Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

MAHREZ AMEUPANDA MLIMA KITONGA KWA MATUMAINI SASA NI WAKATI WAKE KUTULIA KIVULINI

$
0
0

Mahrez7

Rirad Mahrez amezaliwa February 21, 1991 ni mchezaji wa soka la kulipwa anayekipiga kwenye klabu ya Leicester City ya England na timu ya taifa ya Algeria kama winger.

Mahrez alianza soka lake kama mchezaji kijana kwenye klabu ya AAS Sarcelles ya nchini Ufaransa. Mwaka 2009 akaanza rasmi kucheza soka la kulipwa alipojiunga na klabu ya Quimper ambako alichea kwa msimu mmoja pekee na kujiunga na klabu ya Le Havre ambayo aliitumikia kwa miaka mitatu ambapo mwanzo alianza kucheza kwenye kikosi cha wachezaji wa akiba na baadaye kuingia kwenye kikosi cha kwanza na kupata nafasi ya kuanza mara kwa mara.

January 2014, Mahrez alijiunga na Leicester City wakati huo ikishiriki ligi daraja la kwanza (Championship) na kukisaidia kikosi hicho kutwaa taji la Football League Championship na kufanikiwa kupanda daraja kucheza Premier League.

Mahrez alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa akiwa na Algeria mwaka 2014 na kuiwakilisha nchi yake kwenye fainali za kombe la dunia (FIFA World Cup)michuano iliyofanyika mwaka 2014 pamoja na ile ya Africa Cup of Nations ya mwaka 2015.

Maisha binafsi

Mahrez amezaliwa Sarcelles Ufaransa baba yake akiwa ni mu-algeria wakati mama yake anamchanganyiko wa Algeria na Morocco. Wakati anakua, maisha yake ya likizo alikuwa anakwenda Algeria, baba yake amezaliwa Beni Snous, wilaya ya Tlemcen.

Wakati akiwa na umri wa miaka 15, baba yake alifariki kwa shambulio la moyo. Mahrez anasema, “sifahamu kama nilianza kuwa makini lakini baada ya kifo cha baba mambo yalianza kwenda vizuri”

Mahrez amemuoa mpenzi wake mwenye asili ya England mwaka 2015.

Safari ya soka inaanza

Kiwango anachokionesha sasa kilianza kuandaliwa kwenye kituo cha AAS Sarcelles alichojiunga nacho mwaka 2004.

Mwaka 2009 akajiunga na Quimper akitokea AAS Sarcelles, akafanikiwa kucheza mechi 22 na kufunga magoli mawili kwenye msimu wake wa kwanza klabuni hapo.

Mwaka 2010 akajiunga na Le Havre, akizipiga chini offer kutoka Paris Saint-Germain na Marseille kutokana na kuvutiwa na mfumo wa Le Havre namna inavyowalea vijana wake. Alicheza kwenye timu ya wachezaji wa akiba kabla ya kupata nafasi ya kucheza mara 60 kwenye kikosi cha kwanza na kufunga magoli 6 kwenye French Ligue 2 tangu mwaka 2011 hadi alipoondoka January 2014.

Aliikosoa Ligue 2 kwa kile alichodai kuwa timu nyingi za ligi hiyo zinacheza soka la kujilinda zaidi zikiwa na lengo la kupata matokeo ya sare tasa kwenye kila mechi.

Mahrez anaanza maisha Leicester City

Alijiunga na Leicester City mwaka 2014 wakati huo ilikuwa inashirik Football League Championship, akiwa amesaini mkataba wa miaka mitatu na nusu. Ndugu na jamaa zake wa karibu walistushwa na uamuzi wake wa kwenda kucheza soka England kutokana na ligi za nchi hiyo kutumia mpira wa nguvu wakiamini aina ya uchezaji wake ingefaa zaidi kama angeenda Hispania.

Mahrez alicheza mechi yake ya kwanza January 25, 2014 akiingia uwanjani dakika ya 79 kuchukua nafasi ya winger Lloyd Dyer kwenye mechi waliyoshinda magoli 2-0 dhidi ya Middlesbrough. Baabda kuingia mara nne kwenye kikosi cha Leicester City akitokea benchi pamoja na kufunga goli lake la kwanza kwenye klabu hiyo likiwa ni goli la kusawazisha dakika 82 dhidi ya Nottingham Forest.

Manager wa Nigel Pearson mwezi February 2014 alitangaza kwamba, alikuwa anafikiria Mahrez alikuwa tarari anatakiwa kuanza kwenye kikosi cha kwanza. Leicester ikamaliza msimu ikiwa bingwa wa Championship na kurejea Premier League kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10.

Ndoto zinatimia Mahrez anaingia kukipiga EPL

Alisaini mkataba mpya wa miaka minne kuichezea Leicester August 2015. August 8, 2015, Mahrez alifunga magoli mawili kwenye mchezo wa ufunguzi wa EPL dhidi ya Sunderland wakati imu yake ikipata ushindi wa nyumbani wa magoli 4-2. Baadaye akatajwa kama mchezaji wa ushindi wa klabu na nahodha Wes Morgan kufuatia kupachika magoli manne kwenye mechi tatu za mwanzo wa msimiu.

Baada ya kufunga magoli manne katika mechi nne za mwanzo wa msimu wa 2025-16, Mahrez alitajwa kuwa mchezaji bora wa mwezi (Premier League Player of the Month.)

Hadi kufikia November 3, 2015 alikuwa amefunga magoli 7 katika mechi 10 za Premier League. Mwezi December Mahrez alipiga hat-trick wakati Leicester ilipoichapa Swanea City kwa magoli 3-0 na kukwea kileleni mwa Premier Leaguena kumfanya afikishe magoli 10 kwenye ligi na kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Algeria kufunga magoli matatu (hat-trick) kwenye Premier Leaue.

Mahrez pamoja na viongo wenzake wa Leicester Marc Albrighton, N’Golo Kante pamoja na Danny Drinkwater wamejizolea sifa lukuki kutokana na uwezo mkubwa waliouonesha huku kocha Claudio Ranieri akimwelezea Mahrez pamoja na Jamie Vardy hawana bei wakati wa majira ya usajili wa dirisha dogo mwezi January.

Umaarufu wa Mahrez unatawala Ulaya

Kufikia January 2016 inadaiwa kuwa, thamani ya ada ya uhamisho ya Mahrez ilikuwa imepanda kutoka £4.5 million hadi £30.1 million na kumuweka kwenye orodha ya wachezaji 50 ghari barani Ulaya.

Mwaka huohuo, umaarufu wa Mahrez kwenye ardhi ya kwao uliifanya Leicester kupata wafuasi wengi sana (mara tatu zaidi ya wale wa Uingereza) kwenye mtandao wao wa facebook.

Saloon ambayo ipo kwenye mji wa Sarcelles alipokuwa ananyoa enzi za utoto wake  ikapata umaarufu mkubwa ambapo kuna mashabiki waliokuwa wakisafiri kutoka Ubelgiji kwenda kunyoa hapo kwa style ambayo anaitumia Mahrez.

Anatwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka EPL

Mwezi April Mahrez alikuwa ni miongoni mwa wachezaji wanne kutoka klabu ya Leicester City waliotajwa kwenye kikosi cha PFA Team of the Year kisha baadaye kutwaa tuzo ya the PFA Player of the Year.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>