Moja kati ya wachezaji walioirudisha Liverpool kwenye mchezo ni pamoja na Divock Origi ambaye alifunga goli la kwanza dakika chache baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.
Kinda huyo wa Ubeligiji anakisema kile ambacho Jurgen Klopp aliwaambia wachezaji wake kwenye vyumba vya kuvalia wakati wa mapumziko.
“Wakati wa mapumziko kocha alituambia lazima tutengeneze kitu cha kuja kuwasimuli watoto au wajukuu zetu na kuufanya usiku huu kuwa maalumu kwa mashabiki”, amesema Origi ambaye alifunga bao la kwanza dakika ya 48 kipindi cha pili na kufanya matokeo kuwa 2-1 kabla ya Reus hajawaongezea mlima wa kupanda alipofunga goli la tatu na matokeo kuwa 3-1 lakini magoli ya Sakho na Lovreni yakaokoa jahazi la Liverpool.
Mchezo huo utakumbukwa na wachezaji wa Liverpool na baadaye watakuwa wakiwasimulia wajukuu zao juu ya usiku huo ambao waliingia hatua ya nusu fainali kwa style ya aina yake.
Angalia video Divock Origi akihojiwa baada ya mchezo wa Liverpool vs Borussia Dortmund