Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all 9000 articles
Browse latest View live

Tanzania imepokea ugeni, ni mchezaji wa zamani wa Liverpool

$
0
0

Asikwambie mtu Bongo nzuri, inavutia na tamu, kama ulikuwa hujui chukua hii toka kwangu, beki kitasa wa zamani wa Liverpool Martin Skrtel ambaye kwa sasa anakipiga Fenerbahce ameshuka Kilimanjaro International Airport kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali nchini.

Taarifa za ujio wake nilizinyapia kupitia account yake ya instagram baada ya ku-post tickets tatu (yeye, mkewame na mtoto) zikionesha wanakuja kutembelea Tanzania.

Mishale ya saa 7:30 usiku jamaa akatua zake nchini pamoja na familia yake.


Mfahamu Mganda hatari anayetarajia kucheza kombe la dunia mwaka huu.

$
0
0
Haijalishi umezaliwa mazingira gani. Wala usimlaumu Mungu kwamba wazazi wako walizaliwa au waliishi maisha ya tabu. Huenda upo Kibondo au kasulu unawaza utafika lini Dar.

Huenda upo Rombo unaenda kulima viazi Rongai upate basikeli ya kwenda Kenya kununua vitunguu. Wala usiwaze sana. Kuna mtu anaitwa N’golo Kante alikuwa muokota makopo. Yupo Zinedine Zidane Wazazi wake walikuwa wakimbizi. Wewe muombe Mungu.


Wakati Mtanzania Yussuf Poulsen akisali kuomba aitwe kwenye kikosi cha kombe la dunia kitakachoiwakilisha Denamrk, Waganda nao watapeleka maombi yao kumuombea Sisto Pione.

Katika klabu Midtjylland ndipo Sisto alikutana na Riddersholm. Kutokana na jitihada zake alipandishwa katika kikosi cha wakubwa. Sisto ni mganda. Wala sio mganda kwa asili tu ila pia ni mganda kwa kuzaliwa.


Wakati sisi tunajivunia Samatta kucheza ulaya waganda wao wanajivunia kuwa na mchezaji wa Kiganda kule Urusi kwenye kombe la Dunia akiiwakilisha taifa la Denmark. Kocha Riddersholm ndiye aliyempa nafasi katika kikosi cha wakubwa.

Wachezaji wengi wa kibongo wanapenda maisha ya uree ree. Hawajitumi wapo wapo tu kama mizigo. Katika klabu ya FC Midtjylland wachezaji walipaswa kufanya mazoezi kwa masaa 12 kwa wiki. Sasa Sisto kwa kuwa alikuwa na malengo zaidi alikuwa anapiga mashuti, krosi na kukimbia mpira kwa zaidi ya masaa 24 kwa siku 5.


Mwaka 2014 kocha Glen Riddersholm ambaye alikuwa mkufunzi wa timu ya vijana ya FC Midtjylland, . “kuna mchezaji nilikuwa namuona wa gaofauti kabjsa na wenzake, kila mara ukipita uwanja wa mazoezi unamkuta pekee yake.

Ilikuwa nadra sana hasa katika mazingira ya joto kama hapa nchini kumkuta mchezaji mdogo yupo juani anakimbia. Pione alikuwa wa tofauti . Mwenyewe alinishangaza, kiujumla nina amini kuna wachezaji wakiobarikiwa na wachezaji wenye jitihada, kwangu mimi Sisto alipewa vyote.”

Sisto ni mzaliwa wa Uganda on 4 February 1995. Alizaliwa kipindi Augustino Mrema akiwa wamoto wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza wa Tanzania wa vyama vingi. Kisha baadae wazazi wake walielekea nchini Sudan. waliishi maisha ya tabu sana kabla hawajakimbilia ulaya. Walifikia katika mitaa ya mabanda yaani uswahilini pajulikanpo kama Hoejslev, kaskazini mwa mji wa Jutland nchini Denmark. Sisto ana ndugu 8 na yeye ni 9 kayika familia yao. Wote walienda shuleni ispokuwa yeye shule yake ilikuwa soka.


Walipokuwa Sudan walikuwa wakulima. Kablda hawajazamia Denamrk kila mtu kwenye familia alikuwa na jukumu la kuhakikisha maisha ya familia nzima yanasonga mbele. Walipokuwa Denmark walihamia mji mwingine wa Tjørring ambako Sisto alionekana na klabu ya Midtjylland.

Ndugu Jyllands-Posten aliitembelea familia ya akina Sisto umbali wa kilometa 60 kutoka mji wao wa awali kusini mwa Hoejslev Stationsby.

Katika maisha yake ya soka alianzia katika klabu bora na kubwa kabisa nchini Denmark. Mganda huyu ilikuwa kama ngekewa kwake. Sio ngekewa ila ni jitihada.

Kuna wachezaji wamepata nafasi kubwa katika vilabu vikubwa lakini wanashindwa kutumia fursa. Leo Adam Salamba na Mohamed Rahsid wamejiunga Simba lakini je wanajua thamani ya jezi ya Simba au wao wanawaza wapate mpunga wanunue mkoko na wapate madem hapa mjini?


Nahodha wa Denmark Simon Kjaer ni mmoja wa wachezaji wakubwa waliotkkea kwenye klabu hii. Achilia mbali bekiwa West Ham Winston Reid na nyota wa Celtic Erik Sviatchenko.

Jina lake lilianza kutamkwa sana mnamo mwaka 2015. Sisto aling’aa na klabu yake ya Midtjylland walipotwaa ubingwa wa ligi na msimu uliofuata aliifunga Manchester United nje ndani kwenye michuano ya Europa League.

