Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

LITTLE MOZART, MACHO YANAPOTOA MACHOZI NA SURA YENYE TABASAMU

$
0
0

Tom

Na Brian Marian

Kama kuna kiumbe niliyewahi kumshuhudia katika uso wa dunia akileta ladha ya ubunifu ndani ya uwanja basi Tomas Rosicky ni mmoja wapo.

Alikuwa mbunifu wa kupiga pasi zile za autor, hakika
machozi yake, jasho na damu vyote alivipigania katika soka lake ila maisha ya mpira yalimkataa. Wakati mwingine naumia sana napomwona Mozart akiwa ameishia njiani wakati thamani ya miguu yake ilikuwa imejaa virutubisho halisi ndani ya miguu yake.

Hata Edo Kumwembe anajua thamani ya miguu yake, natamani ningekuwa karibu na miguu yako niweze kutoa machozi pembeni yako ndani ya Emirates jioni ya leo. Safari ya mwanadamu wakati mwingine husubiri matumaini ya kile akipiganiacho ili kuweza kumletea wepesi katika mafanikio yake.

Mozart napomwona akitoa machozi, huku sura yake yenye tabasamu likionekana ndani
yake.Walicheka na wewe,walilia na wewe katika kipindi chako chote cha majeruhi yako ndani ya club yako hakika utakumbukwa sana kwa ufundi wako ndani ya uwanja.

Miaka kumi (10) uliyokaa ndani ya Arsenal ulipigana kwa ajili ya timu kuweza kuipa timu thamani yake.Majeruhi (INJURY) ndiyo yaliharibu maisha yako ya soka na kushindwa kushuhudia vingi vilivyopo
ndani ya miguu yako. Ilibidi mwanadamu huyu Mozart akubali kusogea katika uso wa dunia ili dunia iweze kujitegemea katika himaya yake. Hatimaye leo ndiyo hatamu ya miguu yake itakapo
fikia mwisho.

Kila mcheza soka au shabiki wa soka hapa ndipo mahala ambapo machozi huwabubujika ndani ya nyuso zao,
zilizokuwa zimefichwa na tabasamu ndani yake. Hapa ndipo
mahali ambapo akili itakuwa bado inahitaji kucheza,mwili utakuwa
unakataa.

Ndio wakati ambao tutakumbuka mengi mazuri yako ambayo utakuwa umeyafanya katika mchezo wa soka,hapa ndipo mashujaa wengi watakumbukwa. Ulimwona David Beckham, Ronaldo de Lima, Thiery Henry n.k. walitoa machozi yao kwamaana walishajua kile walichokuwa wanakipigania ndiyo kilikuwa kinafika
tamati mbele yao.

Siku nyingine tena pembezoni mwa London mitaa ya Woolwich jioni nyingine tena nilimshuhudia Tomas Rosicky (LITTLE MOZART) akiwaaga mashabiki wake waliompenda katika kipindi chake chote walichokaa naye. Umri wa miaka 35 ni muda sahihi wa yeye kwenda kupumzika na kuupa mkono wa kwaheri mchezo wa
soka.Wakati mwingine nikijaribu kuvuta ubora wa miguu yake bila kuwa na majeruhi ya mara kwa mara.
Imani yangu dhidi yake angekuwa mmoja kati ya mastaa hawa katika ubora wake Iniesta, Cazorla, Pogba, David Silva n.k.

Tatizo changamoto za majeruhi ndiyo zimetunyima kushuhudia ubora wake. Hakika utakuwa shujaa wa wapenda soka na ndani ya familia ya Arsenal kwa ujumla. Bado ninaimani miguu yake inahitaji kucheza soka ila majeruhi ndiyo yameharibu safari yako ya matumaini.

TOMAS ROSICKY (LITTLE MOZART) MACHO YAKE YANAPOTOA MACHOZI, SURA YENYE TABASAMU NDANI YAKE.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>