili, alipokea pia kisasi cha pesa kwa ikiwa ni ada ya usajili lakini mwisho wa siku akaishia mikononi mwa Yanga ambao walimaliza bishara akatia dolegumba na kuzima ndoto za Simba.

Buswita alitoa msemo uliobamba kipindi hicho ‘shetani alinipiti’ hiyo ilikuja baada ya kuwa amesaini Yanga huku Simba akiwa ameshasaini makubaliano ya awali ya kujiunga na klabu hiyo ya Msimbazi.

Kosa alilofanya Buswita alistahili kufungiwa kucheza soka kwa mwaka mmoja lakini baadae mchezaji huyo alifunguliwa kifungo hicho kwa sharti la kulipa pesa alizochukua kutoka Simba (Tsh.10 milioni) pamoja na kuilipa Simba gharama za tiketi ya ndege waliyomtumia.

Buswita amecheza mechi tano (5) za VPL kati ya tisa ambazo Yanga imecheza hadi sasa, mechi yake ya kwanza akiwa Yanga ilikuwa dhidi ya Mtibwa Sugar na baada ya hapo akacheza mechi zote zilizofuata zilizoihusisha Yanga.

  • Yanga 0-0 Mtibwa Sugar
  • Kagera Sugar 1-2 Yanga
  • Stand United 0-4 Yanga
  • Yanga 1-1 Simba
  • Singida United 0-0 Yanga

Ameshafunga goli moja katika mechi tano ambazo amecheza. Goli lake la kwanza alifunga wakati Yanga ikicheza dhidi ya Stand United, katika ushindi wa mabao manne alifunga goli moja huku Ajibu akifunga mawili na Chirwa kufunga goli moja.

Wachezaji wengine wanne waliotoka Mbao

Jamal Mwambeleko

Amekuwa katika wakati mgumu kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Simba, licha ya Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ kuwa katika majeraha kwa kipindi kirefu lakini nafasi hiyo ikazibwa na Erasto Nyoni ambaye ni kiraka wa eneo lote la ulinzi hadi kiungo. ‘Zimbwe Jr’ taratibu amerejea kwenye timu hivyo kufanya nafasi ya Mwambeleko kuwa finyu zaidi kwenye kikosi cha Simba. Hajacheza mechi hata moja ya VPL msimu huu.

Emanuel Mseja

Golikipa aliyejiunga na Simba licha ya kwamba hakuwa akipata nafasi mara kwa mara kwenye kikosi cha Mbao, ana mlima mzito wa kumweka nje Aishi Manula golikipa namba moja wa Simba na timu ya taifa ‘Taifa Stars’, namna pekee ambayo Mseja anaweza kucheza kwenye kikosi cha Simba ni kutokuwepo kwa Manula kutokana na majeraha, adhabu ya kadi au vinginevyo, lakini nafasi yake ni ndogo kucheza kwenye timu ya kwanza huku Manula akiwa fit kwa 100%. Hajacheza mechi hata moja ya VPL msimu huu.

Benedict Haule

Golikipa mwingine aliyekula shavu Azam baada ya kufanya vyema kwenye kikosi cha Mbao, alichukua nafasi ya golikipa namba moja wakati huo Mussa Ngwengwe ambaye alifungiwa baada ya Simba kusawazisha magoli matatu ndani ya dakika za majeruhi.

Haule yupo kwenye mtihani mgumu kufaulu ili kucheza kikosi cha kwanza cha Azam, kumtoa kwenye goli Razak Abarola ambaye tayari amethibitisha ubora wake tangu kuanza kwa msimu akicheza mechi saba bila kuruhusu goli kati ya mechi tisa. Mechi zote tisa zilizochezwa, Haule hajakaa hata kwenye benchi badala yake golikipa mkongwe wa klabu hiyo Mwadini Ali ndio amekuwa golikipa namba mbili. Hajacheza mechi hata moja ya VPL msimu huu.

Salmin Hoza

Utitiri wa viungo ndani ya kikosi cha Azam (Himid, Sure Boy, Domayo, Stephan Kingue, Masoud Abdallahna wengine) bado wanafanya nafasi ya Hoza kuwa ngumu kwenye kikosi cha kwanza. Kiungo kama Mudathir Yahya kutolewa kwa mkopo kwenda Singida United inaashiria ni jinsi gani eneo la kiungo lilivyo na changamoto, kwa kiwango anachoonesha Mudathir siku za hivi karibuni ni ishara tosha ya kazi kubwa aliyonayo Hoza ili kuchomoza kwenye kikosi cha kwanza cha Azam. Hajacheza mechi hata moja ya VPL msimu huu.