Kila klabu ya Ulaya ilianza kummendea hasa baada ya kuonekana kwamba ni aina ya viungo ambao hawahitaji mtu kumzunguka ili acheze vizuri. Alikuwa na uwezo wa kucheza namba 6,8,10 bila wasiwasi wowote. Mwisho wa siku alitimkia Celta Vigo. Moja kwa moja alijumuishwa kikosini na pia alijatwalia namba kikosi cha timu ya taifa.

Sisto alipata uraia wa Denmark mnamo Desemba 2014 pia aliitwa kwenye kikosi cha U-21. Alianza kuichezea Denmark kila mchezo tokea Oktoba 2016 na alifunga goli lake la kwanza kwenye mchezo dhidi ya Panama.

Kilichoshangaza wengi ni kitendo cha kufunga goli huku akiwa hajafunga vizuri kamba za viatu kama Diego Maradona au Lionel Messi.

kocha mkuu wa Denmark Åge Hareide, amejaribu kutengeneza muunganiko mzuri wa Sisto na Christian Eriksen. Faida kubwa atakayopata Sisto ni kwamba wapinzani watamkodolea zaidi macho Ericksen na watamsahau sisto ambaye anaweza kufanya makubwa na kushangaza wengi.

Familia ya Sisto imekuwa bega kwa bega na ndugu yao. Sisto alipoitwa kwenye kikosi cha U21 Familia nzima ilivuruga mkutano ule wa kocha mmuu kwa kuanza kuimba na kucheza ngoma za kiafrika tukio ambalo lilizua gumzo kubwa sana. Ndugu waliofika walikuwa Lobolohitti, Margaret, Akari, Cathy, Angelo, Lopunyak, Adeleide na Regina.

Wale wa ndondo Cup nwakumbusha mchezaji bora atakwenda Uturuki. Atakwenda Besiktas. Ashindwe yeye sasa.

Wereba Sisto Tunaalabagana Russia, na Tambula bulungi

Hicho nilichoandika hapo Muulizeni Owki atawatafsiria.

Makala hii imeandaliwa na Privaldinho (Instagram)

#RoadToRussia, mkosi wa goli 3 unavyoitafuna “Three Lions” kombe la dunia

$
0
0

Usiku wa leo timu ya taifa ya Uingereza itakuwa katika uwanja wao wa nyumbani kuwakaribisha Nigeria katika kujiandaa na kombe la Dunia, ni mchezo muhimu kwa pande zote mbili kujiweka sawa kabla ya kuelekea nchini Urusi.

Kuna jambo la ajabu kuhusu timu ya taifa ya Uingereza ambalo mashabiki wao wengi mitandaoni wanalijadili, bao 3. Uingereza wanaomba chonde chonde usiku wa leo wasiwafunge Nigeria magoli 3.

Rekodi zinaonesha kwamba timu ya taifa ya nchini Uingereza ilipata matokeo mabovu katika kombe la dunia baada ya kupata ushindi wa mabao 3 katika mechi ya mwisho ya kujiandaa na kombe la dunia waliyocheza Wembley kwenye misimu mitatu mfululizo iliyopita.

Kombe la dunia 2014, mchezo wa mwisho wa maandalizi ya kombe la dunia kwa Three Lions mwaka 2014 ilikuwa dhidi ya Peru katika dimba la Wembley, katika mchezo huu Three Lions waliibuka kidedea kwa mabao 3-0.

Daniel Sturridge, Gary Cahill na Phil Jagielka walikuwa wauaji katika mchezo huu, lakini walipokwenda katika michuano ya kombe la dunia nchini Brazil, Uingereza walishuhudia wakiondolewa katika hatua ya makundi.

Kombe la dunia 2010, mwaka 2010 nao Uingereza mchezo wao wa mwisho kujiandaa na kombe la dunia ulipigwa Wembley, safari hii walicheza dhidi ya Mexico na kuibuka kidedea kwa mabao 3-1.

Ledley King, Peter Crouch na Glen Johnson waliiua Mexico, baada ya hapo Waingereza wakakwea pipa na kwenda zao nchini Afrika Kusini walipofika kwa Madiba wakadharilika hatua ya 16 bora kwa kupigwa na Ujerumani bao 4-1.

Kombe la dunia 2006, Steven Gerrard, John Terry na Peter Crouch waliifunga Hungary bao 3-1 mwaka 2006 katika mchezo wa mwisho wa Uingereza kabla ya kombe la dunia na safari hii mchezo ulipigwa Old Traford.

Walipokwenda Ujerumani walisogea sogea hadi robo fainali, lakini Wareno wakawaondoa kwa matuta huku Wayne Rooney akipewa moja ya kadi nyekundu maarufu zaidi katika michuano hii.

Usiku wa leo ni Uingereza na Nigeria pale Wembley, je kitakachotokea kitaathiri safari ya Urusi?

Mtibwa ilivyouchukua ubingwa mikononi kwa Singida United

$
0
0

Mabao 3-2 yametosha kuifanya Mtibwa kuwa bingwa mpya wa Azam Sports Federation Cup mbele ya Singida United kwenye mchezo wa fainali uliochezwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Watu wengi walikuwa wanaichukulia poa Mtibwa kwa kulinganisha wachezaji wake na wale wa Singida United, timu ambayo imesajili wahezaji wengi wa kimataifa.

Ukiniuliza Mtibwa waliizidi wapi Singida United kwenye mchezo wa fainali nitakwambia ni uzoefu wa wachezaji waliopo Mtibwa lakini makosa ya golikipa wa Singida United yaliwarahisishia Mtibwa kupata matokeo.

Tangu mwanzo kabisa , Zubery Katwila alikuwa anaibadilisha Mtibwa kulingana na timu anayokutana nayo. Kuwepo kwa wachezaji wengi wenye uzoefu kama Nditi, Henry Joseph na Dickson Daud ni wachezaji ambao wamecheza mechi nyingi sana kitaifa na kimataifa.

Wachezaji wazoefu wanajua namna ya kuwafanya wachezaji wa timu pinzani washindwe kutekeleza majukumu yao. Singida inawachezaji wazuri kama Kutinyu lakini walichokuwa wanafanya Mtibwa ni kutowaruhusu Singida kuvheza kwenye eneo lao la hatari.

Mtibwa walikuwa wanaibutua mipira yote iliyokuwa inakuja kwenye eneo lao la hatari. Ukiangalia magoli waliyofunga Singida United yalitokana na makosa yaliyofanywa na mabeki wao katika wakati ambao walidhani wanaweza kutuliza mpira nchini (mfano goli la Kutinyu).

Uzoefu na game plan waliyokujanayo leo Mtibwa kuhakikisha hawawapi nafasi Singida kutengeneza nafasi nyingi huku wao wakijitahidi kutumia mipira iliyokufa kwa sababu wanawavhezaji kama Kelvin Kiduku ambao ni wazuri wa kupiga mipira hiyo (mfano goli la pili kona iliyopigwa na (Baba Ubaya).

“Mechi ilimshinda mwamuzi”-Shaffih Dauda

$
0
0

Tukio la mwamuzi Emmanuel Mwandembwa kutoa kadi nyekundu kwa Hassan Dilunga halau mchezaji huyo hakutoka limewavuruga watu kibao waliokua wanafatilia mchezo wa fainali ya Azam Sports Federation Cup vs Singida United.

Mwandembwa alijichanganya wakati anamwonesha kadi ya njano Hassan Dilunga alidhani ni kadi ya pili ya njano kwa mchezaji huyo kisha akamkandamiza na ‘umeme’.

Lakini kumbe ilikuwa ni kadi ya kwanza kwa Dilunga, mwamuzi alijichanga akadhani anatoa kadi kwa Issa Rashid ‘Bada Ubaya’.

“Wakati mwingine waamuzi wanahitaji kuwa na uzoefu ukilinganisha na mechi wanazopangiwa, mwamuzi wa leo mechi ilimshinda.”

“Mara nyingi maamuzi aliyokuwa akiyatoa hakuwa na uhakika nayo, alikuwa kama anabahatisha ndiyo maana tukio la kadi nyekundu linaonesha alipoteza focus.”

“Hakuwa makini ndio maana matukio mengi sana yalikuwa yanamzidi.”

Shaffih Dauda amchambua Barthez

$
0
0

Shaffih Dauda amezungumzia magoli aliyoungwa golikipa wa Singida United Ally Musta ‘Barthez’ kwenye mchezo wa fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Mtibwa Sugar ambao wameshinda taji hilo.

Barthez amefungwa magoli yanayofanana na yele aliyowahi kufungwa enzi zake wakati yupo Yanga.

“Ally Mustapha ‘Barthez’ ni mbovu wa mipira ya juu, kama utakumbuka goli la kona alilifungwa leo na Baba Ubaya ni kama goli ambalo alifungwa na Shiza Kichuya akiwa Yanga. Goli la kwanza alilofungwa na Salum Kihimbwa linafanana na ambalo aliwahi kufungwa na Okwi akiwa Yanga.”

“Barthez ni golikipa mwenye uwezo anashindwa kuhimili mipira ya juu kutokana na kimo chake (mfupi) ndiyo maana wenzetu walioendelea (Ualaya) wanatumia kanuni yao ya golikipa lazima awe mrefu, sio wajinga.”

“Ufupi wa Barthez umekuwa disadvantage kwa Singida United hususan mbele ya wachezaji wenye uwezo mzuri wa kupiga mipira juu inakuwa.”

Morocco katambulishwa Singida kaona mapungufu fainali ASFC

$
0
0

Timu ya Singida United imemtangaza kocha mpya Hemed Morocco kuchukua nafasi ya Hans van Pluijm ambaye ameshatangazwa kuwa kocha mpya wa Azam.

Baada ya game ya fainali ya Azam Sports Federation Cup ambapo Singida United ilipoteza kwa kufungwa 3-2 na Mtibwa Sugar, Morocco amesema timu yake mpya ilipoteza umakini na hiyo ndio sababu kubwa ya kuruhusu goli la tatu.

“Kila kitu kipo katika hatua za mwisho, nitasaini mkataba wa mwaka mmoja Singida United.

“Mechi ilikuwa nzuri imeleta hamasa halisi ya fainali, Mtibwa walitawala sana kipindi cha kwanza wakaweza kufunga magoli mawili. Kipindi cha pili Singida wakaingia na nguvu mpya wakafanikiwa kusawazisha magoli.”

“Singida United ilipoteza umakini ikaruhusu goli la tatu ambalo liliamua mechi.”

Kuna uhusiano kati ya marehem Shose na ASFC? “Nimetokanae mbali sana”-Henry

$
0
0

May 27, 2017 Simba ilishinda ubingwa wa ASFC baada ya kuifunga timu iliyopanda daraja (Mbao FC) kwenye mchezo wa fainali lakini siku moja baadaye Simba ilipata pigo kwa kumpoteza shabiki wake Shose Fidelis aliyefariki kwa ajali ya gari wakati wanatoka Dodoma kuelekea Dar.

Ni mwaka mmoja sasa tangu Shose afariki, lakini baada ya fainali ya ASFC June 2, 2018 mchezaji wa zamani wa Simba Henry Joseph baada ya kuisaidia Mtibwa kuchukua ubingwa huo alivaa t-shirt yenye picha ya Shose ikiwa imeandikwa ‘R.I.P SISTER SHOSE FIDELIS’.

Henry Joseph amesema ameamua kufanya hivyo ili kumuenzi Shose ambaye alifariki baada ya fainali ya kombe la ASFC ndio maana ameimevaa baada ya mchezo wa fainali.

“Ni dada yangu ambaye nimetokanae mbali sana, alifariki kwenye fainali baada ya Simba kutwaa ubingwa kwa hiyo namkumbuka sana alikuwa mtu wa kipekee na kila mtu anajua.”

“Hii nimevaa kwa niaba ya watu wote wa Makongo Secondary kwa sababu tumesoma pamoja.”


“Singida ilicheza kufurahisha mashabiki”-Kocha Mtibwa

$
0
0

Mtibwa Sugar imekutana na Singida United kwa mara ya tatu, imeshinda mechi mbili na kutoka sare mchezo mmoa. Singida United imepigwa bao 6-2 katika mechi mbili zilizopita (Singida United 3-0 Mtibwa Sugar-VPL, Mtibwa Sugar 3-2 Singida United-ASFC na sare moja Mtibwa 0-0 Singida United).

Kocha wa Mtibwa Sugar Zubery Katwila ameelezea sababu ya kuwapa vipigo Singida United kila wanapokutana na kuongeza kuwa huenda wachezaji wa Singida wanapenda kucheza ili kufurahisha mashabiki.
Wanatawala sehemu kubwa ya michezo  lakini wanashindwa kuimaliza mechi.

“Unatakiwa ku-win game sio mechi kwa hiyo wao wali-win mechi sisi tumewin game.”

DoneDeal: Kutinyu kaungana na Ngoma Azam

$
0
0

Kiungo wa Singida United Tafadzwa Kutinyu anaungana na kocha Hans van Pluijm kuelekea Azam FC kwa ajili ya msimu ujao.

Meneja wa Azam FC Philip Alando amethibitisha usajili wa Kutinyu kutoka Singida United.

“Kweli tumememsajili Kutinyu, amesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka mwingine”-Alando

Kutinyu alijiunga na Singida United kabla ya kuanza kwa msimu huu akitokea klabu ya Chicken Inn ya Zimbabwe na baada ya kufanya vizuri ndani ya msimu mmoja akiwa Singida sasa anaelekea Azam.

Akiwa Azam ataungana na raia wenzake wawili kutoka Zimbabwe Bruce Kangwa na Donald Ngoma ambaye pia amejiunga na klabu hiyo hivi karibuni.

Msuva kaendesha kliniki ya soka mbele ya Mwakyembe

$
0
0

Mchezaji wa club ya Difaa El Jadida na Taifa Stars Simon Msuva leo Juni 3, 2018 ameendesha kliniki kwa ajili ya kuwasaidia vijana wa umri wa miaka 15 zoezi ambalo lilifanyika uwanja wa JMK Park.

Kliniki hiyo imeandaliwa na kampuni ya ISDI ambayo inamsimamia Msuva katika masuala mbalimbali ndani na nje ya uwanja.

Waziri mwenye dhamana ya Michezo Dr. Harrison Mwakyembe alihudhuria tukio hilo ambapo aliwapa motisha vijana kwa kuwataka wafuate nyayo za Msuva.

Siku 11 kuelekea Urusi, ni zamu ya ulaya tena.

$
0
0

Na Elizabeth Lyavule

Ikiwa zimesalia siku kumi na moja tu mataifa 32 kuanza kucheza fainali za 21 za kombe la dunia huko nchini Urusi, vikosi vyote wameanza maandalizi kujinoa vikali na michuano hiyo na wameonesha ubora wa hali ya juu lakini je nani kuibuka kidedea na kupokea kijiti kwa timu ya taifa ya Ujerumani kwa kubeba kombe hili lenye ubora na hadhi ya juu duniani?

Miaka ya 80 na 90 timu kutoka bara la America (Brazil na Argentina) walikua na vikosi bora hivyo haikua ajabu kubeba kombe hilo mara kwa mara hata hivyo upepo ulikuja kubadirika ghafla na ufalme huo ukahamia ulaya timu za Ujerumani, Hispania, Italia, zikiimarika na kufanya mapinduzi makubwa kisoka hivyo kuwapa mtihani mgumu timu kutoka bara la America, Asia na kwingineko kuchukua taji hilo.

Ndani ya fainali kumi zilizopita katika michuano hii ya kombe la dunia, takwimu zinatuonesha matokeo yafuatayo :

Fainali za mwaka 1978. Mwenyeji wa fainali hizi alikuwa ni Argentina, alifanikiwa kumfunga Uholanzi 3-1 ndani ya dakika 90 hivyo kubeba kombe hilo kunako ardhi ya nyumbani kwao

Fainali za mwaka 1982. Zilifanyikia nchini Hispania, huku Italy akiwa bingwa kwa kumfunga Ujerumani 3-1 fainali.

Fainali za mwaka 1986 zilifanyika nchini Mexico na ni Argentina tena aliibuka shujaa nakubeba kombe safari hii akimfunga Ujerumani mabao 3-2.

Fainali za mwaka 1990 Italy akiwa mwenyeji wa michuano hiyo tulishuhudia Ujerumani ikibeba kombe kwa kumfunga argentina goli 1-0

Fainali za mwaka 1994 zikipigwa kule Marekani, ni Brazil walifanikiwa kubeba kombe wakimfunga Italy kwa mikwaju ya penalty 3-2 hii ni baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya bila kufungana

Fainali za mwaka 1998 kule Ufaransa zilishuhudia mwenyeji timu ya Ufaransa akiwa bingwa kwakumfunga Brazil mabao 3-0

Fainali za mwaka 2002 nchi mbili zilikua mwenyeji (Japan na Korea kusini) na si wengine ni Brazil alibeba kombe safari hii akimfunga Ujerumani goli 2-0

Fainali za mwaka 2006 zilifanyikia ujerumani, tukashuhudia Italy akiwa bingwa alimfunga Ufaransa kwa mikwaju ya penalty 5-3 baada ya dakika 120 kwenda sare ya goli 1-1

Fainali za mwaka 2010 kwa mara ya kwanza zililetwa bara la Afrika kule Afrika kusini huku zikishuhudia Hispania kuwa mabingwa wakimfunga Uholanzi goli 1-0 ndani ya dakika 120

Fainali za mwaka 2014 zilifanyika kule Brazili, si wengine bali timu ya Ujerumani ilimfunga Argentina katika fainali goli 1-0 na kubeba kombe hilo

Hivyo katika historia ya michuano hii nchi ya Brazil iliyopo katika bara la Amerika inaongoza kuwa na mafanikio kwakulibeba kombe hili mara tano ikifuatiwa na Ujerumani iliyopo bara la ulaya kwakubeba mara nne hata hivyo ndani ya miaka kumi kama nilivyokuonesha takwimu.

Ulaya wamebeba mara sita na Amerika mara nne tu na kwa upepo unavyovuma naimani kombe linakwenda ulaya tena mfululizo hivyo kuwa la 7 katika miaka kumi maana vipaji na ubunifu ukiongeza na soka la ushindani vimehamia ulaya na majina ya mtu mmoja mmoja vimebaki kwa timu za amerika

Brazil wamekuwa watamu

$
0
0

Zikiwa zimesalia siku 12 kuelekea fainali za kombe la  dunia ndani ya Ardhi ya Putin nchini Urusi ,timu ya taifa ya Brazil  imekuwa ya moto sana .
Mchezo wa Leo dhidi ya timu ya taifa ya Croatia unakuwa mchezo wa 20 kwa mwalimu Titte na tayari katika michezo 20 Brazil wameshinda jumla  ya michezo kumi na sita (16), Goli la leo na Neymar likikuwa goli la 43 na Firmino akafunga goli la pili ambalo limekuwa goli la arobaini na nne (44) kwenye michezo 20 ni uwiano wa goli mbili (2) kwa kila mchezo ,wameruhusu kufungwa magoli 5 huku wakicheza michezo 15 bila kuruhusu nyavu zao kuguswa .

Brazil ndio taifa lenye  rekodi nzuri kwenye  mashindano haya makubwa ya mpira wa miguu kwa ngazi ya tumu za taifa duniani kwani katika mara 25 ambazo kombe la dunia limechezwa Brazil imekosa mara 5 tu huku ikiwa imeshinda mataji matano ya kombe la Dunia.

Kikosi cha Brazil kina nyota kama Neymar (Psg), Ederson (City),Willian (Chelsea), G.Jesus (City),T.Silva (Psg),Casemiro( Madrid) ,Marcelo  (Madrid ) ,Countinho (Barcelona ),Firmino (Liverpool ),Ferndandinho (city) na wengine wengi.

Timu ya Taifa ya Brazil imepangwa  kwenye kundi pamoja ya mataifa ya Uswizi ,Croatia na Serbia . Je Brazil watarudisha Samba Nchini Urusi.?

Mkemi amejivua uongozi Yanga

$
0
0

Baadhi ya viongozi wa Yanga wameendelea kuikimbia klabu hiyo kwa kujiuzulu nafasi zao za uongozi.

Mjumbe wa kamati ya utendaji Yanga Salum Mkemi ambaye mara kadhaa alihusishwa kuikacha Yanga leo ameandika waraka ambao umesambaa kwenye mitandao akitangaza kupisha nafasi kwa watu wengine kuongoza.

Ujumbe wa Mkemi kujiuzulu uasomeka hivi: Kusema kweli viongozi hatukwepi lawama hizi, kwa hakika tumepata aibu kubwa.

Nikiwa kama kiongozi napaswa kuwajibika kwa hili ni hatua nzuri ya kupisha mawazo mapya kwa wanachama wengine kuongoza timu na kutupeleka mbele.

Pia ningependa kuwashauri viongozi wenzangu wajitathimini na ikibidi nao waachie ngazi ufanyike uchaguzi mkuu kwa pamoja tupate viongozi wapya kabla msimu mpya haujaanza.

Napenda kuomba samahani kwa wote niliowakwaza na nimesamehe wote walio nikikwaza.

Naomba kutamka rasmi mimi Salum Mkemi
najaiuzulu nafasi zangu zote za uongozi ndani ya klabu yangu pendwa Young Africans Sports Club ‘YANGA’ kuanzia tarehe ya leo 03/06/2018.

