Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

EXCLUSIVE: KIIZA AFAFANUA MAANA YA STAILI YAKE YA USHANGILIAJI…

$
0
0
Hamisi Kiiza akishangilia goli la kwanza na wachezaji wenzake wa Simba

Hamisi Kiiza akishangilia goli la na wachezaji wenzake wa Simba alipofunga wakati timu yake inacheza dhidi ya Kagera Sugar Jumapili kwenye uwanja wa Taifa

Mshambuliaji wa Simba Hamisi Kiiza jana alifanikiwa kuweka rekodi kwenye msimu huu wa ligi kwa kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli matatu (hat-trick) kwenye mchezo kati ya Simba dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa Jumapili kwenye uwanja wa taifa.

Baada ya mchezo huo kumalizika, mtandao huu ulipata nafasi ya kuzungumza na Kiiza licha ya mchezaji huyo kuonekana kuwa na haraka ya kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. Kikubwa tulichotaka kujua ni siri ya kasi aliyoanza nayo mshambuliaji huyo raia wa Uganda ambae ameshafunga kwenye mechi zote tatu na jingine ni kuhusu staili aliyoitumia kushangilia kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar.

Shaffihdauda.com: Kiiza umekuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli matatu nadi ya msimu huu, nini siri ya mafanikio yako maana mbali na kufunga goli tatu leo lakini kila mechi umefunga

Hamisi Kiiza: “Tumeshinda kwasababu tumecheza kitimu, tulifanya mazoezi kitimu sifa zote zinaenda kwa timu yangu na sio mimi”.

Shaffihdauda.com: Umefunga hat-trick leo (jana) mechi ijayo unakutana na Yanga, mchezo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa timu zote mbili. Itakuwa mechi yako ya kwanza dhidi ya timu yako ya  zamani ya Yanga tangu utue Simba, watu watarajie nini siku hiyo?

Hamisi Kiiza: “Ni mechi ngumu sana inafaa kujipanga, bado hatujakaa sawa kama vile tunavyotaka. Tunamuomba Mungu ili tupate matokeo mazuri kwenye mechi hiyo”.

Shaffihdauda.com: Kila bao ulilofunga ulikuwa unashangilia kwa kuashiria muda, ulikuwa unamaanisha nini kwa kufanya hivyo?

“Namaanisha ligi bado kwahiyo kuna mambo mengine mazuri yanakuja, mashabiki wa Simba waendelee kutupa muda na kuwa na subira”.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles