Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Panama Paper Leaks: Raisi wa FIFA ahusishwa na skendo ya rushwa ya uuzaji wa haki za matangazo ya TV

$
0
0

Raisi wa FIFA Gianni Infantino ametoa utetezi zaidi kuhusu nafasi yake kuhusiana na sakata la ‘Panama Papers Leak’ linahusisha dili la haki ya matangazo ya TV.

  Infantino alichagulia kuwa raisi wa FIFA mwezi February akimrithi Raisi aliyejiuzulu na kisha kufungiwa Sepp Blatter – sasa ana majukumu ya kulisafisha shirikisho hilo baada ya taswira yake kuchafuka na skendo za rushwa. 

Issue ya skendo ya rushwa imeibuka baada ya kuvujishwa kwa siri kupitia magazeti ya Panama iliyotoa taarifa za makampuni ya mifukoni na kuhusisha taasisi na watu wengi maarufu. Taarifa iliyoibuliwa inasema kwamba kampuni ya Cross Trading iliyopo Panama, ikiongozwa na wakurugenzi ambao walihusishwa na skendo ya FIFAGate, walipata faida kubwa katika uuzwaji wa mara mbili wa haki za matangazo ya TV ya michuano ya Champions League.

Uuzaji wa kwanza kabisa  wa haki za matangazo ya TV, muongo mmoja uliopita, mkataba wake ulisainiwa mwaka 2006 na wakurugenzi wawili wa UEFA akiwemo Infantino ambaye alikuwa mkuu wa kitengo cha sheria cha shirikisho. 

Cross Trading ililipa kiasi cha $111,000 kununua haki za matangazo ya UCL, kisha wakauza haki hizo kwa kampuni ya utangazaji ya Ecuador  Teleamazonas kwa $311,700.
Mnamo March 2007 Cross Trading walirudi tena na kununua haki za kombe la UEFA CUp na UEFA Super Cup kwa $28,000 kisha wakaenda kuwauzia tena Teleamazonas kwa  $126,200.
Uchunguzi uliofanywa na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali wa Uswiss katika kesi ya uvunjifu wa sheria katika shirikisho la soka duniani – ulipelekea maofisa wa usalama kuvamia za UEFA na TEAM Marketing (Kitengo cha masoko cha UEFA) ili kupata ushahidi. 
Mnamo mwaka 2006 hakuna aliyekuwa na idea kwamba wakurugenzi wa Cross Trading Hugo na Mariano Jinkis wangekuja kuwa kwenye mkono wa sheria nchini Marekani kupitia  United States Department of Justice kutokana na tuhuma za utapeli, rushwa katika level ya juu kwenye soka huko Latin American.

  Katika mahojiano yake na harida la Kicker la Ujerumani, Infantino alisema: “Mchakato mzima ulikuwa sawa na kuwekwa vielelezo, lakini namna ulivyoripotiwa kwenye vyombo vya habari inatia aibu. Kitengo cha masoko kilitoa maoni kwamba atakayetoa ofa mbili za juu zaidi apewe mkataba wa haki za matangazo ya TV.

“Mkataba ulijadiliwa na timu ya masoko kwa kina na kwa mujibu wa kanuni za shirikisho, ulisainiwa na wakurugenzi wawili wa UEFA. Kwa maana hiyo, mimi nikawa mmoja wa wakurugenzi lakini ilitegemea na upatikanaji wa wakurugenzi kwenye shrikisho, wangeweza kuwa hata wakurugenzi wengine.

“Kama, baada ya mkataba kusainiwa, wanunuzi wa haki hizo wakaenda kufanya biashara kinyume na sheria, basi sio UEFA au mimi tuliohusika na jambo hilo.”

Hata hivyo UEFA walichangia sana katika kulikuza sakata hili baada ya kukataa kufanya biashara ya aina yoyote au mahusiano ya kimamkataba na Cross Trading na wakurugenzi wake Hugo na Mariano Jinkis pamoja na kupewa ushahidi ulionesha vinginevyo. Lakini baadae wakjirudi na kusahihisha kanusho lao kwa kusema taarifa waliyotoa mwanzo haikukamilika. 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>