Nawatakia kila la heri viongozi wenzangu waliobaki na kuwataka radhi tena wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga kwa matokeo mabovu tuliyopata naomba tusamehane.

Nawashukuru kwa muda mlionipa kuiongoza klabu hii kubwa Afrika naomba Kuwajibika kwa kujiuzulu.

Wenu mwanachama mwenzenu mtiifu.

Salum Mkemi.

NIMENG’ATUKA

Breaking News: Fred kutua Man U, sakata la kocha mpya Chelsea

$
0
0

Katika taarifa zilizoshika kasi barani ulaya ni taarifa kuhusiana na usajili wa nafasi ya ukufunzi katika klabu ya Chelsea.

Habari za fuku fuku amefukua kwamba Laurent Blanc kocha wa Zamani wa PSG ndiye anayeongeza katika orodha ya makocha wanaowania kibarua cha Antonio Conte. Kocha wa zamani wa Napoli Maurizzio Sarri ameondolewa katika kinyang’anyiro hicho. Muda wowote kuanzia sasa Blanc atatajwa kuwa kocha mkuu wa Chelsea.

De gea auza mechi

Katika pita pita zetu hasa hasa mechi za kimataifa. David De gea amefanya makosa ambayo yameisaidia timu ya taifa ya Switzeland kupata bao la kusawazisha mnamo dakika 62 katika mchezo wa kirafiki.

Taarifa pia zinadai Dani Carvajal bado amepewa muda wa kuuguza jeraha lake ili kuona kama kuna uwezekano wa yeye kwenda Russia.

Nafasi yake kwa sasa ipo chini ya kinda wa Real Sociedad ambaye katika mchezo wa leo amefunga bao lake la kwanza ikiwa ni mechi yake ya tatu tu kwa timu ya taifa.

Hapa saasaa.. wale mashabiki wa klabu ya Manchester United watakuwa kesho wanakenua tu baada ya kiungo wa Kibrazil wa Klabu ya shaktar Donetsk Fred kukubali kujiunga na Mashetani wekundu.

Fred atasafiri mpaka Carringhton ambako atakwenda kufanyiwa vipimo vya afya leo chanzo ni skysports

Mo Salah mambo ni shwari. Madaktari wa Misri waliosafiri nia Salah mpaka mjini Vakencia kwa ajili ya vipimo na matibabu wamesema Salah agakuwa fiti na mpaka sasa haki yake sio mbaya.

Wamesema watahitaji wiki tatu kuweka kila kitu shwari.

Wakala wa Fekir amesema hakuna makubaliano yaliyofanywa kati ha Liverpool na Lyon kuhusiana na mchezaji huyo.

“Mimi nimeshaongea na mabosi wa Liverpool sawa, lakini hili dili bado sana, kila kitu kitakuwa sawa endapo tu Liverpool watakutana na Michael Aulas pamoja na Lyon.

mwisho kabisa kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery ameishawishi bodi ha Arsenal kuhakikisha inaoata huduma za Steven Nzinzi wa Seville na muda wote kuanzia sasa atatua klabuni hapo.


Samatta ameomba ushauri Taifa Stars ifuzu AFCON

$
0
0

Nahodha wa timu ya faifa ya Tanzania Mbwana  Samatta ametoa fursa kwa wadah kushauri chochote ambacho kinaweza kuifanya Stars ifuzu michuano ya AFCON 2019.

Kupitia ukurasa wake wa instagram na twitter, Samatta ame-post ujumbe wa kuomba ushauri.

“Hivi ukipata nafasi ya kushauri chochote ambacho kinaweza kuifanya ‘taifa stars’ kupata tiketi ya AFCON mwakani inadhani ungeshauri jambo gani? Nini kifanyike? Sina maana ushauri utafatwa au la lakini tuongelee tu hili jambo hapa. Lets start.”

Stars ipo Kundi L kwenye mapambano ya kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika ikiwa katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi hilo baada ya kucheza mechi moja.

Breaking news: Kiungo wa Liverpool afanya vipimo, Kocha aponea chupuchupu

$
0
0

Selena William hatimaye amerudi tena kwenye French open. Selena amesema amefurahi kurudi tena lakini atajipima nguvu katika mpambano wake na Maria Sharapova. Sharapova hajawahi kumfunga Selena tokea 2014.

Swansea inatarajia kumteua Graham Potter kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo. Graham yupo katika mazungumzo ya mwisho kufanya makubaliano. Potter mwenye umri wa miaka wa 42 anatarajia kuchukua nafasi ya Carvalhal aliyetimuliwa

Manuel Pellegrin amewashukuru Polisi baada ya kumsaidia alipokuwa na mke wake walipovamiwa na majambazi. Mke wa Pelegrin bibie Carola alipoteza begi lake wakati wa vurumai hilo. Carola na Pellegrin walikuwa jijini Santiago wakielelekea kwenye mgahawa.

Mchezaji wa Zamani wa Arsenal Nicklas Bendtnar atalikosa kombe la dunia. Nicklas raia ya Denmark alipata majeraha ya mishipa nyonga baada ya kujiumiza mwenyewe kwa bahati mbaya. Nicklas alikosa mchezo wa timu yake ya taifa hivi mwishoni mwa wiki hii.

Vicent Kompany ameitwa kwenye timu ya taifa licha ya kuwa na majeraha hivyo atakwenda kombe la dunia.