David Luiz anakwenda Manchester United? Habari 5 kubwa za magazeti ya Uingereza hii leo

$
0
0

Daily Express. Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anatajwa kuwa mbionj kujaribu kumshawishi David Luiz ajiunge naye ifikapo mwezi wa kwanza baada ya beki huyo kutajwa kutokuwa na mahusiano mazuri na kocha wa Chelsea.

Daily Mirror. Klabu ya Liverpool sasa italazimika kutoa kiasi cha £70m kwa ajili ya kumnunua mliniz wa Southampton Virgil Van Djik ambaye wamekuwa wakimtaka kwa muda mrefu na sasa kocha wa Southampton amesema wako tayari kumuachia kama wakipata kiasi hicho.

Daily Star. Steve Kaplan ambaye ni moja kati ya wamiliki wa klabu ya Swansea amepiga kura ya kutokuwa na imani na kocha wa Swansea Paul Clement na sasa kocha huyo anakuwa amekalia kuti kavu ndani ya klabu hiyo.

The Sun. Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal na pia Manchester City Emmanuel Adebayor ameishutumu familia yake kwamba ilimfanya atamani kujiua zaidi ya mara tatu kutokana na matatizo yaliyosababishwa na familia hiyo.

Daily Mail. Klabu ya soka ya Manchester United imezipiga chini tetesi za Jose Mourinho kuhamia PSG na kusisitiza kwamba tetesi hizo sio za kweli kwani kocha huyo bado atakaa Old Traford kwa muda mrefu zaidi.

Miaka 4 imepita, Simba haijaifunga Prisons uwanja wa Sokoine

$
0
0

Imepita miaka minne tangu Simba ilipopata ushindi wake wa mwisho dhidi ya Tanzania Prisons kwenye uwanja wa nyumbani wa maafande wa jeshi la Magereza, matokeo mazuri kwa Simba katika kipindi hicho yamekuwa ni sare.

Katika mechi tano mfululizo ambazo Simba wamecheza ugenini dhidi ya Tanzania Prisons wameshinda mchezo mmoja pekee, hiyo ilikuwa  20/02/2013 Tanzania Prisons 0-1 Simba. Tangu hapo Simba imekuwa ikitoka kichwa chini kwenye uwanja wa Sokoine kwani tangu kuanza kwa mwaka 2014 hadi sasa bado wanapambana kuupata ushindi wa kwanza tangu waliposhinda kwa mara ya mwisho 2013.

Namba hazidanganyi

Matokeo ya mechi za Tanzania Prisons vs Simba kwenye uwanja wa Sokoine tangu mwaka 2014

  • 09/11/2016 Tanzania Prisons 2-1 Simba
  • 21/10/2015 Tanzania Prisons 1-0 Simba
  • 25/10/2014 Tanzania Prisons 1-1 Simba
  • 09/03/2014 Tanzania Prisons 0-0 Simba

Msimu uliopita Simba ikiwa katika kiwango bora huku ikiuwinda ubingwa, ilijikuta ikichezea kichapo cha 2-1 kama imesimama, licha ya Jamal Myante kutangulia kuifungia Simba bao la kuongoza dakika ya 44 kipindi cha kwanza, Prisons walitoka nyuma na kuzima ndoto za Simba kupata ushindi mbele yao kwenye uwanja wa Sokoine.

Victor Hangaya (kwa sasa yupo Mbeya City) ndio alikuwa mtu mmbaya kwa Simba katika siku hiyo, aliisawazishia timu yake dakika tatu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili. Wakati Simba wakipambana kuongeza bao la pili ili waondoke na pointi tatu, Hangaya akapachika bao la pili dakika ya lililoimaliza Simba.

Msimu huu Simba wanaingia kuikabili Prisons wakiwa hawajapoteza mechi hata moja tangu kuanza kwa ligi, wameshinda mechi tano na kutoka sare katika michezo minne kati ya tisa, Simba inaongoza ligikwa wastani mzuri wa magoli ikiwa imelingana pointi na Azam (zote zina pointi 19). Prisons yenyewe imeshinda mechi tatu, (imeshinda mchezo mmoja nyumbani katika ya mechi nne) imetoka sare mara tano na kupoteza mchezo mmoja kati ya tisa.

Matokeo ya Prisons kwenye uwanja wa Sokoine msimu huu

  • Tanzania Prisons 2-2 Majimaji
  • Tanzania Prisons 0-0 Ndanda
  • Tanzania Prisons 0-0 Stand United
  • Tanzania Prisons 1-0 Ruvu Shooting

Simba imeshacheza mechi nne nje ya uwanja wa Uhuru kati ya michezo tisa, katika mechi hizo imeshinda mara mbili huku ikitoka sare mbili katika mechi za nje ya uwanja wa Uhuru.

