Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all 9000 articles
Browse latest View live

Taarifa za hivi punde za usajili n.k

$
0
0

Beki wa klabu ya Ac Milan, Leonard Bonucci, amewasili jijini Turin, kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na kujiunga na klabu ya Juventus.

Kocha wa klabu ya Leicester City, Claude Puel, amesema kuwa atawakosa nyota wake wawili kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu England, dhidi ya Manchester United.

Puel,amesema kuwa atamkosa beki wake Harry Maguire, na mshambuliaji wake Jamie Vardy, ambaye bado wapo likizo walikuwemo katika kikosi cha timu ya taifa England, kilichoshiriki michuano ya fainali za kombe la dunia nchini Urusi.

“Puel, tumebakiwa na siku tano kutoka sasa kujiandaa na mchezo wetu wa ufunguzi dhidi ya Manchester United, lakini wachezaji hao wataukosa mchezo huo,”maneno ya kocha wa Leicester City.

Klabu ya Bayern Munich, imekamilisha usajili wa mchezaji wa klabu ya Schalk 04 Leon Goretzka.

Chama cha soka cha FA cha nchini England, kimethibitisha Kuwa kocha wa timu ya taifa England, Gareth Southgate, ataiongoza taifa hilo tena katika fainali za kombe la dunia za Mwaka 2022 nchini Qatar.

Mara ya mwisho taifa hilo kufika hatua ya nusu fainali ilikuwa mwaka 1990 katika fainali za kombe la dunia.


Viongozi waridhishwa na kiwango cha Yanga

$
0
0

Uongozi wa Yanga umesema unaendelea kuridhishwa na kiwango kinachooneshwa na timu yao ambayo inaendelea na mazoezi mara baada ya mechi yao ya kimataifa dhidi ya Gor Mahia.

Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo Omar Kaya amesema kiwango cha Yanga ilipocheza na kupoteza 4-0 dhidi ya Gor Mahia ni tofauti na ilivyopoteza 3-2 kwenye mechi ya marudiano. Kuna maendeleo kwenye kikosi.

“Baada ya mchezo wa Gor Mahia wachezaji walipatamapumziko ya siku moja sasa hivi wanaendelea na mazoezi kwenye viwanja vya polisi kwa ajili ya mechi nyingine ya kombe la shirikisho na msimu ujao wa ligi.”

“Wanaendelea vizuri na bado tupo kwenye program zingine kwa ajili ya kuboresha kambi ili tuwe nanyimu yenye ufanisi na ubora.”

“Kuna mabadiliko yapo ukiangalia mechi tuliyocheza Nairobi na ambayo tumecheza Dar utaona kuna mabadiliko kwenye timu na inatoa picha kwamba tuongeze ufanisi na muda wa kuwa pamoja ili mwalimu awe na wepesi wa kuwapa anachotaka.”

Mashabiki Zanzibar wanataka kujua tatizo Yanga

$
0
0

Baada ya Yanga kuendelea kufanya vibaya kwenye mashindano ya kombe la shirikisho Afrika, mashabiki wa timu hiyo visiwani Zanzibar wamekutana kutaka kujua mbali na hali mbaya kiuchumi kunatatizo gani jingine?

Katibu wa matawi ya Yanga Zanzibar Hatibu Kofi ameeleza lengo la kikao chao.

“Tulikuwa na kikao kidogo tukijaribu kuzungumzia masuala ya timu yetu ya Yanga hususan mambo ya usajili na mambo yanavyokwenda kwenye uendeshaji wa timu.”

“Kipindi hiki tunachopitia ni kigumu, ni kipindi ambacho hatujakizoea sana sasa kauli za viongozi wetu wakati mwingine huwa hazitupi matumaini kwa sababu kila mmoja ana lake huyu anasema hili yule anasema lile.”

“Tumekuja kujadili kauli za viongozi halafu tuje na msimamo mmoja kama wanayanga Zanzibar tunafanya nini? Halafu tutawasiliana na viongozi.”

“Kiwango cha timu yetu sasa hivi sio kizuri, tumecheza Kenya na Gor Mahia tumefungwa 4-0 tumerudi nyumbani tumefungwa 3-2. Ni matokeo mabaya sana kutokea katika misimu 10 ya hivi karibuni, ni vitu ambavyo wazanzibar hasa wanayanga vinatuumiza.”

“Viongozi wetu watuambie tatizo letu ni nini? Tunajua hatuna pesa lakini kwa hawa wachezaji waliosajiliwa wanatunzwaje, wanapataje stahiki zao ndio mambo ambayo tumejadiliana na kuona tunafanyaje.”

Hee! Kumbe Fei Toto na Obi Mikel wana wenzao wengi Ulaya

$
0
0

Feisal Salum aka Fei Toto, kama ni man of the match wakati wa dirisha la usajili baaso Fei Toto angebeba kiatu hicho, Toto kutoka JKU alizua kizungumkuti katika usajili akizihusisha Yanga na Singida United.

Fei Toto bwana asubuhi alitangazwa amejiunga na Singida United ya mjini Singida na picha kabisa zikaoneshwa lakini jioni akatangazwa Jangwani nao na picha zao, lakini kama unadhani hiyo ni Bongo tu baasi utakuwa umekwama.

John Obi Mikel. United hawaji kusahau hili suala mwaka 2005, achana na hizi photoshop za mashabiki wa United wanafanya katika suala la usajili, Obi yeye alipiga picha akiwa United lakini kesho yake akahamia Chelsea, timu hizi zilivutana sana lakini baadaye akaja kumilikiwa na Chelsea.

