Luis Suarez yupo njiani kutengeneza historia katika klabu ya FC Barcelona.
Mpaka sasa tayari ametengeneza rekodi ya kuwa mchezaji katika La Liga kufunga magoli manne katika mbili mfululizo. Magoli yake manne dhidi ya Sporting Gijon yanamaanisha mchezaji huyo ameivunja rekodi yake bora ya ufungaji wa magoli ndani ya msimu mmoja.
Kwenye msimu huu mpaka sasa, mshambuliaji huyu wa Uruguay ameshafunga jumla ya magoli 53 katika mechi 49. Takwimu zake zinampeleka kwenye kilele cha msimamo wa wafungaji bora kuelekea kutwaa tuzo ya PICHICHI akiwa na magoli 34, magoli matatu zaidi ya CR7 ambaye wikiendi hii hakucheza, magoli yake 8 katika mechi mbili zilizopita yamemrudisha kwenye kinyang’anyiro cha kugombea kiatu cha dhahabu cha UEFA.
Mpaka sasa, msimu wake bora kabisa ulikuwa msimu wa 2009-10, alipokuwa akicheza Ajax. Msimu huo alifunga jumla ya magoli 49 katika mechi 48, kiasi cha magoli ambacho alikifikia wakati Barca walipoifunga 8-0 Deportivo la Coruna kabla ya wikiendi hii kuja kushinda 6-0 vs Sporting Gijon pale Camp Nou.
Kiwango cha ’Pistolero’ kimekuja kuimarika wakati ambao Barca wametoka kupitia aakati mgumu. Ikiwa ataendelea na moto huu katika mechi 3 za mwisho za msimu basi ataiwezesha timu yake kutwaa ubingwa. Pia huenda akausitisha utawala wa muda wa Cristiano Ronaldo katika tuzo ya PICHICHI japo mwenyewe sio kitu muhimu sana kwake.
Hizi hapa ndio rekodi za ufungaji za msimu za Suarez tangu alipokuja kucheza soka ulaya.
2006/07 (Groningen): 14 goals / 36 games
2007/08 (Ajax): 22 goals / 43 games
2008/09 (Ajax): 28 goals / 43 games
2009/10 (Ajax): 49 goals / 48 games
2010/11 (Ajax/Liverpool): 16 goals / 37 games
2011/12 (Liverpool): 17 goals / 39 games
2012/13 (Liverpool): 30 goals / 40 games
2013/14 (Liverpool): 31 goals / 37 games
2014/15 (FC Barcelona): 25 goals / 43 games
2015/16 (FC Barcelona): 53 goals / 49 games
Takwimu za msimu huu
Liga: 34 goals
Champions: 9 goals
Copa del Rey: 3 goals
Mundial de Clubes: 5 goals
Supercopa de Europa: 1 goal