Msimu uliopita Tanzania Prisons ndio ilikuwa timu ya kwanza kuifunga Simba nje ya Dar, kabla ya mchezo huo Simba ilikuwa imepoteza mechi moja (ilipoteza dhidi ya African Lyon uwanja wa Uhuru Dar). Je Prisons itakuwa timu ya kwanza tena kuifunga Simba nje ya Dar?

Matokeo ya Simba nje ya uwanja wa Uhuru msimu huu 

  • Azam 0-0 Simba
  • Mbao 2-2 Simba
  • Stand United 1-2 Simba
  • Mbeya City 0-1 Simba

Utamu wa mechi ya kesho Jumamosi November 18, 2017

Simba watakuwa ugenini kupambana na Tanzania Prisons, mechi hii ina pande mbili, upande wa kwanza Prisons itakuwa ikipambana kuhakikisha inaendeleza rekodi ya kutopoteza dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Sokoine wakati upande wa pili Simba itakuwa ikifanya kila liwezekanalo kuivunja rekodi ya kushindwa kuondoka na pointi tatu mbele ya Prisons kwenye uwanja wa Sokoine.

Pierre Aubameyang na BvB hali yazidi kuwa mbaya

$
0
0

Klabu ya Borussia Dortmund imemuacha mchezaji wao tegemezi Pierre Aubameyang katika kikosi chao kitakachocheza zidi ya Stuttgart usiku wa leo huku chanzo cha tukio hilo ikitajwa ni utovu wa nidhamu.

Gazeti moja nchini Ujerumani limetoa taarifa kuhusu adhabu aliyopewa Aubameyang ambapo limedai kwamba nyota huyo alichelewa katika mazoezi ya mwisho ya klabu kujiandaa na mchezo wa leo ambapo alichelewa kwa dakika 20.

Matatizo kati ya Pierre Aubameyang na klabu yake ya Dortmund yalianza baada ya kwenda kumtembelea Ousmane Dembele aliyeko Barcelona ambapo inadaiwa alipewa ruhusa ya kwenda lakini akachelewa kurudi.

Aubameyang mwenyewe amesisitiza kwamba baada ya mchezo wao na Ac Milan msimu uliopita alielewa kwanini alialidhibiwa na hakuwa na tatizo, lakini anashangaa adhabu aliyopewa safari hii hajui ni kwanini amefanyiwa hivyo.

Tatizo lingine linalotajwa kumtia matatani Aubameyang ni kitendo cha kurekodi video na mchezaji wa nitindo huru ya mpira aitwaye Sean Garnier ambapo video hiyo ilirekodiwa katika uwanja wa Dortmund huku Garnier akiwa chini ya Red Bull.

Kampuni ya Red Bull ndio wadhamini wa klabu ya Rb Leizpg ambao ni wapinzani wa Borussia Dortmund na suala alilofanywa Aubameyang liliwaudhi wadhamini wa klabu hiyo kiasi cha kulazimisha aadhibiwe.

Vile vile baadhi ya wachezaji wa BvB wametajwa kumchongea Aubameyang kwa kocha mkuu wa klabu hiyo kwa kile kilichotajwa kwamba mshambuliaji huyo amekuwa mvivu ambapo ameanza kuwa mvivu hadi uwanjani.

Tukio hili linatajwa kuibua upya na kwa kasi kubwa tetesi za Pierre Aubameyang kuihama Dortmund, tayari vilabu vingi duniani ikiwemo Bayern Munich vimeanza kutupa macho kuhusu mwisho wa Aubameyang na Dortmund.

“Mara nyingi nilitamani kujiua” Emmanuel Adebayor

$
0
0

Emmanuel Adebayor amekuwa mwanasoka ambaye ametawaliwa na matukio mengi sana nje ya uwanja, Adebayor amekuwa na maisha magumu ndani ya uwanja na mara zote  amekuwa akiishutumu familia yake.

Mara kadhaa Adebayor amekuwa akidai kwamba chanzo cha yeye kuwa na kiwango kibovu uwanjani ilikuwa ni uchawi anaofanyiwa na ndugu zake. Adebayor alishawahi kwenda mbali kwa kudai kuwa mama yake alimchongea atimuliwe Madrid.

Sasa Emmanuel Adebayor ameibuka na jipya ambapo anasema familia yake ilimchanganya kiasi cha kumfanya kujaribu kujiua mara kadhaa, Adebayor anadai familia ilimpa msongo wa mawazo wakati wote.

Familia ya Adebayor ambayo inaishi nchini Togo ni maskini sana na wanatajwa kwamba walikuwa wakihitaji kiasi kikubwa cha pesa kutoka kwa mwanasoka huyo kiasi cha kutumia mbinj nyingi ili wazipate.

“Nilitamani kujiua mara nyingi tuu na hili nilikuwa silisemi kwa mtu na nimekaa nalo kwa muda mrefu, sikutaka kuliongea jambo hili lakini sasa naona kama kulisema hadharani itanisaidi kuwa huru” alisema Adebayor.

