Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

FC Midtjylland 2-1 Man Utd:  Imetosha Sasa – Van Gaal Aondoke – Kazi Ameishindwa

$
0
0

Wamiliki wa Manchester United ‘The Glazers’ na CEO wa klabu hiyo Mr Ed Woodward hawapaswi kuendelea kuvumilia kifo cha taratibu cha klabu hii pendwa inayoendelea kubomoka kila wiki.

  Sifa ya Louis van Gaal kama mmoja wa makocha bora inazidi kupotea kila kukicha, hata ile CV yake ya zamani iliyombeba na kumpa kazi Theatre of Dreams haipo tena, na sifa ya klabu hii ya Old Trafford waliyojijengea kwa miaka mingi inazidi kuharibika.

  Red Devils waligeuka kituko cha kuchekesha watu barani ulaya huko Denmark baada ya kufungwa na timu ambayo ilianzishwa mwaka 1999 – wakati ambao United ilikuwa klabu bora kabisa duniani.
Klabu ambayo ilikuwa inavifunga vilabu vya Barcelona, Real Madrid, Bayern Munich na Juventus katika Champions League – imedhalilishwa na FC Midtjylland katika michuano ya Europa – hii kitu kisichokubalika kabisa kwa klabu ya aina ya Man United.
Miaka miwili iliyopita Mr Woodward alipiga picha kupitia simu yake matokeo ya mchezo katika dimba la Karaiskakis Stadium jijini Athens wakati United ilipofungwa 2-0 na Olympiakos katika raundi ya 16 bora ya Champions League.
Inasemekana picha hiyo aliichukua kwa madhumuni ya kujikumbusha kwamba United haipaswi kufikia hatua ya kunyanyaswa na timu aina ya Olympiakos – na angefanya kila awezalo jambo hilo lisitokee tena. Miaka miwili baadae jambo la aibu zaidi limetokea, klabu ipo kwenye shimo la aibu ambalo linashusha sana hadhi ya klabu.

  Bora hata wagiriki walikuwa wanaongoza ligi yao ngumu kwa pointi 20 mnamo 2014, lakini timu waliyofungwa nayo jana usiku haikuwa imecheza mechi yoyote tangu December 10, 2015 huku ikiwa haijashinda mchezo wowote tangu November mwaka jana.
Baada ya mechi ya Olympiakos – David Moyes aliendelea kuwa kocha wa Man United kwa siku 56 zaidi na alifanikiwa kushinda mechi 5 kati ya 10 za mwisho. Lakini upande wa Van Gaal hali imekuwa mbaya kiasi cha kwamba hakuna ambaye angependa kumuona kocha akipewa muda zaidi kama ilivyokuwa kwa Moyes.

  Baada ya mchezo dhidi ya Southampton wengi tulisema ‘imetosha’ lakini LVG akaendelea na sasa hali imezidi kuwa mbaya.
Matokeo ya mchezo wa jumamosi iliyopita yaliwafanya United kupoteza matumaini ya kuingia kumaliza kwenye nafasi 4 za juu na wakaelekeza mategemeo kwenye michuano ya Europa League kuwa njia pekee ya kuingia kwenyw Champions League msimu ujao. Matokeo yake jana usiku wamepigwa 2-1 na kuweka rehani uwepo kwenye michuano hiyo – huku mashabiki waliosafiri kutoka Manchester kwenda Denmark wakidhalilishwa pamoja na kulipishwa fedha nyingi kwa ajili ya viingilio kwenye mechi hiyo – paundi 71, zaidi ya laki 2 za kibongo.

  Mitandao  ya kijamii ililipuka kwa maneno ya kejeli na hasira kutoka kwa mashabiki wote wa klabu hii na hata wapinzani. Mashabiki waliohojiwa kwenye TV ya klabu MUTV pia hawakuweza kuendelea kuvumilia.
Ni muda sahihi sasa kwa uongozi wa klabu kusikiliza na kufanyia kazi vilio vya mashabiki.  
Kwa namna hali ilivyo kama Ed Woodward na Glazers hawatochukua hatua – sitoshangaa kuona mashabiki wakichukia hatua ambazo zitaiumizaklabu – mauzo ya tiketi, merchandise mbalimbali za klabu kususiwa na mashabiki – ukimya wa viongozi hao utasababisha mashabiki kufanya vitu wsivyopenda kuonyesha namna gani wanaumizwa na matokeo ya timu yao.

Inaripotiwa kwamba Van Gaal mwenyewe aliongea na Woodward siku ya Boxing Day baada ya kipigo cha Stoke na kumwambia kwamba kama klabu inadhani kuna mtu mwingine anaweza kuifanya kazi yake vyema basi yeye angeondoka bila hata kudai fidia ya kuvunjiwa mkataba – Kwanini Woodward na wenzie hawakuchukua uamuzi wakati ule – hakuna anayefahamu. 

 Kwa hali ilipofikia sasa – mashabiki hawatojali ni Jose Mourinho, Maurico Pachettino ndio aanayefaa kumrithi Van Gaal – haijalishi kwao – wanachotaka wao ni mabadiliko ya kocha kutokana aliyepo sasa anazidi kuiangamiza klabu yao.
IMETOSHA SASA – LVG AONDOKE


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles