Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

WAAMUZI WANALIPWA VILEVILE, JE, TF F INAJENGA KITU GANI….?

$
0
0

Refaree's kit

 Na Shaffih Dauda, Dar es Salaam

 LIGI Kuu Bara Jumamosi hii imeingia katika wiki yake ya pili kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja tofauti.

Jana kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Tanzania Prisons imecheza na Mbeya City, kule Shinyanga kwenye Uwanja wa Kambarage, Stand United ikacheza na Africans Sport wakati pale Mkwakwani, Tanga, wenyeji Mgambo JKT walikutana na Majimaji FC.

Jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa, mabingwa watetezi Yanga wakacheza na JKT Ruvu ambayo ni majeruhi waliopoteza mechi tatu mfululizo.

 Jumla ya mechi 30 tangu ligi hiyo ilipoanza wiki iliyopita zimeshachezwa. Licha ya ligi kuanza kwa ushindani tayari kuna baadhi ya maeneo katika udhamini wake, hali si vile ilivyotarajiwa.

Hapa nazungumzia waamuzi, ambapo kabla ya kuanza kwa ligi, wadhamini wakuu Kampuni ya huduma za simu za mikononi ya Vodacom, ilisema ingeboresha malipo yao.

 Kabla ya ligi kuanza ilisemwa kuwa waamuzi watakuwa wakilipwa kiasi cha Sh 550, 000 kwa kila mechi watakayochezesha lakini katika uchunguzi nilioufanya, nimegundua kuwa waamuzi hawapewi kiasi hicho cha fedha.

 Hili limetokea katika michezo ya mzunguko wa kwanza na ule wa pili. Wamepewa kati ya Sh 350, 000 hadi Sh 400, 000, tena kwa baadhi tu. Hakuna mwamuzi aliyelipwa kiasi kinachofikia Sh 500, 000 hadi sasa.

 Kocha wa JKT Ruvu, Fred Minziro mara baada ya timu yake kufungwa mabao 3-0 na Mbeya City Jumatano iliyopita, alinukuliwa akilalamikia maamuzi ya waamuzi wawili.

Alimlaumu mwamuzi wa kati kwa kitendo alichokiita ‘kuwapa’ Mbeya City penati isiyo halali, pia akamlalamikia mwamuzi wa pembeni kwa kuruhusu bao la tatu la Mbeya City wakati mfungaji alikuwa ‘off side’. Minziro alimaanisha kuwa waamuzi walichezesha vibaya mechi hiyo waliyopoteza.

 Ukitazama kwa makini unaweza kupata sababu ya kuwalaumu wahusika kwa kushidwa kuwalipa waamuzi vile inavyotakiwa kwa kuwa njia yingine ya waamuzi kuharibu mechi ni kuipendelea timu ambayo itakuwa na maslahi mazuri kwa upande wake.

Simaanishi kuwa waamuzi wa mechi hiyo walikuwa upande wa City, wala sina maana kuwa maneno ya Minziro yanamaanisha jambo hilo, ila wakati mwingine sababu za maslai madogo pia huchangia waamuzi kuzipendelea baadhi ya timu.

 Inawezekana mwamuzi akashindwa kuimudu mechi kwa sababu ya kushindwa kutafsiri sheria za mchezo, ama inaweza ikawa kwa utashi au mapenzi yake tu kwa timu fulani.

Ama inaweza kuwa anatumika kwa maana ya kukubali kupewa rushwa ili kuipendelea timu fulani ambayo itakuwa ikihitaji matokeo.

 Nakumbuka wakati ule wa kusainiwa kwa mkataba mpya, Vodacom kama wadhamini wakuu wa ligi na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, kwa pamoja walisema moja kati ya maeneo ambayo watahakikisha upungufu haujitokezi ni upande wa waamuzi, Akasisitiza kuwa, waamuzi watakuwa ‘fair’ kabisa na ili kuhakikisha hilo linafanyika, wamewaongezea posho ili wapate kiasi cha fedha kinachoweza kuwasaidia kujikimu.

Hali ni tofauti sasa, kwani bado fedha haijaongezwa na leo mechi zinaendelea kuchezwa, Je, haki itatendeka kama ilivyotarajiwa? Hapa lazima lifanyike jambo la sivyo imani kwa mdhamini na TFF itapungua.  

Kwa mwenendo huu, ni kama TFF inafungua mianya kwa waamuzi hao kutafuta fedha kwa namna nyingine ili waweze kuishi. Waamuzi wanakuwa na gharama za lazima katika maeneo wanayokwenda kuchezesha mechi.

Ningependa kuona TFF inatekeleza hili la ongezeko la posho za waamuzi kuelekea michezo ya mzunguko wa tatu wikiendi hii.

 Kingine ni katika suala la vifaa vya waamuzi, namaanisha jezi zao za kuchezeshea mechi. Misimu iliyopita wadhamini walikuwa wakitoa begi la michezo kwa kila mwamuzi, ndani yake kuliwa na jozi  mbili tofauti za jezi, viatu na soksi.

Lakini sasa wamekuwa wakipewa jozi mojamoja tu ya vifaa hivyo. Je, ikitokea jezi za waamuzi zimetofautiana au kufanana na za timu husika hali itakuwaje?

Kutokana na hali hiyo, waamuzi wengi wamekuwa wakilazimika kuingia sokoni tena kwa kutumia kiasi hichohicho kidogo wanachopewa kama posho kununua jezi nyingine.

Tunajenga kitu gani kwa mwamuzi anayekutwa na hali hii?


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>