Anaitwa Hueng-Min Son, baada ya kufunga bao 14 msimu uliopita katika Bundesliga Marcio Pocchetino alikubali Spurs itoe paundi milion 22 kumnunua kijana huyu toka Korea kusini akiichezea Bayer Leverkusen.
Jana akianza katika kikosi cha Spurs kilichosheheni vijana watupu kikiwa na wastani wa miaka 24 kwa kikosi kilichoanza dhidi ya Crystal Palace alifunga bao pekee la ushindi ikiwa ni mechi yake ya pili akiwa na Spurs.
Son amefunga mabao matatu katika mechi mbili alizoichezea Tottenham mabao mawili akiyafunga katikati ya wiki katika michuano ya Europa League.
Jumatano atakuwa na kazi ngumu kuiongoza Spurs dhidi ya Arsenal katika mechi ya kombe la Capital one katika uwanja wa White Hart Lane jijini London.
Yawezakua ni neema kwa kijana huyu ambaye amempokea Harry Kane kufunga lakini pia ni mtihani kwa kikosi cha Arsenal ambacho kama kitazubaa basi kinaweza kufungwa katika mechi 3 mfululizo hali ambayo itawafanya watu wajiulize kwanini Wenger hakusajili hasa kwa watu kama Son au Martial yule wa Man United ambao Impact yao imeanza kuonekana mapema kabisa katika mechi hizi za mwanzo.
Tottenham vs Arsenal Jumatano Macho yangu yatakua kwa kijana huyu wa Korea.