Adebayor anasema amekuwa akizungumza na mdogo wake mara nyingo kuhusu familia yake inavyomfanyia kiasi cha kufikia kuamua kubadili namba ya simu ili kuwafanya wasiwe wanamtafuta.

Adebayor anasema kati ya sababu kubwa iliyomfanya kubadili namba ya simu ni tukio la familia yake kumpigia simu wakati akiwa majeruhi na kumuomba pesa bila hata kumuuliza anaendeleaje.

Ukiachana na dada yake Adebayor amekuwa akiamini kikwazo kikubwa kwake ni mama yake mzazi ambapo wakati akiwa Tottenham alisema wazi kwamba kiwango kibovu kilitokana na ndumba za mama yake.

Baada ya kuachana na Crystal Palace, Adebayor alikaa nje kwa muda mrefu akiwa hana timu ya kuichezea lakini sasa yuko nchini Uturuki katika klabu ya Istanbul Basksehir.

Singida United yaikaba koo Yanga

$
0
0

Ushindi wa goli 1-0 ilioupata timu ya Singida United dhidi ya Lipuli unaifanya timu hiyo ya mkoani Singida kufikisha pointi 17 sawa na Yanga pamoja na Mtibwa Sugar.

Licha ya kufungana pointi na timu hilo (Yanga na Mtibwa) Singida United ipo nafasi ya tano kutokana na wastani wa magoli. Tayari timu hiyo imeshacheza mechi 10 za VPL sawa na Lipuli huku vilabu vingine vikiwa vinataraji kucheza michezo ya mzunguko wa 10 kesho Jumamosi na keshokutwa Jumapili.

Singida United imepata ushindi wake wa kwanza kwenye uwanj wa nyumbani (Namfua) tangu imepanda kucheza ligi kuu msimu huu, awali timu hiyo ilikuwa ikiutumia uwanja wa Jamhuri Dodoma wakiwa wamepisha ukarabati wa uwanja wa Namfua. Mechi yao ya kwanza kucheza uwanja huo msimu huu ilikuwa dhidi ya Yanga ambapo ilimalizika bila timu hizo kufungana.

Kikosi cha Hans van Pluijm kimepata ushindi wa kwanza baada ya kutoka sare katika mechi tano mfulizo zilizopita. Ushindi huo ni wa nne katika mechi 10 ambazo tayari wamecheza. Singida imepoteza mechi moja tu msimu huu ambapo ilifungwa 2-1 na Mwadui kwenye mechi yao ya kwanza.

Simba hawajui wako wapi, walipotoka na wanapokwenda, kamati ya usajili itaendelea kuwaangusha

$
0
0

Na Baraka Mbolembole

WAKATI wa usajili wa dirisha kubwa katikati ya mwaka huu nilikosoa waziwazi usajili wa klabu ya Simba SC na kusema, saini za Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Mghana, Nicolas Gyan, Mganda, Emmanuel Okwi. Magolikipa Said Mohamed, Emmanuel Mseja, Yusuph Mlipili hazikuwa sajili zilizotokaoa na mapendekezo ya benchi la ufundi au mapungufu yaliyoonekana katika kikosi ambacho kilimaliza nafasi ya pili kwa mara ya kwanza katika ligi kuu Tanzania baada ya kusubiri kwa misimu minne.

Usajili wa kitaalam ulikuwa

Jamal Mwambeleko, Ally Shomari upande wangu ndiyo usajili ambao ulizingatia mapungufu ambayo kikosi cha Mcameroon, Joseph Omog iliyaonyesha msimu uliopita. Katika beki ya kulia ambako, Mcongoman, Javier Bukungu alikuwa akicheza palionyesha mapungufu hasa pale mchezaji huyo alipokosena kwa sababu za majeraha ama adhabu na aliyekuwa mbabadala wake,Hamad Juma alishindwa kufanya vizuri hivyo ilikuwa ni lazima Simba ifanye usajili wa nyongeza katika nafasi hiyo. Usajili huo haukupaswa kuwa wa Shomari Kapombe ambaye alisajiliwa kwa dau lisilopungua milioni 60 wakati mchezaji huyo hakuwa amecheza michezo walau 20 kwa kipindi cha mwaka mmoja akiwa Azam FC kutokana na matatizo ya majeraha.

Tatizo ni Poppe na kamati yake

Nimekuwa nikimkosoa wazi Zacharia Hans Poppe ambaye kutokana na nafasi yake ya uenyekiti wa kamati ya usajili amekuwa akiitia hasara kubwa klabu hiyo kwa kushinikiza kuachwa na kusajiliwa kwa wachezaji kila wakati wa usajili unapofika.

Poppe hana ufahamu mkubwa kuhusu soka, ndiyo maana katika kipindi cha miaka zaidi ya mitano akiwa katika nafasi hiyo Simba imesajili wachezaji wengi na wagharama kubwa kutoka ndani na nje ya Tanzania lakini wameambulia ‘patupu.’

Mwambeleko alikuwa ingizo bora na zuri katika beki ya kushoto. Huyu alisajiliwa ili kuwa msaidizi wa mchezaji bora wa klabu na ligi kuu msimu uliopita, Mohamed Hussein.

Kwa kuwa walisajili kwa ‘matakwa yao’ Ally, Kapombe, Nyoni na Mwambeleko wote walisajiliwa katika usajili uliopita na wote wanatakiwa kugombea nafasi mbili katika beki za pembeni. Huu ulikuwa ni usajili wa kocha Omog? Kama ni wake anapaswa kufukuzwa lakini kama ulikuwa usajili wa viongozi wanapaswa pia kuwajibika kwa maana tayari katika kundi hili Kapombe hatakiwi na Poppe kwa sababu tangu asajiliwe amekuwa na majeraha yaliyosababisha asicheze mchezo wowote hadi sasa.

Najiuliza, Poppe na kamati yake ya usajili hawakuwa wakifahamu lolote kuhusu majeraha ya Kapombe akiwa Azam FC? Kama walikuwa wakifahamu kwa nini sasa walimsaini kwa dau kubwa na sasa wanataka kuvunja mkataba wake hata miezi 6 haijatimia?

Kwa hakika bora kuwa nafasi ya mwisho kwa sababu unaweza kufanya juhudi na kusogea, lakini kuwa katika mwelekeo usiofahamu unapotoka, ulipo na unapokwenda ni hatari sana kwa maendeleo na hiki ndicho wanakifanya Simba hivi sasa.

Klabu hii licha ya kila mwanzo wa msimu kujinasibu watashinda ubingwa, lakini wamekuwa wakishindwa kutimiza hilo kwa sababu ya uwepo wa watu wenye madaraka mengi na wanaopenda ‘ukubwa wa kimaamuzi.’

Tazama sajili hizi za kulipwa

Sawa, tangu kina Lino Musombo, Kanu, Donald Msoti, Danny Sserunkuma,  Musa Mude, Pierre Kwizera, Simon Sserunkuma, Hamis Kiiza, Brian Majwega, Blagnon, Vicent Angban, Daniel Agyei, Bokungu, Musa Ndusha hadi sasa kina Laudit Mavugo, James Kotei, Method Mwanjale, Juuko Murshid, Niyonzima na wengineo ni dhahiri Simba imefanya usajili usio na faida chini ya kamati ya Poppe.

Hao niliowataja ni baadhi tu ya wachezaji wa kigeni ambao mwenyekiti huyo wa kamati ya ujenzi wa uwanja wa klabu (Bunju Complex) aliufanya kati ya mwaka 2013 hadi sasa. Vipi kuhusu sajili ghali alizowahi kuzifanya kwa wachezaji wa kitanzania?

Anguko zaidi

Wakati ule niliposema Kagera Sugar inapaswa kubaki na ushindi wao vs Simba, watu walipinga sana, lakini ndani ya uwanja kila mmoja aliona Simba ilivyochapwa 2-1. Niliposikia Simba wamekimbilia FIFA kwa madai ya kutotendewa haki kuhusu rufaa yao ya kadi 3 za njano za mlinzi wa Kagera Sugar, Mohamed Fakhi niliwaambia wazi kuwa uongozi wa klabu hiyo unatengeneza imani ya kuwaaminisha wanachama wao kuwa walishindwa kutwaa ubingwa kwa sababu walinyimwa ushindi na TFF, nikawaambia, ‘Barua ile haikuwa na mashiko’ wapo waliopinga, lakini miezi zaidi ya 7 sasa hakuna kitu.

Pia nilisema watafunika ‘kombe mwanaharamu apite’ wakati wa usajili wa Juni-Agosti kwa kuwasaini wachezaji wenye majina makubwa na kuwasahaulisha kuhusu barua yao ya FIFA. Nini kilitokea? Sikuacha, nikawaambia usajili wa Simba haukuwa mapendekezo ya benchi la ufundi, napo hapa wakatokea wapingaji, lakini nini kinaendelea sasa? Jicho langu la tatu huwa linaona mbali zaidi, hasa kimpira.

Sasa linaona anguko lingine la kujitakia kwa maana rundo la wachezaji waliosajiliwa kwa mbwembwe nyingi katika usajili uliopita wanaondoka katika usajili huu wa dirisha dogo ili kupisha ‘thamani mpya’ za wachezaji. Nitawaambia kwanini wanaenda kuanguka wakati ni klabu iliyofanya usajili ghali zaidi msimu huu.

Kuongoza ligi si ‘kitu’ sababu ya kuwaaminisha watu kuwa Simba inakwenda kutwaa ubingwa wao wa kwanza baada ya kupita misimu mitano, ‘la-hasha’ kwani wameshafanya sana hilo, lakini kuna tatizo kubwa ambalo linaweza kumalizika katikati ya mwaka ujao wakati klabu itakapomaliza uchaguzi wake mkuu, ama Poppe ajiuzulu sasa katika nafasi yake.


Madrid Derby: Wanda Metropolitano kuandika historia hii leo hii

$
0
0

The Estadio Wanda Metropolitano ndio uwanja ambao Derby ya Madrid itapigwa jumamosi hii, utakuwa uwanja wa 16 kuwahi kutumika kwa kwa ajili ya mchezo huu wa mahasimu wa jiji la Madrid.

Ni ukurasa mpya wa upinzani uliodumu kwa zaidi ya karne kwa vilabu hivi vya mji mkuu wa Hispania.

Tangu vilabu hivi vilipoanzishwa, mechi baina ya Atletico na Real Madrid zimechezwa katika maeneo yote yenye vikubwa jijini Madrid.

Kipindi soka likiwa ndio linaanza kutambulika jijini Madrid na Spain, viwanja vilikuwa ndani ya Jiji la Madrid. Atletico Madrid wakiwa wanategemea dimba la Athletic Club mnamo 1905, walikutana katika uwanja wa Hipodromo – uwanja ambao ndio Madrid walikuwa wakitumia wakati huo..

Baada ya hapo wakaenda kucheza viwanja vya Fuente del Berro na Campo del Retiro, uwanja wa kwanza wa nyumbani wa Rojiblancos (Atletico).

Halafu uwanja wa Estadio O’Donnell, ukawa unatumika kwa mechi za nyumbani za ugenini, kwa timu zote, kama ambavyo Milan na Inter wanavyoutumia uwanja wa Stadio Giuseppe Meazza.

Dimba la Velodromo Ciudad Lineal lilitumika kwa ajili ya Derby mwaka 1923 kabla ya Estadio Chamartin na baada ya hapo uwanja wa mwanzo kabisa wa Estadio Metropolitano.

Vita vilikuja kuuharibu uwanja huo wa Atletico na ikawabidi waende kuhamia kwanza Campo de Vallecas na… baadae Chamartin.

Mpaka kufikia katikati mwa karne iliyopita timu zote zikapata viongozi/ maraid ambao walikuja kufanya mapinduzi na kuzipa mwanga timu hizo.

Hapo ndipo Santiago Bernabeu na Vicente Calderon vikajengwa na kuanza kutumika na vilabu hivyo.

Derby ya Madrid ndio mchezo ambao umejirudia sana katika soka la Hispania na pia umekuwa ukichezea mpaka nje ya mipaka ya nchi hiyo.

Katika michuano ya ulaya mwaka 1959, uwanja wa La Romareda ulitumika kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali wa Madrid Derby. Lisbon ukafuatia mwaka 2014 katika fainali na 2016 mtanange huo ukapigwa tena Giuseppe Meazza.

Rekodi za Manyika Jr zamkalisha Aishi Manula

$
0
0

Peter Manyika Jr ambaye ni golikipa wa Singida United amemkalisha  golikipa wa Simba Aishi Manula kwa kucheza mechi nyingi bila kuruhusu goli (clean sheets). Mechi ya jana ambayo Singida walishinda 1-0 dhidi ya Lipuli,Manyika alifikisha jumla ya michezo saba bila kufungwa katika mechi 10 za VPL zilizopita.

Manula ambaye ndiye golikipa namba moja wa kikosi cha Taifa Stars, hajaruhusu goli katika mechi tano za VPL kati ya mechi tisa alizocheza hadi sasa. Amezidiwa cleans sheets mbili na Mayika Jr lakini wawili hao wametofauiana katika idadi ya mechi walizocheza. Manyika tayari amecheza michezo 10 wakati Manula akiwa na mechi tisa huku leo akitarajiwa kucheza mechi yake ya 10 VPL wakati Simba itakapokuwa ikicheza dhidi ya Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine Mbeya.

Manyika Jr taratibu anarejea kwenye ubora wake baada ya kuondoka Simba alipokuwa ‘anachoma mahindi’ kwa muda mrefu. Uwepo wa magolikipa wa kigeni Vicent Angban na Daniel Agyei kwa nyakati tofauti ulipelekea Manyika Jr kupoteza nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza pale Msimbazi.

Jana Ijumaa November 17, 2017 Manyika Jr ameandika rekodi yake ya kucheza mechi saba bila kuokota mpira ndani ya nyavu zake katika mechi 10 ambazo amesimama langoni, huku mchezo wa jana ukiwa ni wa tano mfululizo bila kufungwa. Hili si jambo dogo kwake amefikia rekodi ya golikipa wa Azam Razak Abarola ambaye hajaruhusu goli katika mechi saba za VPL katika mechi tisa alizocheza.

Clean sheets za Manyika Jr katika mechi 10 za VPL msimu huu

  • Stand United 0-1 Singida United
  • Singida United 1-0 Kagera Sugar
  • Ruvu Shooting 0-0 Singida United
  • Ndanda 0-0 Singida United
  • Mtibwa Sugar 0-0 Singida United
  • Singida United 0-0 Yanga
  • Singida United 1-0 Lipuli

Clean sheets za Manula katika mechi 9 zilizopita VPL msimu huu

  • Simba 7-0 Ruvu Shooting
  • Azam 0-0 Simba
  • Simba 3-0 Mwadui
  • Simba 4-0 Njombe Mji
  • Mbeya City 0-1 Simba

Baba mzazi wa golikipa huyo Manyika ambaye ni golikipa wa zamani wa Yanga na Taifa Stars alishawahi kuiambia shaffihdauda.co.tz kuwa,  kushuka kiwango kwa kijana wake wakati akiwa Simba kulichangiwa na mambo mengi ya nje ya uwanja na kutozingatia miiko ya soka.

Badae Manyika Jr alirudi kwa mzee wake baada ya kugudua amekosa mwelekeo na kipaji chake kimekosa njia, alipokelewa na baba yake kisha kurejeshwa kwenye kituo cha magolikipa kinachomilikiwa na baba yake (Manyika Sr) pale Karume. Alianzishiwa mazoezi maalum ya kupunguza uzito na kuwekwa fit hatimaye akarejea katika hali yake.

Baba yake ambaye ndio meneja wa mtoto wake alisema, mkataba wa Manyika Jr na Simba utakapomalizika hawatakubali kuongeza mwingine badala yake watamtafutia timu nyingine ambayo wataweka masharti ya kimkataba kuhakikisha anacheza mechi nyingi pale anapokuwa fit, hapo ndipo safari ya kwenda Singida United ikawadia baada ya timu hiyo kujiridhisha na ubora aliokuwanao Manyika Jr wakati huo.

Ubora wa Manyika katika milingoti mitatu umemrejesha Stars

Baada ya kufanya vizuri katika mechi za ligi kuu, kocha wa Stars Salum Mayanga alianza kumuita Manyika Jr kwenye timu ya taifa ili kutoa changamoto kwa Aishi Manula. Inawezekana wengi waliamini Manyika ndio basi tena, lakini baada ya kugundua alikosea wapi na anatakiwa kufanya nini amesimama kwa mara nyingine na kuwaamisha watu bado kipaji chake hakijapotea.

Manyika Jr vs Abarola

Wote hawajaruhusu magoli katika mechi saba hadi sasa, Manyika amecheza mechi 10 wakati Abarola amecheza mechi tisa. Abarola ndio wa kwanza kufikisha mechi saba bila kuruhusu goli lakini Manyika ameifikia rekodi hiyo ya golikipa kutoka Ghana baada ya mchezo wa jana Singida United 1-0 Lipuli.

Manyika Jr anampiku Abarola kwa kucheza mechi tano mfululizo bila kufungwa goli, katika mechi tano zilizopita mfululizo Manyika Jr ameidakia Singida United bila kuruhusu wavu wa goli lake kucheza. Abarora aliwahi kucheza mechi nne mfululizo za mwanzo wa ligi bila kufungwa, Abarola aliruhusu goli la kwanza dhidi ya Singida United timu hizo zilipotoka sare ya kufungana 1-1 kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma

Leo Jumamosi Nov 18, 2017 Abarola yupo kwenye nafasi ya kufikisha mechi nane bila kufunga na kumwacha  Manyika Jr endapo hatafungwa kwenye mchezo kati ya Njombe Mji dhidi ya Azam kwenye uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe.

Manuel Pochettino mbabe wa Wenger ambaye hajawahi kushinda Emirates

$
0
0

Mechi 6 za mwisho ambazo Arsenal walicheza zidi ya Tottenham Hotspur walishindwa kupata ushindi, wamesluhu 4 na kupoteza 2 na hawa ndio wapinzani wa Arsenal waliowaonea sana katika mechi 6 za mwisho.

Lakini katika michezo 32 iliyopita Tottenham Hotspur waliyocheza zidi ya Arsenal ugenini wameshinda michezo 2 tu na mara ya mwisho ilikuwa 2010 walipoipiga Arsenal bao 3 kwa 2 katika uwanja wa Emirates.

Uwanja wa Emirates unawapa jeuri Arsenal hivi sasa kwani hadi sasa wameshinda michezo 10 mfululizo ambapo ndio ushindi wao mrefu katika uwanja huo tangu waanze kuutumia.

