Kocha wa Coastal Union Ally Jangalu anasema mchezo wa dhidi ya Simba angeumaliza mapema kama angekuwa na beki wake Miraji Adam ambaye anacheza Coastal kwa mkopo akitokea Simba huku akiwa na pingamizi la kucheza dhidi ya timu yake ya Msimbazi.
Kijana huyo ameakiiokoa timu yake hiyo anayoichezea kwa mkopo kutokana na umahiri wake wa kupiga mipira ‘iliyokufa’. Adam ameshawaliza Azam pamoja na Yanga kwenye uwanja wa Mkwakwani akitumia vyema mipira ya adhabu ndogo.
“Kama angekuwepo Mireaji Adam leo kwa mipira ile tuliyokuwa tunapata nje ya 18 mchezo tungeumaliza mapema, Simba walitufunga Tanga lakini ni kutokana na udhaifu tuliokuwanao sisi. Sikuile golikipa wetu hakuwa mchezoni kwahiyo tukamwambia makosa ya sikuile asiyarudie kwenye mchezo wa leo ndiyo maana leo amedaka kama ambavyo huwa anadaka kila siku”, anasema kocha huyo ambaye timu yake ilipoteza mchezo wa ligi dhidi Simba mwezi March kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Simba iliifunga Costal Union kwenye michezo yote ya ligi kuu ya Vodacom msimu huu lakini leo imeshindwa kuchomoka dhidi ya timu hiyo ya mkiani mwa ligi.
Coastal Union inaungana na Azam FC, Mwadui FC pamoja na Yanga SC na kukamilisha idadi ya timu nne zitakazocheza nusu fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup.
Simba imekubali kichapo cha magoli 2-1 kutoka kwa Coastal Union kwenye mchezo wa robo fainali uliopigwa uwanja wa taifa na kusukumwa nje ya michuano hiyo ambayo bingwa wake ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.