Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

EL HADJI DIOUF: GERARD ANANIONEA WIVU

$
0
0

Gerrard vs DioufMshambuliaji wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya Senegal, El Hadj Diouf amemjibu nahodha wa zamani wa Liverpool, Steven Gerard kutokana na alichokiandika Gerard katika kitabu chake hivi karibuni.

Gerard ambaye anaichezea LA Galaxy ya Marekani hivi sasa, ameandika katika kitabu chake kiitwacho ‘My Story’ akimuelezea Diouf kama usajili mbaya kwa maana Diouf alikua haijali Liverpool bali yeye mwenyewe.

Gerard ameandika kwamba mara kadhaa watu walimuuliza kama kuna ushabiiano wa tabia kati ya Diouf na Mario Baloteli, lakini Gerard anasema siku zote huwa anasema haoni uhusiano wa tabia zao, huku akiamini Diouf alikua ni mtukutu zaidi.

Akiongea na kituo cha radio nchini kwao Senegal, El Hadj Diouf amesema kuwa yote hayo yamemtoka Gerard kwa sababu ya wivu wake tu juu ya kipaji cha msenegali huyo aliyeng’arisha fainali za kombe la dunia 2002 akiwa na Senegal.

Diouf anaekipiga katika klabu ya Bhai nchini Malaysia, anasema Gerard lazima amuonee wivu kwa maana Gerard hajapata mafanikio ya kimpira kama yeye.

Diouf anajinadi kuwa alitangazwa miongoni mwa wachezaji 7 bora duniani mwaka 2002, akaingia pia katika orodha ya wanandinga 100 bora wa karne, kitu ambacho hajakipata Gerard.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles