Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Jay Z anaifukuzia saini ya Marcus Rashford wa Man United

$
0
0

  Marcus Rashford ni moja ya majina katika wiki za hivi karibuni yamekuwa yakitawala sana midomoni mwa washabiki na waandishi wa habari wa michezo duniani – uwezo wake wa uwanjani umewavutia watu wengi na mmoja wao ni rapper/mfanyabiashara JAY Z

Kampuni ya uwakala wa wanamichezo ya mwanamuziki huyo, Roc Nation Sports, ni moja ya taasisi/watu wanaowania saini ya kumuwakilisha kinda huyo wa Manchester United. 

Mawakala wenye majina makubwa kwenyebsoka wamekuwa wakipigana vikumbo kumsaini Rashford mwenye umri wa miaka 18, ambaye kwa sasa anawakilishwa na familia yake.

Familia yake inategemewa kuendelea kudili na madili ya mtoto wao lakini hilo halijawafanya mawakala wengine kujaribu kutaka kufanya kazi na Rashford, huku Roc Nation ikijaribu kutaka kuanza makubaliano na familia ya kinda huyo wa kiingereza. 

  Kampuni hiyo ya Jay Z ina miaka mitatu tangu ilipoanza kazi, mpaka sasa tayari imewasaini wanamichezo kadhaa wa baseball, basketball, na hata ndondi huku mwanasoka Jerome Boateng wa Bayern Munich akiwa mteja wao pekee kwenye soka barani ulaya. 

United wanategemewa kumpa Rashford mkataba mpya mwishoni mwa smimu baada ya kuonyesha kiwango bora msimu huu tangu alipopewa nafasi katika kikosi cha kwanza. 

Rashford na mwaka mmoja katika mkataba wake mpya na sasa anategemea kupata mkataba ambao atakuwa akiingiza  angalau £15,000 kwa wiki. 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>