Leo club ya FC Barcelona imetoa maelezo kuhusu afya ya mchezaji wao Lionel Messi ambae alitolewa nje baada ya kupata maumivu wakati wa mechi dhidi ya Athletic Bilbao.
Kwenye mechi hiyo Messi alitolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Arda Turan. Baada ya Messi kufanyiwa uchunguzi wa afya Barcelona wamesema kwamba maumivu aliyopata sio makubwa sana.
Barcelona wamesema kwamba mchezaji wao yupo vizuri na huenda akarudi tena uwanjani Jumatano kwenye mechi ya Copa Del Rey. Lakini kwenye mechi ya wiki ijayo dhidi ya Malaga kuna uwezekano mkubwa akacheza tena kama kawaida.