Real Madrid kwa mara nyingine tena watakuwa wanamuangalia mshambuliaji wao Cristiano Ronaldo wakati watakaposafiri kwenda kupambana na Wolfsburg katika robo fainali ya michuano ya kombe la ulaya.Mshambuliaji huyo wa Ureno mpaka sasa ameshaifungia Madrid magoli 13 katika michuano ya ulaya msimu huu baada ya mechi 8, mbele ya mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandoski katika chati ya ufungaji.
Nahodha wa Ureno pia yupo katika mchuano wa kuendelea kuwa na rekodi ya kuwa mfungaji bora wa UCL wa muda wote dhidi ya mpinzani wake Lionel Messi – Ronaldo anaongoza kwa kufunga magoli 90 mpaka sasa.
Goli lake muhimu katika uwanja wa Stadio Olimpico, lilofanya matokeo kuwa 2-0, lilipelekea mchezo wa pili katika dimba la Bernabeu kuwa wa kukamilisha ratiba na kuiwezesha Madrid kufuzu kuelekea robo fainali.
Ushindi wa Champions League, ambao utaleta taji la 11 Benarbeu kwa hakika utamuweka Zinedine Zidane katika historia tajiri ya Madrid na kumpa himaya katika dunia ya makocha duniani.
Ronaldo pia yupo katika mission ya kuivunja rekodi yake ya kufunga magoli zaidi katika msimu mmoja wa ulaya – magoli 17, ambayo aliiweka msimu ambao Madrid walichukua taji lao la 10 la ulaya. Katika magoli yake 13 ya msimu huu, ni mawili tu ameyafunga kupitia mikwaju ya penati.
Messi amezidi kuachwa nyuma kwenye vita yake na Ronaldo ya kuwa mfungaji bora wa michuano hii wa muda wote – msimu huu amefunga magoli 7 tu, idadi sawa na mchezaji mwenzie wa Barca Luis Suarez.
Magoli manne aliyofunga dhidi ya Malmo katika hatua ya makundi – ndio idadi kubwa aliyofunga katika mechi moja msimu huu.
Kuelekea mchezo dhidi ya Wolfsburg – Ronaldo atakuwa anaitazamia rekodi yake bora dhidi ya vilabu vya Bundesliga, ambvyo dhidi yao amefunga magoli 7 katika viwanja vya ugenini.
Magoli yake mawili dhidi ya bayern msimu wa 2013/14 ni moja ya magoli yake ya kukumbukwa, lakini pia Schalke na Borussia Dortmund wamewahi kuwa wahanga wake.
Wakati huo huo mpaka kufikia sasa Ronaldo amefunga magoli 29 katika La Liga, na amejiweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa tuzo ya Pichichi mbele ya Suarez.