Sol Campell. Hii ilikuwa mwaka 2009 ambapo klabu ya soka nchini Uingereza ya Notts Country walikubaliana kumnunua Campell lakini baada ya siku zisizozidi saba beki huyo wa kimataifa wa Uingereza alitimkia Porsmouth.

Stephan Guivarch. Alitokea Ligue 1 huyu akikipiga Auxerre kwa £3.4m akajiunga na Newcastle United, na Newcastle walimnasa baada ya kuwa kati ya nyota walioibeba Ufaransa hadi wakabeba kombe la dunia 1998. Akiwa Newcastle alicheza mechi 4 tu na kocha Ruud Gullit wakati anaondoka kwenda Rangers na yeye akaondoka.

Dietmar Hamann. Alikuwepo wakati Liverpool wanaipiga Ac Milan mwaka 2005 kwenye Champions League, hii ikawashawishi Bolton kutoa pesa kumnunua lakini siku chache baada ya kumpata akahamia Manchester City ambapo baadae City waliilipa Bolton.

Robert Jarni. Baada ya michuano ya kombe la dunia mwaka 1998 nyota huyu wa Croatia alisainiwa na Coventry akitokea Betis, lakini akiwa na Coventry hakucheza mechi hata moja na baadae akahamia Real Madrid kwa ada ya £1m huku akisema hilo lilikuwa shinikizo la familia.

Mkongwe Chuji anarudi VPL “ukijua tuliza mpira na kutoa pasi inatosha”

$
0
0

Star wa zamani wa vilabu vya Simba nanYanga Athumani Idd ‘Chuji’ msimu wa 2018/19 tutamuona tena ligi kuu Tanzania bara akiwa na timu ya ‘wagosi wa kaya’ Coastal Union kutoka Tanga.

Coastal Union tayari imeingia kambini kujiandaa na ligi kuu, miongoni mwa wachezaji waliowahi kuingia kambini ni mkongwe Chuji ambapo kambi ya timu hiyo ipo maeneo ya Kange nje kidogo ya jiji la Tanga.

Chuji amezungumzia mambo mbalimbali kuelekea msimu mpya wa ligi kuu.

Usajili wa Coastal Union

Kwa wachezaji waliosajiliwa tukikaa na kushirikiana tutafanya kazi vizuri.

Msimu wa 2018/19 kutakuwa na timu 20 ambapo kila timu itacheza mechi 38, Chuji ni mzoefu wa ligi anaona msimu utakuaje?

“Ligi ya timu 20 itakuwa na changamoto nyingi, lazima wachezaji tuwe fit, tukiwa fit tutaweza kufanikisha malengo ya timu. Mechi 38 si mhezo kama hatutakuwa fit ligi itakuwa ndefu.”

Coastal Union imechanganya wachezaji wazoefu na vijana, Chuji anaamini timu itafanya vizuri.

“Kwa mchanganyiko uliopo kwenye timu tutapambama kuhakikisha tunatetea kinachowezekana ndani ya Coastal. Hatutaki kushuka kama maandalizi yetu tutakuwa na maandalizi mazuri tutamaliza kwenyenafasi nzuri.”

Muda mrefu hajaonekana ligi kuu, wadau wa soka wamtarajie Chuji yupi?

“Kwa Tanzania wamtegemee Chuji yuleyule, waangalie kutakuwa na mabadiliko gani yatakuwa yamekuja. Wanasema, ukijua kutuliza mpira na kutoa pasi inatosha, mengine yanakuja tu. Kujengwa kisaikolojia tunaingiaje kwenye ligi kwa sababu msimu uliopita tulicheza ligi daraja la kwanza.”

“Tunaingia msimu wa ligi kuu, mimi naijua ligi kuu inamaana ushindani utakuwepo, lazima tuoneshe ushindani kwa vijana.”

Watu wanamsema sana Chuji

“Mambo ya kusemwa yameanza tangu miaka hiyo, bora uangalie yako usisikilize ya mtu. Kama kusemwa ingekuwa unatoboka, mimi mwili mzima ungekua na matobo.”

Ana kiwango cha kurudi tena Taifa Stars?

Sijui, lakini kwanza ngoja nitetee timu yangu.”

Rostand safari imeiva Yanga

$
0
0

Hatma ya Youthe Rostand itajulikana wakati wowote kuanzia sasa ndani ya Yanga. Inaelezwa uongozi wa timu hiyo upo katika mipango ya kumpiga chini kuelekea msimu ujao wa 2018/19.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili Yanga Hussein Nyika amesema kamati ya usajili inajadili mustakabali wake huku Youthe akiwa hajasafiri na timu kwenda Morogoro kwenye kambi ya maandalizi.

“Kamati ya usajili tuna kikao kwa ajili ya kuangalia mustakabali wa golikipa huyo na bahati nzuri hakuwa sehemu ya kikosi kilichoenda Morogoro. Siwezi kulitolea taarifa sasa hivi mpaka tutakapokutana na kamati nzima tutatoa maamuzi wanahabari watafahamishwa pamoja na umma wa wanayanga.”

“Tutakapokua tumefanya maamuzi tutatangaza kama ataendelea kuwa mchezaji wa Yanga au ataenda sehemu kwa mkopo kwa sababu sehemu nyingine madirisha bado yapo wazi ndio maana hakuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji waliokwenda Morogoro.”

“Tumeshaanza maongezi na mchezaji mwenyewe tumemsikiliza mawazo na ushauri wake  tutakaa kama jopo na sisi kutoa maamuzi kama viongozi itakapofikia mwafaka watu watajua.”

“Ukiwa kama mwanahabari za michezo umeshaona tumefanya usajili wa golikipa mwingine toka Congo DR, hiyo tu inalnesha kuna kitu kwa sababu huwezi kuwa na magolikipa wawili wakigeni mbaya zaidi huwezi kuwa na magolikipa wanne kwenye timu.”

“Hivyo vitu vyote lazima mwelekeo, kama viongozi wa Yanga na technical bench ni nini walichoamua kukifanya atolewe kwa mkopo au  kuvunja mkataba, hivyo ni vitu vinavyojulikana.”

“Kiwango chake sio kama tulivyomchukua mwanzo, kimezidj kushuka kila siku kwa hiyo ndio maana benchi la ufundi likashauri atafutwe golikipa mwingine.”

Yanga yaingia chimbo Morogoro

$
0
0

Yanga imesafiri kwenda Morogoro kuweka kambi ya maandalizi kwa ajili ya mechi zake mbili zilizobaki za kimataifa pamoja na maandalizi ya ligi kuu Tanzania bara.

Mwenyekiti wa usajili na mashindano Yanga Hussein Nyika amethibitisha timu imefika salama Morogoro.

“Vijana wamefika salama Morogoro kesho wataanza program zao kama mwalimu alivyopanga kwa ajili ya kambi.”

“Kambi hiyo ni kwa ajili ya vitu viwili, mashindano ya kimataifa (mechi mbili zilizosalia za kukamilisha ratiba) na maandalizi ya ligi kuu inayotarajia kuanza August 22, 2018.”

“Lazima mwalimu apate muda wa kutosha kukaa na wachezaji wote waliosajiliwa na wazamani kutengeneza kikosi kitakachopambana kwenye ligi kuu.”

Bakayoko amechana mkeka

$
0
0

Jorginho amejiunga na klabu ya Chelsea. Mashabiki wa Chelsea wameshaanza kumpaka rangi. Wanadai hapotezi pasi hata moja. Sawa sisi yetu macho. Sitaki kusema lolote juu yake nisije nikaonekana mwanga.Lakini nyuma ya daraja inaonekana kuna nguzo imeng’olewa. Inaonekana kuondoka kwa Matic ni sawa na kuondolewa kwa nguzo hiyo. Ingekuwa ni mti tungesema Man United kumchukua Matic waling’oa mti na mizizi yake yote hawajakata shina.Wachezaji wanne wamekwisha nunuliwa ili kuziba shimo aliloacha Matic. Amekuja Rose Barkley, akaja Drinkwater Danny, kabla ya hapo alisajiliwa Tiemoe Bakayoko na hivi sasa Jorginho amejiunga nao. Wote hawa ni kwa lengo ya kutafuta kiungo atakayemsaidia N’golo Kante kwenye dimba la katikati.Bakayoko wakati anatokea Monaco alinunuliwa kwa Euro milion 40. Chelsea walicheza kamari sawa na ile waliocheza Man united kumnasa kinda Anthony Martial kwa dau la Euro 50 lengo ikiwa ni kufanya usajili wa bahati nasibu. Ni bahati nasibu ndio kwa sababu hata kama soko limekua lazima tukubaliane milioni 40 kwa mchezaji ambaye hajacheza mechi 60 ni kurusha jiwe gizani.Kwa united kamari yao tunaweza kusema ilitiki hajachana sana mkeka wao. Inawezekana msimu wa kwanza Martial alirudisha fadhila kwa kufunga mabao 17 na kuwa kinara wa timu. Msimu huu uliopita licha ya kukumbana na matatizo na kocha lakini yeye ndiye mfungaji bora nyuma ya Lukaku kwenye kikosi cha United.Bakayoko amechana mkeka kwa mtazamo wangu mimi. Narudia tena kwa mtazamo wangu mimi. Namuona ameshindwa kuonesha kwamba ufanisi wake ni katika sehemu gan haswa ya uwanja. Antonio Conte amejaribu kulazimisha kumweka Bakayoko kwenye nafasi tofauti tofauti ilimradi tu apate majira ya saa hivi mbovu. Kuna watu wanadai kuwa Bakayoko kuna baadhi ya mechi alicheza vyema. Sawa kubaliana na mimi kuna wakati saa mbovu inakwenda sawa kisha inaoteza tena majira.Lakini Bakayoko amekuja Chelsea kipindi ambacho kwake ni neema. Amecheza takribani mechi 29 akiwa na umri wa miaka 23. Tena kwa kiwango kibovu kile kile. Bila shaka kwake ni neema. Ndio ni neema kwa sababu hajakumbana na ushindani mkubwa.Mwenzie Matic alikuja Chelsea kipindi ambacho hata benchi hakuwa na nafasi. Tena mbaya zaidi alikuja kipindi anatumika kama kiungo mchezeshaji nafasi ambayo Bakayoko anatumika kwa sasa. Miaka ile nafasi hiyo alikuwepo Deco, alikuwepo Yuri, alikuwepo Malouda ambaye ilibidi asukumwe pembeni ilimradi majani yaenee bandani, pia alikuwepo kiungo namba 8 bora kwa wakati wake Frank Lampard achilia mbali akina Kalou. Huyu Matic angecheza wapi? Sasa hivi Bakayoko amekuja kipindi amabcho wapinzani wake ni akina Loftus Cheek huku benchi la Chelsea likiwa na watu kama Kenedy kabla ya kuletwa Drinkwater ambaye nae alifeli.Huyu Bakayoko angekuja kipindi kile hata nafasi ya kiungo mkabaji asingepata hiyo nafasi. Alikuwepo Obi Mikel, alikuwepo Essien na mbaya zaidi alikuwepo kiungo bora wa Ujerumani Michael Ballack. Hata yeye benchi angekaa nani atoke?Bakayoko ametumia mali za marehemu vibaya na mzimu wake utamnyonya damu. Ila kuna wakati nailaumu klabu ya Chelsea kwa kutoa fedha nyingi kwa mchezaji ambaye katika michezo 38 ya Monaco amecheza mechi 20 tu dakika 90 huku akiwa na miaka 21. Binafsi ni kama walibugia pombe za kupewa.Chelsea ya kipindi kile ulikuwa huwezi kupata namba kama huna namba kwenye kikosi cha timu yako ya taifa. Acha Jorginho atuoneshe kama ana hekima ya kuitunza karatasi ya mirathi.Privaldinho (instagram)


Bayern yamkataa Martial, Kessy apata ulaji nje ya nchi

$
0
0

Mwenyekiti wa klabu ya Bayern Munich, Karl -Heinz Rummenigge, amesema kuwa mchezaji wa klabu ya Manchester United, Anthony Martial, hayupo kwenye mipango ya kumsajili.

Martial, ambaye amekuwa hakiushwa kuondoka katika klabu ya Manchester United, na amehusishwa kujiunga na klabu za Chelsea, na Paris Saint Germain, huku mwenyekiti wa klabu ya Bayern Munich, amesisitiza kuwa hawana mpango na mchezaji huyo.

Siku kama ya leo mwaka 2017 mshambuliaji wa wa zamani wa klabu ya Barcelona, Neymar, alijiunga na klabu ya Paris Saint Germain, kwa kitita cha paundi million 198 na kuwa mchezaji ghali zaidi duniani.

Beki wa zamani wa klabu ya Yanga, Hassan Kessy, aliyemaliza mkataba na klabu ya Yanga, leo hi ametambulishwa rasmini na klabu yake ya Nkana Fc, ya Zambia inayoshiriki ligi kuu.

Mnamo Agosti 3, 2016: klabu ya Manchester City ilikamlisha dili la £27m kumnasa Gabriel Jesus kutoka Palmeiras. Gabriel Jesus atakuwepo City hadi 2023!:

Gabriel Jesus amecheza michezo 27 kwa Manchester City na hajwahi kuanza mchezo wowote na klabu yake ya City kupoteza(W23 D4), amehusika mabao 24 (18 mabao, na kuasisti mara 6). .

Martial arejea, Arsenal na Chelsea zapata saini nyingine.

$
0
0

Mchezaji wa Manchester United. Martial amerejea rasmi katika mazoezi na kujumuika na Manchester United, kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya ligi kuanza baada ya kuchelewa kurudi alipoenda kumuona mke wake alipojifungua.

Martial amekumbana na faini kutoka kwenye uongozi wa United. Je atasalia katika kikosi?! Ni swala la muda, tusubiri tuone.

Winga wa klabu ya Arsenal Alex Iweobi, amesaini mkataba mpya na klabu ya Arsenal. Iweobi, ambaye alijiunga na klabu ya Arsenal, akitokea academy ya Hale, mwaka 2015 pia ameichezea Arsenal, michezo 98 na kufunga mabao nane.

Mchezaji wa chelsea Pedro ameongeza mkataba mpya na klabu yake ya Chelsea.

Pedro amesaini kandarasi itakayomuweka klabuni hapo hadi mwaka 2020.

Kwa heri Youthe Rostand

$
0
0

Uongozi wa Yanga umetangaza kiachana na golikipa Youthe Rostand raia wa Cameroon baada ya pande mbili kukubaliana kuvunja mkataba.

Ofisa habari wa Yanga Dismas Ten amesema Rostand klabu hiyo ilikuwa tayari kumtoa kwa mkopo kwenda African Lyon lakini golikipa huyo hakuwa tayari.

“Golikipa Rostand hayupo Morogoro kwa sababbu tayari makubaliano ya pande mbili (mchezaji na klabu) yamefikiwajuu ya kusitisha mkataba wake.”

“Klabu ilikuwa na mpango wa kumpeleka kwa mkopo African Lyon lakini yeye mwenyewe kwa sababu zake za kiafya alisema hayuko vizuri sana ‘ki-saikolojia’ kwa hiyo anahisi hawezi kuitumikia Yanga kwa 100% akaomba klabu ifanye makubaliano ya kusitisha mkataba.

“Jambo hilo limekubaliwa, kinachosubiriwa sasa ni yeye kupatiwa stahiki zake ili aende akapumzike na kufanya taratibu nyingine za maisha akiwa nyumbani kwao.”

“Rostand atalipwa stahiki zake, pesa ya usajili iliyobaki na mishahara ambayo alikuwa hajapata katika kipindi cha hivi karibuni, ndio makubaliano yaliyofikiwa na baada ya hapo ataondoka kwenda kuanza maisha mengine.”

Baada ya kusaini Juventus, Ronaldo aibuka tena Sampdoria

$
0
0

Cristiano Ronaldo, Cristiano Ronaldo ndio jina ambalo sasa kila mtu analizungumzia na kila mtu anasubiri kuona namna ambavyo nyota huyo atafanya makubwa katika ligi ya Serie A.

Tangu ajiunge na Juventus kumekuwa na mengi yanaendelea katika soka kuhusu yeye, yapo ya kuchekesha na yapo ya kustaajabisha ili mradi tu anayeongelewa ni Cristiano Ronaldo.

Sasa sikia hii, klabu ya soka ya Sampdoria leo iliushangaza ulimwengu baada ya wao nao kufanya kama kile walichofanya Juventus kumsajili Ronaldo wao kwa njia ile ile waliyofanya Juventus.

Lakini Ronaldo wa Samdoria sio Ronaldo aliyetokea Real Madrid bali huyu anatokea Leeds ya nchini Uingereza na yeye haitwi Cristiano Ronaldo balo anaitwa Ronaldo Vieira.

Vieira ni raia wa Uingereza na amekuwa gumzo sana kwani majina yake yote mawili yemetoka kwa nyota wakubwa wa soka, Ronaldo linamuwakilisha Ronaldo wa Brazil na huyu wa Ureno na pia ana jina la mwisho la nyota wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira.

Wakati Ronaldo wa Juventus amenunuliwa kwa £100m huyu wa Sampdoria amenunuliwa kwa £7.7m tu ikiwa ni pungufu ya karibu £93m kutoka kiasi cha Cr7.

Kwa mara ya kwanza Ronaldo hawa wawili watakutana tarehe 29/12 katika mchezo wa Serie A kati ya Juvetus Vs Sampdoria kabla ya kurudiana tarehe 26/05 hapo mwakani.

Utake usitake lakini Cr7 anatuhamishia Serie A

$
0
0

Bado wiki mbili tu ligi kuu nchini Italia kuanza lakini habari zote kwa sasa zimehamia Italia baada ya Cristiano Ronaldo kusaini Juventus, kuna mengi yanasemwa kuhusu Cr7 na leo tuone baadhi yaliyotawala vichwa vya habari kuhusu Cr7.

Cr7 amewaaunfollow Real Madrid Insta. Katika hali ambayo si ya kawaida na imezua maswali mengi kwa wapenzi wa soka, ni kitendo cha Real Madrid kutoonekana katika orodha ya watu Ronaldo aliowafollow.

Wengi wanashindwa kuelewa sababu ya Ronaldo kufanya hivi, japo hii imekuwa kawaida kwake kwani kila klabu anayoondoka huwa anaiunfollow kwenye mitandao ya kijamii.

Awaburuza wenzake katika mshahara. Cristiano Ronaldo ndiye nyota ambaye anapokea mshahara mkubwa zaidi Serie A na kama hujui ni kwamba anayemfuatia Ronaldo hata uzidishe mshahara wake mara tatu bado hamkuti Cr7.

Anapokea £30m akiwa na Juventus, huku anayemfuatia ni Gonzalo Higuain ambaye anachukua £8m, Paulo Dyabala yuko nafasi ya tatu akiwa anapokea £7m na kisha anafuatia mlinda lango wa Ac Milan Donnaruma anayepokea £6m.

Amfanya raisi wa As Roma amtamani Messi. Raisi wa As Roma James Pallota amekiri kwamba Serie A panaweza pasiwe rahisi sana kwa Ronaldo hata kama ni mchezaji mkubwa na anaona atahangaika kuzoea.

Lakini pia raisi huyo wa As Roma ameongea utani ambao mashabiki wa Roma wanatamani iwe kweli baada ya kusema kwamba wao kama Roma wameanza maongezi na Lionel Messi ili kuja kuwa mpinzani wa Cr7 Serie A kama walivyokuwa La Liga

Ni wachezaji hawa wawili tu waliobarikiwa kucheza pamoja na Ronaldo na Messi

$
0
0

Kuna masuala katika soka ni bahati sana hembu fikiria mfano umecheza na Maradona katika klabu moja, na baadae ukahamia klabu nyingine ukamkuta Pele naye yupo.

Sasa kwa kisasa ni imagine unacheza na Messi timu moja na baadae unahamia kwingine unamkuta Cr7 hii ndio wanaita bahati ya mtende, ni wachezaji wawili tu ambao wamewahi kucheza na nyota hawa wawili katika klabu.

Gerrard Pique. Pique kati ya nyota ambao hawaipendi kabisa Real Madrid lakini aliwahi kucheza pamoja na Cristiano Ronaldo katika klabu moja.

Mwaka 2004-2008 alikuwa akijaribu kutafuta nafasi United ambako pia alikuwa na Cristiano Ronaldo baadae aliuzwa kwa £5.5m kwenda Barca ambako alikutana na Lionel Messi.

Henrik Larsson. Raia huyu wa Sweden alijiunga na Manchester United kwa mkopo mwaka 2007, kama unakumbuka huu ndio msimu ambao Cristiano Ronaldo alipasia nyavu mara 42 katika msimu mmoja.

Lakini kabla ya hapo usisahau kwamba Larsson alikuwepo katika kikosi cha Barcelona ambacho kilibeba michuano ya Champions League 2005/2006 wakati huo Messi ndio anaanza anza Barcelona.

Ukiacha nyota hao wawili kuna nyota ambao wao timu za taifa ndio zimewafanya wacheze na Messi na Cr7 huku mtu wa karibuni mwenye bahati hiyo akiwa ni Paulo Dyabala.

Dyabala wakati wa kombe la dunia alikuwa na Messi lakini upepo umebadilika ameletewa Cristiano Ronaldo na sasa wawili hao watakuwa pamoja katika klabu ya Juventus.

Carlos Tevez naye alicheza na Cr7 akiwa United akacheza na Messi akiwa Argetina, Higuain alicheza na Messi akiwa timu ya taifa ya Argentina huku akicheza na Cristiano akiwa Real Madrid.

Angel Di Maria naye ni kama Gonzalo Higuain, huku Nelson Semedo, Deco na Andre Gomes wenyewe walikutana na Lionel Messi Barcelona na waliporudi timu ya taifa wakacheza na Ronaldo.

Ozil apokonywa jezi, Vidal kutua Barcelona

$
0
0

Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Alvaro Morata, ameamua kubadilisha namba 9 na akuvaa jezi namba 29 msimu ujao. Morata, ameamua kuchukua maamuzi hayo baada ya mkeo wake Alice, alijifungua mapacha mawili siku ya tarehe 29 julai, mwaka huu watoto hao wa Morata, moja anaitwa Alesandro, na mwengine anaitwa Leonardo. Amewashukuru mashabiki wa Chelsea, kwa kumpa sapoti kubwa.

Inasemakana Vidal Arturo tayari ameshamalizana na klabu ya Barcelona na jumatatu atatambulishwa rasmi pale Camp Nou
Vilabu vya Vidal
– Colo-Colo ✅
– Bayer Leverkusen ✅
– Juventus ✅
– Bayern Munich ✅
– Barcelona

Kwa wale wazururaji wa mitandaoni hatimaye Ronaldo amewafolo baadhi ya wachezaji wa Juventus, kupitia ukurasa wake wa Instagram, kama Chiellin, Brazlgi, na Dybala. Lakini cha kusikitisha amewaunfollow Real Madrid…. Daaah…

Klabu ya Burnley, imefikia makubaliano na klabu ya Manchester City, kumnunua goli kipa Joe Hart, kwa kitita cha paundi million 4. Hart, anatarajiwa kufanyiwa vipimo na kukamilisha usajili huo.

Gerarrd Stevens Vs Frankie Lampard
Wote hawa vilabu vyao vitakuwa ugani leo na kesho.

Derby vs. Reading
Aberdeen vs. Rangers

Kiungo wa mpya wa klabu ya Arsenal, Lucas Torreira, aliyesajiliwa na klabu ya Arsenal ,akitokea Sampodoria, kwa kitita cha paundi million 25 anapewa jezi namba 11 hapo awali ilikuwa inavaliwa na Mesut Ozil. Ozil amepewa jezi namba 10 iliyokuwa inavaliwa na Willshere.

Henry alisajiliwa Arsenal tarehe kama ya leo. Alitokea Juventus.


Arsenal yapata pigo, Barcelona yamnasa Vidal (Done deal)

$
0
0

Zikiwa zimebaki siku 7 ligi kuu ya England, kutimbua vumbi ligi kuu ya England, ndo ligi ambayo imeongeza kutumia pesa za usajili mpaka sasa imetumia kiasi cha Euro billion 1 huku klabu ya Liverpool, ndo ikiongoza kutumia pesa nyingi katika usajili.

Liverpool, wametumia kiasi cha paundi million 195 kwenye usajili huku wakiweka rekodi ya kumchukua goli kipa wa klabu ya As Roma, Allison Becker, kwa kitita cha paundi million 75 na wamemsajili kiungo kutoka klabu ya Leizpg, Naby Keita, kwa kitita cha paundi million 60 huwo ndo ukiwa usajili ghali zaidi wa Liverpool.

Nafasi ya pili inashilikiwa na ligi kuu ya Itali, wametumia kiasi cha Euro million 927 kufanya usajili huku mchezaji ghali akiwa Cristiano Ronaldo, akitokea klabu ya Real Madrid, kwa uhamisho wa paundi million 100.

Nafasi ya tatu inashikiliwa na Ligi kuu ya Hispania, imetumia kiasi cha Euro million 643. Nafasi ya nne ikishika ligi kuu ya Ujerumani, ikiwa imetumia pesa kiasi cha Euro million 415.

Nafasi ya tano ikishika ligi kuu ya Ufaransa, ikiwa imetumia kiasi cha Euro million 376.

Kocha wa klabu ya Manchester City, amesema kuwa anahitaji kusajili mchezaji moja kabla ya dirisha la usajili halijafungwa. Guardiola, ambaye hivi karibuni alikuwa akimuhitaji kiungo wa klabu ya Napoli, Jorginho, ambaye amesajiliwa na klabu ya Chelsea, hivi karibuni. Guardiola, amesema kuwa anahitaji kiungo moja mwengine katika eneo la kiungo.

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Africa Lyon, Mbeya city, Tiko Okello,amerejea nyumbani Uganda, na kusaini mkataba na klabu ya Vipers Fc, akitokea klabu ya Benefica, De Macau.

Kiungo wa klabu ya Bayern Munich, Arturo Vidal, amefikia makubaliano na klabu ya Barcelona, na atafanyiwa vipimo na kusaini mkataba wa miaka mitatu utakaomfanya abaki klabuni hapo mpaka mwaka 2021.

