
Nahodha na golikipa namba moja wa kikosi cha Toto Africans Erick Ngwegwe ame-graduate masters degree Jumamosi iliyopita siku ambayo kikosi cha Toto kilichezea kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Ngwegwe amehitimu masters ya History kwenye Chuo Kikuu cha St. Augustine cha jijini Mwanza na huenda golikipa huyo ndiye mchezaji mwenye elimu ya juu kuzidi wachezaji wengine wanaocheza soka kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kwa sasa.

Golikipa huyo alipata degree yake ya kwanza ya Education lakini akaona bado anahitaji kusonga mbele kwenye elimu ya darasani na kuamua kupiga book zaidi na hatimaye amemaliza mastars yake ya History.

Mbali na golikipa huyo kuhitimu masters degree, mwandishi wa habari za michezo Lasteck Alfred kutoka kampuni ya The Guardian Limited wachapishaji wa magazeti ya The Guardian, Nipashe na Lete Raha pia alikuwa miongoni mwa wanafunzi waliohitimu masters siku hiyo.
Lasteck amehitimu masters degree ya Mass Communications pamoja na Erick Ngwegwe kwenye mahafali ya Chuo Kikuu cha St. Augustine Mwanza yaliyofanyika January 16, 2016.


Mtandao huu (shaffihdauda.co.tz) kwa niaba ya wafanyakazi wote unwapongeza Erick Ngwegwe na Lasteck Alfred kwa hatua kubwa waliyopiga katika elimu. Tunaamini elimu waliyoipata itakuwa na tija katika sekta ya michezo Tanzania na wao watakuwa mfano wa kuigwa kwa wanamichezo wengine ambao wako shuleni au wanaotaka kurudi shule kujiendeleza.
Kwa pamoja tunasema Hongereni sana!!