Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

SPURS YAENDELEZA REKODI BAADA YA KUIADABISHA LEICESTER CITY

$
0
0

Son 4

Mabao yaliyofungwa na Son Heung-min pamoja na Necer Chadli kwa upande wa Tottenham yameipeleka timu yao kwenye raundi ya nne ya michuano ya FA Cup na kuitupa nje ya michuano hiyo klabua ya Leicester City ambayo ni klabu sumbufu kwas asa kwenye ligi kuu ya England.

Son 1

Mchezo huo ambao ulizikutanisha timu zote zilizopo kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi kuu ya England ilitarajiwa kuwa mchezo mgumu kutokana na timu hizo kwenda sare kwenye mchezo wao wa awali.

Son 2

Lakini Spurs walijitoa kwenye matatizo baada ya kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 39 wakati ambapo Son aliachia shuti kali akiwa umbali wa mita 18 kutoka golini shuti ambalo lilimshinda mlinda mlango wa Leicester Kasper Schmeichel.

Son 3

Necer Chadli akaipatia Spurs bao la pili alilofunga dakika ya 66 akimalizia kazi iliyofanywa na Son na kihakikishia Spurs unshindi kwenye mchezo huo.

Son 5

Haya ni mambo muhimu ambayo unapaswa kuyafahamu kuhusiana na mchezo huo:

  • Kwenye michezo 13 waliyokutana kwenye kombe la FA Cup (pamoja na mechi mbili za marudiano), Spurs wameshinda michezo nane wakati Leicester wakiwa wameshinda michezo mitatu pekee.
  • Spurs haijapoteza mchezo ikiwa ugenini kwenye michuano ya ndani (England) tangu siku ya kwanza ya mechi ya ufunguzi ya msimu walipokubali kichapo pale Old Trafford.
  • Spurs wamekuwa wa kwanza kufunga kwenye michezo nane iliyopita waliyokutana dhidi ya Leicester City.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>