Lilikuwa ni tukio kubwa kutoka kwa superstar wa kireno na haipaswi kubeza kitu alichokifanya Ronaldo ukizingatia kila tukio analofanya linarekodiwa na mamia ya camera kila sekunde ya siku.
Ronaldo alitoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo akiwa ameambatana na msichana mdogo kabla ya kuanza kwa mchezo wa kwanza wa Champions League dhidi ya AS Roma Jumatano usiku.
Wakati wimbo wa UEFA unapigwa, Ronaldo alimbusu mtoto huyo kwenye shavu lake la kusho kitendo ambacho kilionekana kumfurahisha mtoto huyo lakini pia kiligusa hisia za watu wengi ambao walishuhudia tukio hilo.
Katika mchezo huo Real Madrid ilishinda ugenini kwa bao 2-0 dhidi ya Roma. Mabao ya Madrid yalifungwa na Cristiano Ronaldo aliyefunga goli la kwanza dakika ya 57 wakati bao la pili lilifungwa na Jesse.
Takwimu ambazo unahitaji kuzijua
- Goli alilofunga Ronaldo lilikuwa ni goli lake la 12 katika mechi 7 kwenye michuano ya UEFA Champions League.
- Real Madrid ilishindwa kupiga shuti hata moja langoni mwa Roma katika kipindi cha kwanza hiyo ikiwa ni mara kwanza tangu waliposhindwa kufanya hivyo kwa mara mwisho May 2011.
- Real Madrid bado haijafungwa goli lolote katika kipindi cha kwanza kwenye michuano ya UEFA msimu huu, timu nyingine ambayo inashikilia rekodi hiyo ni Bayern Munich.