Amini usiamini kuna watu wanajiongeza kwenye huu ulimwengu hasa pale wanapotafuta namna ya kutimiza malengo na ndoto zao katika maisha.
Michael Olunga alirekodi video akimwomba kocha wa Arsenal mzee Arsene Wenger amsajili kwenye kikosi cha The Gunners huku akimuahidi hatomuangusha na atakuwa ametimiza ndoto zake za kutaka kuitumikia klabu hiyo ya London.
Olunga ambaye alikuwa ni striker wa Gor Mahia inayocheza ligi ya Kenya (Kenyan Premier League) pia anasema ameshafunga magoli 38 katika msimu huu.

Mchezaji huyo bora wa Kenya kwa sasa amejiunga na klabu yabaada ya kuonesha kiwango kizuri wakati wa majaribio aliyofanya kwa kipindi cha mwezi mmoja. Mkenya huyo amepewa mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia klabu hiyo ya Sweden.
Olunga alikaa kwa msimu mmoja tu kwenye klabu ya Gor Mahia akitokea Thika United pia alikuwa mchango mkubwa kwa Gor Mahia kutwaa ubingwa wa KPL kwa mara ya15 bila kupoteza mchezo hata mmoja.