
Kadi nyekundu aliyooneshwa mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib inamfanya kukosa mechi zote (mbili) za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu huu pamoja na mchezo wa kwanza wa ligi ya msimu ujao.
Ajib alioneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja ‘straight red card’ baada ya kumchezea vibaya Hassan Kabunda wa Mwadui FC zikiwa zimesalia dakika chache pambano hilo kumalizika.

Kwa mujibu wa sheria na kanuni za mchezo wa soka, mchezaji anayeoneshwa ‘straight red card’, analazimika kutumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu mfululizo.
Ajibu atakosa mechi mbili za mwisho ambazo Simba imebakiza kabla ya kufika tamati ya ligi baadaye mwezi huu, pamoja na mchezo wa kwanza wa ligi msimu ujao. Mechi ambazo Ajib atazikosa ni ule wa Majimaji vs Simba (11-05-2016) na mchezo wa mwisho wa kumaliza ligi ambapo Simba itakuwa ugenini kucheza na Mtibwa Sugar (15-05-2016).
Kwa maana hiyo, Ibrahim Ajib tayari amemaliza msimu wa ligi wa 2015-16.