Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

LIVERPOOL YASONGA MBELE FA CUP, HIZI NI REKODI 4 UNAZOHITAJI KUZIFAHAMU

$
0
0

Ojo 2

Usiku wa January 20 klabu ya Liverpool ilifanikiwa kusonga mvbele kwenye michuano ya FC Cup baada ya kuivurumisha klabu ya Exeter kwa bao 3-0 na kufanikiwa kutinga raundi ya nne ya michuano hiyo.

Ojo 1

Mabao ya Liverpool yalikwamishwa wavuni na Joe  Allen ambaye alifunga bao la kuongoza ikiwa ni dakika ya 10 tu tangu kuanza kwa mchezo huo. Dakika ya 74 Sheyi Ojo akaiandikia Liverpool bao la pili wakati Joao Teixeira akamaliza kazi kwa kupachika bao la tatu dakika ya 82 na kitupa nje Exeter nje ya michuano ya FA Cup.

Ojo 3

Sheyi Ojo aliibuka man of the match wa mchezo huo akifanikiwa kufunga bao safi huku akionesha kiwango bora . Kinda huyo wa Liverpool alitokea benchi na kuwa msaada mkubwa kwa timu yake kwenye mchezo huo.

Ojo 4

Rekodi ambazo unahitaji kuzifahamu

  • Baada ya kucheza michezo 17 kwenye mashindano yote bila kufunga goli, Joen Allen amefanikiwa kupa bao baada ya kupata nafasi kwenye kikosi cha Liverpool.
  • Brad Smith amehusika moja kwa moja kwenye upatikanaji wa magoli yote matatu yaliyofungwa na Liverpool dhidi ya Exeter. Amefunga gaoli moja na kutoa assists mbili.
  • Liverpool haijapoteza mchezo wowote hadi kwenye hatua ya raundi ya nne ya michuano ya FA Cup ikiwa imecheza michezo 15 bila kupoteza hata mmoja. Imeshinda michezo 12 na kutoka sare mara 3.
  • Liverpool imeshinda michezo sita na haijapoteza mchezo wowote kwenye michezo yake sita ya FA Cup kati ya michezo nane ya FA Cup kwenye dimba la Anfield.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>