Nahodha wa England na klabu ya Manchester United Wayne Rooney leo anatarajiwa kurudi tena dimbani baada ya kukosa michezo miwili ya timu yake kati ya Liverpool na PSV wiki iliyopita kutokana na kuwa majeruhi.
Kocha wa United, Louis Van Gaal amesema haikua ishu kubwa sana bali waliona ni vyema kutomsababishia makubwa nahodha wao. Leo anatarajia kuwaongoza wenzake katika mechi ya ugenini dhidi ya Southampton.
Marcos Rojo anaweza kuchukua nafasi sehemu ya ulinzi kuziba pengo la majeruhi Luke Shaw atakae kaa nje ya uwanja kwa miezi sita baada ya kuvunjika mfupa wa mguu mara mbili alipocheza dhidi ya PSV Jumanne iliyopita katika michuano ya ulaya.
Phil Jones yuko fiti lakini huenda akasubiri kutokana na kutokua na fitness ya mechi baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda hivi sasa. Mechi hiyo itakayopigwa saa kumi na mbili jioni saa za kwetu Tanzania kupitia DSTV.
Kwa upande wao Southampton watakua wakitarajia Saidio Mane kuwa katika fomu yake ya hali ya juu ili kuwadhuru United ambao watataka kupata matokeo kujiimarisha zaidi katika mbio za ubingwa msimu huu.