Nipo hapa mjini Milan kuhakikisha mdau na msomaji wangu wa shaffihdauda.co.tz haupitwi na tukio hata moja la kimichezo ambalo litajiri hapa kuelekea mchezo wa fainali ya Champions League itakayopigwa kesho kati ya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid kwenye uwanja wa San Siro.
Leo kocha wa Atletico akiwa pamoja na nahodha wake Gabi pamoja na Fernando Torres walikutana na waandishi wa habari kuzungumzia mchezo wao wa kesho, maandalizi na mipango yao dhidi ya Madrid.
Hii ni ripoti yangu fupi niliyokuandalia baada ya kumalizika kwa mkutano huo, angalia video hapa chini.