Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

RONALDO KAWEKA REKODI YA KUTUPIA KAMBANI KWA MIAKA 6

$
0
0

Ronaldo-11

Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli 50 kwenye mashindano yote kwa miaka sita mfululizo baada ya kufunga magoli mawili kwenye mchezo wa Jumamosi wakati Real Madrid ikishinda kwa magoli 2-0 dhidi ya Deportivo La Coruna.

Star huyo wa Ureno alianza kufunga goli la kwanza dakika ya saba ya mchezo huo wa mwisho wa La Liga msimu huu, baadaye akaongeza la pili dakika ya 25 bao ambalo lilikuwa la 51 japo taji la La Liga lilielekea Barcelona.

Magoli hayo Mawili dhidi ya Deportivo La Coruna yalimfanya Ronaldo kufikisha jumla ya magoli 35 kwenye ligi msimu huu huku akiwa amepachika mabao mengine 16 kwenye michuano ya Champions League.

Bado anauwezekano wa kuongeza magoli kutokana na kuwa na mchezo mmoja mkononi May 28 ambapo Real itachuana na Atletico Madrid kwenye fainali ya Champions League itakayochezwa Milan.

Ronaldo ameweza kufunga magoli 50 kila msimu tangu msimu wa 2010-11, ukiwa ni msimu wake wa pili tangu alipojiunga na Real Madrid akitokea Manchester United.

Alifunga magoli 53 msimu huo, kisha 60, 55, na 51 kabla ya kufunga magoli mengi zaidi 61 msimu uliopita.

  1. 2010/11: magoli 54
  2. 2011/12: magoli 60
  3. 2012/13: magoli 55
  4. 2013/14: magoli 51
  5. 2014/15: magoli 61
  6. 2015/16: magoli 51(bado mechi moja).

Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>