Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

JE CHELSEA WATAWEZA KUWATOA PSG DARAJANI?

$
0
0

PSG vs Chelsea

Chelsea na PSG walioneshana kazi katika pambano la kwanza la hatua ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya lakini ni wenyeji PSG ambao walitoka kifua mbele kwa ushindi wa bao 2-1.

Shukrani zimuendee Super sub Edinson Cavani aliyefunga goli la ushindi katika dakika ya 78 ya mchezo akitokea benchi kuchukua nafasi ya Mbrazil Lucas Moura.

PSG vs Chelsea 1

Matokeo hayo yanawaweka PSG kifua mbele kuelekea mchezo wa marudiano utakaofanyika Stamford Bridge lakini kwa mujibu wa kocha wa Chelsea Guus Hiddink goli la John Obi Mikel ni muhimu sana kuifanya Chelsea iweze kufuzu katika hatua hii ya mtoano.

Kocha wa muda wa klabu hiyo Mholanzi Guus Hiddink ametoa ya moyoni juu ya Matokeo ya mchezo huo na nini mikakati ya mchezo wa marudiano utakaofanyika Stamford Bridge.

“Mwisho wa siku kufungwa kunauma lakini naamini bado tupo kwenye mbio. Katika michezo miwili goli la ugenini ni bora zaidi kama tutaweza kushinda na kufuzu Stamford Bridge hapo kipigo kitakuwa hakina maana sana.

“Kipigo sio kitu kizuri, lakini ni mashindano ya michezo miwili, kufunga goli ugenini mara zote ni vizuri tulilijua hilo na tulijidhatiti vizuri na tulizuia vizuri.

PSG vs Chelsea 3

“Kiwango cha wachezaji wetu kilikuwa kizuri lakini nadhani tungetakiwa kumalizia vizuri nafasi tulizopata za mashambulizi ya kushitukiza. Ni vigumu sana kucheza dhidi yao ndio maana sina furaha na kufungwa mchezo huu lakini sio ajabu kufungwa.

Hiddink anaamini matokeo yanaweza kubadilika na mchezo huo ni 50-50 kwa sababu bado kuna wiki kadhaa za kujiandaa na mchezo huo.

PSG vs Chelsea 2

Beki wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand amemlaumu kiungo Mnigeria John Obi Mikel kwa kukwepa shuti la Zlatan Ibrahimovic kitendo kilichosababisha goli la kwanza kwa PSG

“Katika vyumba vya kubadilishia nguo nina uhakika wamesema umefanya nini? Kama huwezi kuzuia mpira ni bora usikae kwenye ukuta.

PSG vs Chelsea 4

Mchezo mwingine ulikuwa ni kati ya Benfica na Zenit Saint Petersburg ya Urusi ambao ulimalizika kwa Benfica kushinda ushindi wa goli 1-0 lililofungwa dakika 91 na Jonas

Kuhusu suala la John Terry Hiddink alisema hana sababu ya kumuwahisha Terry uwanjani watasubiri mpaka apone kabisa ndiyo arudi uwanjani.

PSG vs Chelsea 5

Chelsea watacheza na Manchester City Jumapili katika mchezo wa  kombe la FA raundi ya tano.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>