Kocha Maurcio Pochettino naye amekuwa akihangaika zidi ya timu zilizomaliza top six mwaka jana kwani katika mechi 16 alizocheza na timu hizo ameshinda mchezo mmoja tu na kupokea kipigo mara 9 na suluhu 6.

Maurcio Pochettino hajawahi kupoteza mchezo hata mmoja wa London ya Kaskazini tangu afike Tottenham lakini hajawahi kuifunga Arsenal wakiwa kwao wala kufungwa (D4) lakini amewafunga Gunners mara 2.

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Harry Kane kama akifunga mchezo wa leo atakuwa mchezaji wa kwanza katika Epl kuwahi kufunga angalau mabao 2 katika michezo 4 ya ugenini.

Kila shabiki wa United angependa kuyasikia haya kuelekea mchezo wao na Newcastle

$
0
0

Katika michezo 32 iliyopita ya Epl kati ya Newcastle na Manchester United zilizopigwa katika uwanja wa Old Traford, United wamepoteza mechi moja tu huku wakishinda mara 22 na suluhu 9.

Newcastle wamepoteza mechi nyingi zaidi zidi ya Manchester United katika historia kuliko walivyopoteza zidi ya timu yoyote ile Epl ambapo hadi sasa wameshapoteza jumla ya michezo 84.

Kama leo Manchester United watashinda mchezo wao bila kuruhusu goli itakuwa mara yao ya kwanza kushinda michezo 7 bila kuruhusu nyavu yao kuguswa tangu wafanye hivyo msimu wa 2009/2010.

Newcastle United wanakwenda Old Traford katika kipindi ambacho uwanja huo unaonekana kuwa mgumu kwa wapinzani kwani michezo 22 iliyopita hakuna mpinzani aliyeshinda OT huku mechi 6 za mwisho United wakishinda zote bila kuruhusu bao.

Mchezo wa leo unaweza kuwa mchezo mwingine ambao Lukaku atakuwa katika presha kwani baada ya kufunga bao 11 katika mechi 10 za mwanzo, hakufunga tena katika mechi 7 mfululizo zilizopita.

Mchezo wa leo utakuwa jambo kubwa kwa mlinzi wa kulia wa Manchester United ambapo hii leo kama akicheza basi utakuwa mchezo wake wa 300 tangu aanze maisha ya soka.

Habari inayowapa raha mashabiki wa Manchester United ni kwamba leo Zlatan Ibrahimovich, Paul Pogba na Marcos Rojo wote watakuwa fiti kuikabili Newcastle.

Kwa upande mwingine kocha wa klabu ya Newcastle Rafael Benitez atakuwa kocha wa kwanza kuifunga United Old Traford akiwa katika vilabu vitatu tofauti, ameshafanya hivyo na Chelsea akafanya hivyo na Liverpool.

Mwanamke huyu avunja rekodi “Madrid Derby” iliyodumu kwa miaka 86

$
0
0

Ukiachana ns ile Derby ya kaskazini mwa London itakayopigwa pale nchini Uingereza hii leo, kule katika ligi kuu nchini Hispania katika dimba la Wanda Metrpolitana kutakuwa na derby nyingine.

Real Madrid ambao msimu huu wanaonekana kuchechemea watakuwa wageni wa Atletico Madrid ambao nao toka msimu uanze wanaonekana kutokuwa vizuri kama ilivyo kwa majirani zao.

Py Laurance anaweza kuwa mtu pekee ambaye anakwenda katika mchezo huu akiwa na presha kubwa kwani hatapenda timu yoyote kati ya Atletico Madrid au Real Madrid ipoteze mchezo wa hii leo.

Py ni mama mzazi wa mlinzi wa kushoto wa Atletico Madrid Theo Hernandez lakini vile vile Py huyuhuyu ndio mama mzazi wa mlinzi wa Real Madrid Lucas Hernandez jambo linalomfanya kushabikia timu zote mbili.

Katika mahojiano na jarida la Marca mwanamama huyu ameeleza kwamba kabla ya mechi ya leo aliwaita na kuwaambia kwamba anawapenda sana na akiwasisitiza wasipigane kwa kuwa wao ni ndugu.

Py anakuwa mzazi wa kwanza kukutanisha watoto wake katika mchezo wa Madrid Derby tangu jambo kama hili lilipotokea katika msimu wa mwaka 1929/1930 na tangu kipindi hicho hakuna aliyeweza kuvunja rekodi hiyo.

Real Madrid na Atletico Madrid wote wana alama sawa (23) na atakayeshinda katika mchezo wa leo atakaa juu ya mwenzake na kupunguza pengo la alama na vinara Barcelona.

Viewing all 9000 articles
Browse latest View live