Mchezajiwa Manchester United aliyepo kwa mkopo katika klabuya Hull City Nick Powell amesema aliamua kucheza game la FIFA kuliko kuangalia mechi ya United dhidi ya klabu ya Mitdjyland ya kule nchini Denmark.
“Nilisahaukabisanilikuwanacheza FIFA’ Powell aliwaambia waandishi wa habari kuelekea mchezo wa FA raundi ya tano dhidi ya Arsenal
“Nilisomatutarifanasijui, ni vigumu.Wana wakati mgumu kwa sababu kocha ameshasema hiyo ndiyo njia ya uhakika ya wao kucheza ligi ya mabingwa mwakani”
“Walikuwa na majeruhi wengi sana ikiwemo Wazza kuwa nje na David kuumia kabla ya mchezo. Lakini hakukuwa na sababu ili kuwa lazima washinde tu”.
Naye kocha wa Hull City ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Manchester United amesema: “ni matokeo yanayo katisha tamaa wapo katika kipindi kigumu sana lakini naamini watarejea”.
Hull City wanacheza na Arsenal katika pambano la raundi ya tano ya kombe la FA ambalo Arsenal ndiyo watetezi wa kombe hilo.