
Azam FC leo asubuhi imeendelea na maandalizi ya kuikabili Bidvest Wits ya Afrika Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Jumapili kwenye uwanja wa Azam Complex kuanzia saa 9:00 alasiri.

Azam FC ilipata ushindi wa mabao 3-0 kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika uwanja wa Bidvest jijini Johannesburg Afrika Kusini, inahitaji ushindi wowote au sare ya aia yoyote ili kuweza kusonga mbele kwa raundi ya pili ya michuano hiyo.

Endapo Azam wakiingia raundi pili, watakutana na timu kati ya Esperance ya Tunisia au Renaissance ya Chad, ambayo imefungwa mabao 2-0 na waarabu hao kwenye mechi ya kwanza wakiwa nyumbani jijini N’Djamena.
