Baada ya kukamilika kwa michuano ya UEFA Champions League leo nakuletea takwimu na rekodi mbalimbali zilizojitokeza baada ya mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya baina ya Real Madrid na Atletico Madrid.
1• Real Madrid wamefanikiwa kulinda rekodi yao ya kutopoteza mchezo wa fainali wa UEFA Champions League, wakishinda fainali 5 kati ya 5 walizocheza. AC Milan ndio klabu pekee iliyocheza fainali nyingi zaidi – fainali 6, lakini wao wameshinda 3 na wamefungwa 3.
2• Ushindi wa fainali zote 5 wa Madrid umekuja kwenye miaka ambayo namba yake inagawanyika, fainali zao 3 kati ya zote zimekuwa dhidi ya timu za Spain.
3• Madrid sasa wamewazidi wapinzani wao Bsrcelona kama klabu iliyo na mafanikio zaidi katika mfumo wa UEFA Champions League – wakiwa wameshinda makombe matano huku Barca wakishinda 4. Barca wamecheza fainali 5, fainali moja waliyofungwa ilikuwa dhidi ya AC Milan mwaka 1994. ave now overtaken domestic rivals Barcelona
4• Ukiondoa Madrid, klabu nyingine zenye rekodi ya asilimia 100 katika fainali ya UEFA Champions League ni Marseille, Porto na Internazionale.
5• Atlético wameungana na Valencia na Man Utd kuwa klabu pekee kufungwa fainali zaidi ya moja ya UEFA Champions League (wote mara mbili). Waliopoteza kwa mara moja ni Bayer Leverkusen, Monaco na Arsenal.
6• Kwa maana hiyo Diego Simeone anaungana na Sir Alex Ferguson, Hector Cuper kuwa makocha pekee wali owahi kupoteza fainali zaidi ya moja.
7• Zinédine Zidane ndio kocha wa kwanza wa kifaransa kushinda UEFA Champions League. Ufaransa ndio taifa la 8 kutoa kocha mshindi wa UEFA Champions League, Italy na Spain ndio wametoa makocha wengu zaidi – 6 kila mmoja. Ujerumani wanne, na Ureno, Uholanzi, Scotland wametoa makocha wawili wawili, na Belgium wametoa kocha mmoja. Hakuna kocha wa kutoka nje ya ulaya ambaye alishashinda UEFA Champions League.
8• Zidane ndio mchezaji wa pili kuwahi kushinda ubingwa wa UCL – akiwa kocha na mchezaji – baada ya Frank Rijkaard. Pia ndio mchezaji wa kwanza kufunga katika fainali ya ulaya na kushinda akiwa kocha.
9• Fainali 8 kati ya 24 za UEFA Champions League sasa zimeamuliwa katika muda wa ziada na 7 kati ya hizo ziliamuliwa kwa penati. Tano kati ya hizo ziliisha 1-1, ikiwemo fainali ya mwaka 2001 ya Valencia vs Bayern.
10• Matokeo ya 1-1 yapo sambamba na matokeo ya 2-1 ndio matokeo yaliyotokea mara nyingi kwenye fainali (mara 5).
11• Antoine Griezmann ni mchezaji wa nne kukosa penati katika fainali ya UEFA Champions League (ukiondoa changamoto ya mikwaju ya penati) – Penati ya kwanza kukoswa kwenye fainali ya Champions League ilikuwa ndanj ya Milan, San Siro, wakati Mehmet Scholl alipofeli kufunga penati katika mchezo Bayern v Valencia in 2001.
13• Toni Kroos ndio mchezaji wa 13 kuwahi kushinda UEFA Champions League na klabu zaidi ya moja – akiwa na Madrid na Bayern 2013.
14• Sergio Ramos ni mchezaji wa tano kufunga katika fainali ya UEFA Champions League na amekuwa beki wa kwanza kufunga idadi hiyo, wengine waliofanya hivyo ni Raúl González, Samuel Eto’o, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
15• Yannick Carrasco ndio mchezaji wa kwanza wa Belgium kufunga goli katika UEFA Champions League. Wachezaji 20 kutoka mataifa mbalimbali wamefanikiwa kufunga katika fainali. Spain bwanaongoza kwa kutoa wafungaji 10. Hakujawahi kutokea mfungaji wa kujifunga katika fainali ya UCL.