Arturo, atukuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na klabu ya Barcelona, tayari wameshawasajili Arthur, Malcom, Lenglet.

Mchezaji wa Zamani wa West ham, Lionel Scalion ameteuliwa kuwa kocha wa muda wa timu ya taifa ya Argentina, baada ya aliyekuwa kocha wa Argentina Jorge Sampaoli kuondoka.

Beki wa klabu ya Arsenal, Sead Kolasnic, anatarajiwa kuwa nje ya uwanjani kwa muda usiopungua wiki 8 mpaka 10 baada ya kupata majeraha ya goti katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Chelsea. Kolasnic, alitolewa nje dakika ya 70 baada ya kupata maumivu ya goti .

Taarifa zote na Aziz Mtambo

Lampard azidi kutisha klabu yake ya Derby Country imeitwanga Reeding

Taarifa kuhusu Neymar, BVB yateua nahodha mpya, Ribery anena kuhusu Vidal

$
0
0

Winga wa klabu ya Borrusia Dortmund, Marcos Reus, amechaguliwa kuwa nahodha mpya katika kikosi hicho.

Klabu ya Barcelona, imefikia makubaliano na klabu ya Sevilla, kumuuza beki wao wa pembeni Alex Vidal, Barcelona, wapo tayari kumuuza kwa ada ya uhamisho wa paundi million 10. Vidal, alijiunga na Barcelona mwaka 2015 akitokea klabu ya Sevilla, amechezea Barcelona, michezo 51 katika miaka mitatu aliyedumu na klabu hiyo.

Klabu ya Paris Saint, ipo tayari kumsajili beki wa klabu ya Manchester United, Marcos Rojo, kwa ada ya uhamisho wa paundi million 20. PSG, atakutana na upinzani mkubwa kutoka klabu Everton, Zenit Petersburg, ambazo zinamuwania beki huyu raia wa Argentina.

Mshambuliaji wa klabu ya Paris Saint Germain, Neymar, amerejea mazoezini baada ya kuwa na likizo ya muda wa wiki tatu mchezaji huyo alikuwemo kwenye kikosi cha Brazil, kilochoshiriki fainali za kombe la dunia nchini Urusi.
Neymar, amewasili mazoezini na kujiandaa na msimu ujao kwa ajili ya ligi kuu ya Ufaransa.

PSG, wameeka kambi nchini China, kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao lakini siku ya Jumapili mchana watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Monaco, katika dimba la Shenzhen Universiade Sport Center.

Ribery amsifia Vidal

“Kwa mimi, nasema na kuthibitisha kwamba yeye ni bora, na ni mtu wa maadili na kanuni pia.

Ninafurahi sana kucheza nae katika klabu moja, kwa kipindi ambacho tulikuwa wote!

Napenda azidi kuwa bora kwa siku zijazo, yeye ni shujaa katika fani yake na ataendelea kuwa kiongozi huko aendako.”

-Kauli ya Franck Ribery akimzungumzia Arturo Vidal, ambaye yupo mbioni kujiunga na Fc Barcelona ya nchini Hispania.

King Kiba ameanza mazoezi rasmi, Arsenal yamnyatia Vida

$
0
0

Ligi kuu England hiyoooo Inarudi

📆 2 miezi

⏳ 70 siku

⏰ 1,680 masaa

🕑 100,000 dakika

Bila kipute cha England..
Football Is BACK! ⚽

Mwaka mmoja uliopita Juan Mata8
Alianziasha mradi wa kusaidia wa CommonGoalOrg, na kuahidi 1% na kuomba wadau kumsapoti. Pichani ni wale waliokubali.

Klabu ya Arsenal inajiandaa kutoa £25 million ($32m) kwa beki wa Croatia Domagoj Vida, ili kumnasa mlinzi huyo aloyeamba katika michuano ya kombe la duniam

Marko Pjaca amejiunga na Fiorentina kutoka Juventus: huku kukiwa na kipengelea cha kumnunua moja kwa moja.

Klabu ya Everton imenasa saini ya goalkeeper Joao Virginia kutoka katika klabu ya Arsenal nyota huyo amesaini kandarasi ya Miaka mitatu.

Taarifa zinasema pia King Kiba Ali Swalehe kiba ameanza Mazoezi katika klabu yake ya Coastal Union.Mwanamuziki na Mchezaji mpya wa Coastal Union, Ali Kiba akiwa wenzake katika mzaoezi ya timu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.

Burnley imekubali kulipa £13m kama ada ya uhamisho kutoka kwa Middlesbrough ili kumnasa Ben Gibson.

Ndondo Cup mchangani hadi FIFA

$
0
0

Kama una kumbukumbu nzuri utakuwa unakumbuka fainali ya kwanza ya #SportsXtraNdondoCup2014 pale kwenye uwanja wa Bandari, Tandika.

Fainali hiyo iliwakutanisha waliokuwa mabingwa wa kwanza Abajalo FC dhidi ya Tabata United waliofungwa kwa penati huku penati ya mwisho ikifungwa na Kelvin Sabato maarufu kama Kiduku ambaye kwa sasa anachezea Mtibwa Sukari ya Morogoro inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara lakini wakati huo baada tu ya mashindano alijiunga na Mwadui FC ikiwa ligi daraja la kwanza na kuisaidia kupanda ligi kuu huku yeye akiibuka mfungaji bora wa ligi daraja la kwanza.

