
Mashabiki wa timu ya Simba wakizawadia fedha mshambuliaji wa timu hiyo Hamisi Kiiza aliyefunga magoli matatu kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar
Mashabiki wa timu ya Simba ‘Mnyama’ walishindwa kuzuia furaha zao baada ya Hamisi Kiiza kuipa Simba ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa.
Baada ya mpira kumalizika baadhi ya mashabiki walioukuwa wamekaa karibu na lango kuu la kuingilia na kutokea uwanjani, walimwita mshambuliaji huyo aliyetupia hat-trick ya kwanza msimu huu na kumpa zawadi za pesa na vitu vingine kutokana na kufurahishwa na kiwango alichokionesha Kiiza.
Kiiza hakusita kupokea fedha hizo kutoka kwa mashabiki waliokuwa wakiimba wimbo wa kumsifia Kiiza wakati akitoka uwanjani. Baada ya kuzipokea zawadi hizo Kiiza aliwashukuru mashabiki hao na kuelekea vyumbani.