Wachezaji wa timu ya basketball ya Savio kutoka Don Bosco Youth Center wakisherekea ubingwa wa mkoa wa Dar es Salaam baada ya kuifunga Vijana City Bulls kwa jumla ya vikapu 66-59Timu ya mpira wa kikapu Savio kutoka maeneo ya Upanga jijini imetangazwa kuwa mabingwa wapya wa mkoa wa Dar es Salaam baada ya kuichapa Vijana City Bulls kwa jumla ya vikapu 66-59.
Savio kutoka Don Bosco Youth Center kwasasa ndiyo wanashikilia ubingwa wa kikapu Dar baada ya kutangazwa rasmi kufatia kuishinda Vijana kwenye mchezo wa fainali ya michuano hiyo.