Nataka kukukumbusha kuhusu waliosimamia mchezo huo, kwa maana ya waamuzi, kama una kumbukumbu nzuri katikati alisimama Hery Sasii akisaidiwa na Helen Mduma pamoja na Idd Lila wakati Shafii Mohamed yeye alikuwa fourth official.

Waamuzi hawa wakati huo walikuwa katika kiwango cha kawaida tofauti na ilivyo sasa ambapo watatu kati yao wanatambuliwa na Fifa ambao ni Hery Sasii, Helen Mduma pamoja na Idd Lila.

Haya ni mafanikio makubwa kwa #NdondoCup kuona watu waliopita kwenye mashindano haya wanafanikiwa na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.

Hery Sasii aliyesimama katikati katika fainali hiyo amekuwa mwamuzi bora wa ligi kuu Tanzania bara kwa misimu miwili mfululizo sasa na hii ni kutokana na kazi yake nzuri anayoifanya pindi anaposimamia dakika 90 za mchezo.

Kesho Jumapili August 5, 2018 fainali ya 5 na #NdondoCup itachezwa katika uwanja uliotumika kwa fainali ya kwanza lakini mwaka huu zikibadilika timu pekee ambapo Manzese United itakabiliana na Kivule United.

Cha kufurahisha zaidi nachukua fursa hii kuwatambulisha tena waamuzi walewale waliochezesha fainali ya kwanza ndio watakaochezesha fainali ya 5.

Mwamuzi kijana mwenye kujiamini Hery Sasii atasimama katikati akisaidiwa na Idd Lila pamoja na Helen Mduma, hawa wote wanatambuliwa na Fifa huku mezani akiwa ni Shafii Mohamed.

Hii ni historia ya aina yake na ya kupendeza kwenye michuano ya #NdondoCup2018.
#MstueMwana na mwana amstue mwana fainali ya #NdondoCup Jumapili kwenye uwanja wa Bandari, Tandika. Milango itakuwa wazi kuanzia saa 5:00 asubuhi kwa kiingilio cha shilingi 3,000 tu.

Nguzo tegemezi za Mourinho, Klopp na Pep Gurdiola zimeanguka ,wataweza peke yao?

$
0
0

Kesho mchezo wa ngao ya hisani unapigwa kati ya Chelsea vs Manchester City. Hii ni kama honi/kiashirio cha msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza kwa msimu wa 2018/2019 kuanza.

Kuna mambo mengi mapya watu wanatamani kuona, ikiwemo kocha mpya wa Chelsea Marizio Sarri namna ambavyo anaweza kuirudisha Chelsea katika chati.

Juegen Klopp, Jose Mourinho na Pep Gurdiola wenyewe wapo tu kama wapinzani waliopita ,japokuwa msimu huu unaoanza wote watakuwa na mapigo makubwa.

Wote hawa watatu baada ya kipindi kirefu sana watacheza msimu wao wa kwanza bila wasaidizi wao ambao wamekuwa nao kwa muda zaidi ya miaka 10 katika mabenchi yao.

Pep Gurdiola na Domenec Torrent. Pep na Torrent walianza kufanya kazi pamoja mwaka 2007 tangu wakiwa Barcelona B na baadae kwa pamoja wakapanda hadi Barcelona timu ya wakubwa.

Pep na Torrent walikwenda wote Bayern Munich kabla ya kuja Man City lakini mwaka huu mwezi uliopita Torrent alibwaga manyanga kuwa msaidizi wa Pep Gurdiola.

Torrent kwa sasa ni kocha mkuu wa New York City Fc huku Mikel Arteta akirithi mikoba yake kwa Gurdiola, Torrent pamoja na Pep wametwaa makombe 24 tangu wakiwa Barcelona B.

Jurgen Klopp na Zeljko Buvac. Hawa nao wamekaa kwa miaka 17 pamoja, Klopp na Buvac walikutana tangu kabla ya Borussia Dortmund walianza kufanya kazi Mainz mwaka 2001 ndio baadae wakaenda BVB.

2008 hadi 2015 walikuwa pamoja Borussia Dortmund na safari yao kwenda Liverpool ilikuwa moja, mwezi April Buvac aliacha usaidizi wa Klopp japo bado ni muajiriwa wa Liverpool.

Bado kwenye website ya Liverpool Buvac anaonekana kama moja ya makocha wa Liverpool na labda upo uwezekano wa kurejea katika benchi la ufundi la Liverpool katika msimu ujao wa ligi.

Jose Mourinho na Rui Faria. Hawa ndio ambao wamekuwa gumzo kubwa kwa sasa na wengi wanataka kuona je Faria ndio alikuwa anamshauri Mou kuhusu basi au kupaki basi ilikuwa ni style ya Jose Mourinho.

Faria na Mou nao walikutana mwaka 2001 wakapiga kazi Porto baadae Chelsea, kisha wakenda Inter Milan, wakaenda Real Madrid, wakarudi Chelsea kabla ya kuhamia Manchester United.

Tangu Faria aiache Manchester United hali imekuwa si hali, Jose amekuwa akilalamika kila kukicha huku msimu mpya wa ligi bado hata haujaaanza lakini madhara ya Faria yameanza kuonekana.

Inasemekana kwamba kati ya vitu ambavyo Mourinho alikuwa akivuna kwa Faria ilikuwa namna ya kuwapa moyo wachezaji kupambana na hii inaweza labda ikaanza kuwa shida mpya United.

Viewing all 9000 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>