Jumapili ya May 8, 2016, kikosi cha Mwadui FC kiliichapa Simba SC bao 1-0 kwenye uwanja wa taifa na kuchochea zaidi moto wa Yanga kutwaa ubingwa wa VPL msimu huu.
Kocha wa Mwadui, Jamhuri Kihwelo alichukua mfano wa kombe na kuitangaza Yanga kuwa ndiyo mabingwa rasmi wa ligi kwa msimu huu mara baada ya mchezo kumalizika.










