Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

TP MAZEMBE KANISANI KUELEKEA SUPER CUP, ULIMWENGU KAMA KAWA

$
0
0

IMG-20160219-WA0022

Kesho February 20 utapigwa mchezo wa Super Cup kati ya TP Mazembe dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia, unapolitaja jina la TP Mazembe lazima ukutane na jina la mtanzania Thomas Ulimwengu akiipeperusha bendera ya Tanzania kwenye klabu hiyo.

Shaffihdauda.co.tz imepiga story na nyota huyo ambaye kwasasa amebaki mtanzania pekee kwenye timu hiyo baada ya Samatta kuondoka kwenye kikosi hicho cha nchini Congo DR.

IMG-20160219-WA0014

Lakini kubwa zaidi ni utaratibu ambao TP Mazembe wameendelea kuutumia kwenda kanisani kufanya ibada kabla ya kudondoka uwanjani. Mazembe leo walienda kanisani kama walivyofanya wakati wanaelekea kwenye mchezo wao wa fainali ya klabu bingwa Afrika mwaka uliopita.

Shaffihdauda.co.tz: Mabadiliko ya kimfumo kwenye kikosi cha TP Mazembe yapoje, hasa baada ya kuondoka kwa Mbwana Samatta. Ni nani ambaye anacheza kwenye nafasi yake?

Ulimwengu: Tunatumia mfumo ulele wa kocha aliyepita, kwahiyo naona ni kutafuta mchezaji anayeweza kucheza sehemu husika. Naona hakuna mabadiliko makubwa sana ya kimfumo.

IMG-20160219-WA0019

Shaffihdauda.co.tz: Mwaka jana mlikwenda kanisani wakati mnaelekea kwenye fainali ya klabu bingwa Afrika. Vipi mwaka huu kuelekea kwenye mchezo wa Super Cup mmeenda tena kanisani?

Ulimwengu: Kanisani ni lazima twende, hata leo tumeenda pia kumwomba Mungu. Suala la kumwomba Mungu kwa Mazembe ni kawaida kwahiyo kuelekea kwenye mchezo wetu wa kesho tumeendelea na utaratibu wetu wa kwenda kanisani kufanya maombi kabla ya mechi.

IMG-20160219-WA0020

Shaffihdauda.co.tz: Mazembe haikufanya vizuri kwenye fainali za kombe la dunia kwa ngazi ya vilabu kule Japan, kuna mabadiliko yoyote ya kikosi kiuchezaji ukilinganisha kiwango cha Mazembe walichokionesha Japan na sasahivi?

Ulimwengu: Kiwango tulichokionesha Japan kimetokana na watu wengi kutoyatilia maanani yale mashindano. Tulikuwa tumetoka likizo kwahiyo watu hawakuwekea maanani lakini sasa ni mwaka mpya watu wameshakuja kazini kila mtu anatafuta nafasi ya kucheza, kocha mpya, kwahiyo nauhakika watu wengi wataonesha kiwango kizuri.

IMG-20160219-WA0015

Shaffihdauda.co.tz: Binafsi unauzungumziaje mchezo wa kesho ukiwa unaenda kuandika historia ya kuwa mtanzania wa kwanza kucheza mchezo wa Super Cup?

Ulimwengu: Mchezo utakuwa ni mgumu sana wapinzani ni wazuri, lakini na sisi tumejiandaa na mbinu zetu, Mwenyezi Mungu atatujalia tuweze kupata ushindi kwenye hiyo mechi na tuweze kuchukua kombe.

IMG-20160219-WA0017

Shaffihdauda.co.tz: Kuondoka kwa Samatta unahisi kumekuathiri kwa nanmna moja au nyingine katika uwepo wako hapo Lubumbashi?

Ulimwengu: Kuondoka kwa Samatta kumenipa changamoto kubwa lakini hakujaniathiri kwa namna yoyote. Ni changamoto ya maisha ndiyo maana tunapigana tuweze kufika mbali zaidi.

Shaffihdauda.co.tz: Mazembe wanakwenda kwenye mchezo wa Super Cup wakiwa na kocha mpya Hubert Velud amekuja na mbinu ipi ukijaribu kulinganisha na kocha aliyepita Patrice Carteron

Ulimwengu: Huyu namuona anapenda sana kucheza lakini mambo ya kimpira ni yaleyale ambayo tunayoyatumia siku zote ili kuweza kupata ushindi ni jitihada zaidi tukiwa uwanjani kwahiyo naona mambo bado yatakuwa ni yaleyale tu.

IMG-20160219-WA0016

Mchezo huo ndiyo unarasimisha michuano ya klabu bingwa barani Afrika lakini pia kombe la shirikisho 2016. Ni mchezo ambao utazishuhudia TP Mazembe mabingwa mara tano wa kombe la Afrika dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia.

TP Mazembe wameshawahi kuchukua kombe la Super Cup mara mbili, 2010 na 2011. Wataingia uwanjani kutafuta ubingwa huo kwa mara ya 3. Eoile pia wamechukua taji hilo mara mbili mwaka 1998 na mwaka 2008 kwahiyo nao wanaingia kusaka taji hilo kwa mara ya 3.

Kombe hilo lilianza mwaka 1993 ambapo klabu ya kwanza kuchukua kombe hilo ilikuwa ni Africa Sports ya Ivory Cost na mwaka jana klabu ya Entente Sportive de Séti ilinyakua kombe hilo.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>