Emre Can anatarajia kufanyiwa vipimo vya afya kwa klabj yake mpya ya Juventus

Breaking news: Fred atua Manchester kufanya vipimo

$
0
0

*Kona Ya Fuku-Fuku…*

MCHEZAJI kutoka Brazil anayekipiga katika klabu ya Shakthar Donestik Fred, ameonekana akiingia katika viwanja vya mazoezi vya klabu ya Manchester United kwaajili ya kukamilisha usajili wake.

Fred anatarajia kupima vipimo vya afya siku ya leo na kutambulishwa rasmi kuwa mchezaji halali wa klabu ya Man United.

Fred atajiunga na United kwa ada ya Euro 52 milioni.

~ Daniel S.Fute

Sababu za Leroy Sane kuachwa Ujerumani hizi hapa

$
0
0

Msimu mmoja haukutosha kumpatia Leroy Sane tiketi ya kwenda Russia? Umeona picha ya Kyle Walker aliyoweka kwenye ukurasa wake akizungumzia kuachwa kwa Sane? Hii hapa

Mwaka jana wakati Guardiola akiwaza namna ya kumtumia Jesus Navas, akili yake ilimwaminisha kwamba Navas hafai kwenye mipango yake. Mwisho wa siku ilibidi wacheze kamari ya Euro milioni 38 kwa ajili ya Leroy Sane.

Guardiola amefanikiwa kabisa kwa kamari yake ya msimu wa kwanza. Sane amefanya vyema sana msimu wa kwanza. Kwanza alichomfurahisha sana Pep ni uwezo wa Sane kuelewa kiingereza vizuri sana na kwa mapema. Sane ameonekana mara nyingi akiwasiliana na wenzake bila tabu yoyote na amekuwa na uwezo kukwepa majeraha na kila mara alipopata majeraha alirudi mapema.

Akiwa na miaka 22 amemaliza msimu wake wa kwanza kwa mabao 14 na kuasisti mabao 19 katika michezo 49.

Baadhi ya waandishi wa habari wamemfananisha Sane mara kadhaa na staa wa Man United Ryan Giggs kwa namna wanavyocheza. Mwaka wake wa kwanza amefanikiwa kunyakua tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa mwaka PFA.

Joachim Low bado anaamini mfumo wake haumhitaji Sane.

Sane mwezi Januari mwaka huu alitania kwamba kama watashinda kombe la Dunia atastaafu soka. Mambo sio Mambo mbali na kujiandaa vizuri hadi kwa kubadilisha aina yake ya nywele lakini bado kura zake hazikutosha.

Low anasemaje
“Sane Hajafika katika mechi za kimataifa bado, lakini nilipata wakati mgumu kugundua yupi bora kati ya Julian Brandt na Leroy Sane.

Kikosi cha Die Mannschaft wanajiandaa kuchukua ubingwa mara mbili mfululizo kama ilivyokuwa kwa Brazil mwaka 1962.

Low binafsi naona kama amefanya uamuzi mkubwa na mgumu sana. Mwanzo walio wengi walilaumu kuachwa kwa Mauro Icardi lakini hili la Sane binafsi ni kama lina uonevu mkubwa usio na mantiki.

Anasema kwamba Sane amelingana uwezo na Brandt naona kama ni matusi. Sane amehusika mabao 33 hakuna mchezaji yeyote wa Ujerumani mwenye takwimu hizi za Sane.

Michael Ballack mwenyewe anakiri kwamba Low amejiweka katika wakati mgumu na presha kubwa kwa kumuacha mchezaji aliyeng’ara msimu mzima.

Mwandishi nguli wa Mirror Bwana Alex Richard ametoa mawazo yake

Kwanza Ujerumani wana upungufu mkubwa wa wachezaji muhimu kwa baadhi ya nafasi hasa kwa kuangalia wachezaji wazoefu. Wanamkosa Emre Can, Shkrodan Mustafi na Mario Gotze, ambao wote walikuwepo kwenye kikosi cha ubingwa mwaka 2014.

Hili wala sipingani nae kabisa. Kwa ubunifu alio nao Sane sioni mchezaji mwenye flo nzuri ya mpira kama ya Sane labda Reus. Ozil anaweza kukaa na mpira lakini hana kasi kama ya Sane. Yaani leo hii kama Sane angekuwa muingereza kila kona kila faulo hata goli kiki waingereza wangemtaka apige hasa kwa ubunifu wake na uwezo wa mguu wake wa kushoto.

Hebu angalia tu, Hakuna Sandro Wagner, mwenye magoli matano kwenye mechi 8 za timu ya taifa na pia kiungo Serge Gnabry hatokuwepo kikosini.

Hilo benchi lina watu gani sasa?

Sane amekuwa na msimu mzuri sana na amecheza ligi ngumu na yenye ushindani. Mfumo wa Low ni 4-2-3-1. katika mfumo huu Thomas Muller atatokea upande wa kulia na Mesut Ozil atacheza namba 10 na sehemu iliyobakia ni ya kushoto ambako Sane anacheza. Katika sehemu ya kushoto imechukukiwa na Marco Reus ambaye alikosa kombe la dunia mwkaa 2014 na kumbe la Yuro 2016.

Ni mchezaji ambaye amekuwa akikumbwa sana na majeraha. Amecheza michezo 11 kati ya 13 ya Mwisho ya Borussia Dotmund tokea alipotoka Majeruhi mwezi desemba mwaka jana. Reus katika michezo hiyo 11 amefunga mabao 7. Sina shaka na ubora wa Rues. Anajua na ni mpiganaji

Kwa upande wangu nimewaza pia, Ujerumani itakosa mchezaji mwenye uwezo wa kukaa na mpira na kupunguza mabeki kadhaa katika benchi lake.

Sane alikuwa mchezaji mbadala pale Reus atakaposhindwa au ozil kuchoka. Sina imani sana kama kuna Kitu Brandt amemzidi Sane. Bila shaka Low anamalengo yake mengine.

Low anakiri Sane ni mzuri sana lakini anasema shida kubwa ameshindwa kufanya maamhzi sahihi kutokana na ushindani wa nafasi hiyo kuwa kubwa. Low ni kipenzi cha Julian Draxler kwanini hakuntema licha ya kwamba alipata wakati mgumu klabuni PSG?

Julian Draxler, ana miaka 24. amekuwa kwenye wakati mgumu sana tokea Neymar ajiunge na mabwenyenye wa PSG. Draxler amecheza michezo 40 msimu kwa klabu ya PSG licha ya ufinyu mkubwa wa namba.

Draxler alikuwa nahodha kwenye michuano ya Confederation ambapo timu ilibeba kombe hilo nae kuibuka na kiatu cha dhahabu.Sina tatizo na Draxler lakini kwenye suala la ufanisi wake msimu sio bora sana kumzidi Sane

Mpinzani mkubwa wa Sane kijana Brandt amefunga magoli 12 na kutoa asisti 7 katika michezo 39 kwa klabu yake ya Bayer Leverkusen. Brandt sio kwamba amekuwa na uzoefu mkubwa wa mechi za kimataifa tokea 2016, ila faida yake anajituma sana kukaba na ana uwezo wa kubadilisha nafasi moja hadi nyingine.

Sane amekuwa na mambo mengi mno nadhani hili linaweza kuwa sababu kubwa. Katika michuano ya confederation alijittoa kwenge kikosi ili kwenda kufanya uchunguzi wa pua tatizo ambalo ilionekana kuwa dogo na angeweza kujitoa tu kwa taifa lake.

Katika michezo 12 ametengeza bao moja peke na hajafunga bao lolote kwa taifa lake. Low anaweza kujificha kwenye sababu hii pia. Amekuwa mzuri kwenye mifumo ya Guardiola kwa kuwa ana muda mwingi wa kukaa nae mazoezini na kumwelekeza kitu cha kufanya. Naona kama Low hana muda kusumbuka kumweka mchezo mpya kwenye mfumo wake kwa kulazimisha au kwa kuriski.

Tuseme tu kwamba mwalimu mwenyewe ndiye aliyeshindwa kumtumia Sane. Ni kazi ya mwalimu kuhakikisha mchezaji bora anaingia kwenye mfumo wake

Kikosi chao

Walinda lango: Manuel Neuer (Bayern Munich), Marc-Andre Ter Stegen (Barcelona/ESP), Kevin Trapp (Paris Saint-Germain/FRA)

Walinzi: Marvin Plattenhardt (Hertha Berlin), Jonas Hector (Cologne), Matthias Ginter (Moenchengladbach), Mats Hummels (Bayern Munich), Niklas Suele (Bayern Munich), Antonio Rudiger (Chelsea/ENG), Jerome Boateng (Bayern Munich), Joshua Kimmich (Bayern Munich)

Viungo: Sami Khedira (Juventus/ITA), Julian Draxler (Paris Saint-Germain/FRA), Toni Kroos (Real Madrid/ESP), Mesut Ozil (Arsenal/ENG), Thomas Mueller (Bayern Munich), Sebastian Rudy (Bayern Munich), Julian Brandt (Bayer Leverkusen), Ilkay Gundogan (Manchester City/ENG), Leon Goretzka (Schalke 04), Marco Reus (Borussia Dortmund)

Washambuliaji: Timo Werner (RB Leipzig), Mario Gomez (VfB Stuttgart)

Makala hii imeandaliwa na Privaldinho unaweza kunifollow Instagram

Morocco yatoa tahadhari kombe la dunia

$
0
0

Morocco wao wanagawa dozi tu. Morocco ni mwendo wa kutesti mitambo tu, magoli ya Belhanda na El Kaabi yamefanya bao la Gregus kuwa kazi bure.

Morocco 2-1 Slovakia: report

Morocco walicheza soka safi na kutawala kila engo katika dimba Stade de Genève

Morocco chini ya kocha mwenye mafanikio makubwa hapa barani Afrika Harvé Renard walihakikisha wanafanya msako wa nyumba kwa nyumba chini ya nyota wa klabu ya Leganés Nordin Amrabat

Hata Hivyo Morocco walikosa nafasi nyingi sanaa.

Gregus alitandika mkwaju mmoja matata na kumuacha mlinda mlango wa Girona Bono akiruka ovyo bila mafanikio. Baada ya bakora ile Vijana wa kiarabu hawa wa morocco waliokuwa kwenye saumu wakaamsha popo.

Belhanda alifunga kwa kichwa wa mpira wa kona baada ya mabeki wa Slovakia kuruka kizembe.

Kijana machachari El Kaabi akatokea benchi na kufanya mambo kuwa 2 -1.

Morocco watacheza mchezo mmoja hapo baadae dhidi ya estonia kabla ya kwenda kucheza kombe la dunia.

Hapo awali walitawala kila sekunde kwenye mchezo uliotoka bila kwa bila na timu ya taifa ya Switzerland.

kwa kiwango wanachoonesha hizi ni salamu tosha kule Urusi.

Viewing all 9000 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>