Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

TOP 6 YA WACHEZAJI WANAOMILIKI MAGARI YA KIFAHARI BAADA YA RONALDO KUSHUSHA BUGGATTI VEYRON MPYA

$
0
0

Ronaldo's Bugatti

Soka ni moja ya michezo maarufu zaidi ulimwenguni ambapo wachezaji huvuna mamilioni ya fedha. Kutokana na hali hiyo wachezaji humiliki mali nyingi yakiwemo magari ya kifahari ambayo hutokana na pesa nyingi wanazoingiza.

  1. Neymar : Audi R8 GT

Bei : euro 169,130

Nyota huyu wa Barcelona ni moja ya wachezaji wanaoingiza pesa nyingi kwa sasa na kumiliki magari ya kifahari! moja ya magari hayo ni Audi R8 GT!

  1. Zlatan Ibrahimović : Porsche 918 Spyder

Bei : euro 616,500

Mchezaji huyu wa zamani wa PSG na Sweden anassemekana kuwa na majivuno ya hali ya juu kutokana na majibu yake ambayo hutoa kwa waandishi. Alikuwa ndio mchezaji mwenye gharama kubwa klabuni hapo na kumiliki gari lenye thamani kubwa zaidi ya wenzake aina ya Porsche 918 Spyder.

  1. Samuel Eto’o : Bugatti Veyron

Bei : euro 1,168,786

Mchezaji huyu wa kimataifa wa Cameroon ni moja ya wachezaji matajiri zaidi Afrika na ndio maana si ajabu kumwona akiendesha gari la thamani kuliko hata wachezaji wengi maarufu ulimwenguni aina ya Bugatti Veyron.

  1. Karim Benzema: Bugatti Veyron

Bei : euro 1,168,786

Mfaransa huyu ni moja ya wachezaji wanaoishi maisha ya kifahari ulimwenguni. Amekuwa mchezaji tegemeo wa Real Madrid kwa muda mrefu sasa. Anamiliki Bugatti Veyron, ambalo alinunua mwaka jana.

  1. Cristiano Ronaldo : Bugatti Veyron

Bei: euro 1,168,786

Cristiano Ronaldo kwa sasa tunaweza kusema ndiyo mchezaji anayeongoza kwa kuoenda maisha ya kifahari. Anamiliki magari 19, yakiwemo Lamborghini Aventador LP 700-4, BMW M6, Bentley Continental GTC, na Ferrari 599 GTB Fiorano. Hii ni picha ya aliyepigwa wakati akiendesha Bugatti Veyron yake.

  1. Buggatti Veyron : Bugatti Veyron 16.4 Grand Sport Vitesse

Bei : euro 1,288,465

Portugal wamebeba ndoo ya Euro 2016 hivi juzu-juzi, na naodha wao Cristiano Ronaldo akaamua kujizawadia gari mpya aina ya Bugatti Veyron 16.4 Grand Sport Vitesse ili kujipongeza na ubingwa huo. Gari hilo linagharimu dola mil 1.7 na lina uwezo wa kwenda maili 255 kwa saa.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles