Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

VIGEZO 9 VINAVYOZINGATIWA KUPANGA BEI YA MCHEZAJI

$
0
0

Pogba- Man U

Na Mahmoud Rajab

Miaka ya hivi karibuni tumeona mchezo wa soka duniani ukivamiwa na matumizi makubwa ya fedha hasa katika masuala ya usajili wa wachezaji.

Mwenendo wa usajili katika mchezo wa soka unazidi kushangaza ulimwengu huku bei ya wachezaji ikizidi kuwa ya ajabu zaidi. Unaangalia kwa mfano mchezaji kama Anthony Martial ambaye alinunuliwa kutoka AS Monaco kuja Man United kwa paundi ml 38. Akiwa na umri wa miaka 18 tu alinunuliwa kwa pesa ndefu huku akiwa bado hajathibitisha ubora wake nje ya Ufaransa. Je, ingekuwaje kama angeshindwa kuonesha makali kwenye ligi ya EPL ilhali amenunuliwa kwa pesa nyingi kiasi hicho.

Ile tunasema Man United walicheza mchezo wa ‘pata-potea’

Na sasa tena tunaendelea kusikia taarifa juu ya kiasi ambacho Pogba anatajwa kuuzwa. Juventus wamesema wanataka zaidi ya euro mil 100, je, Pogba anasathili kuuzwa kwa pesa nyingi kiasi hicho ukilinganisha na uwezo wake. Hii inaleta maswali mengi sana; ni namna gani mameneja wa soka wanapanga thamani ya bei za wachezaji?

Je, wanafuata takwimu za Opta kupanga bei za wachezaji? Wana kipimo sahihi cha kupima thamani ya gharama za wachezaji? Wana kipimo cha kupanga thamani ya mchezaji kadri anavyokuwa hatua kwa hatua? Kwa kiasi kikubwa, suala hili linachukuliwa kimtazamo zaidi na kuangalia historia. Tunasikia masuala mbalimbali juu ya upandaji thamani usio na mpangalio kwenye soko la usajili hasa ukipandikizwa kwa kiasi kikubwa na Real Madrid, Barcelona, Manchester City, PSG na hata Chelsea ambao ndio watumiaji wa fedha nyingi kwenye usajili.

Wakati fulani Michael Owen alidhihakiwa na mashabiki nchini Marekani kwa kitendo chake cha kuchapisha vipeperushi ili kujaribu kujiuza uza kipaji chake, lakini kwa kutumia aina hiyo ya marketing kusingekuwa na uwezekano wa jipya lolote kutokea katika tasnia ya michezo nchini Marekani ambapo mara nyingi wao wanaenda zaidi na takwimu.

Inatakiwa ifahamike wazi kwamba aina ya michezo ya nchini Marekani kama vile basketball na American Football, ni rahisi zaidi kufanya tathmini ukilinganisha na mchezo wa soka ambapo ni vigumu sana kuangalia thamani ya mchezaji kwa kuangalia takwimu.

Wakati aliyekuwa kocha wa Man United wakati huo Sir Alex Ferguson alipagawishwa na rekodi nzuri ya nyuma ya Owen na kuamua kumchukua, lakini mtazamo wa makocha wengi wa Marekani ni kwamba; Owen kwa wakati huo alikosa ‘mobility’ na ‘movement’ kama ilivyokuwa kwa Torres na. Lakini Ferguson alimchukua Owen kwa kuwa alikuwa hana risk kubwa kwa sababu alikuwa ni mchezaji huru. Hakuwagharimu United fedha yoyote isipokuwa ya kumlipa mshahara tu na isingekuwa kikwazo kwa mchezaji mwingine wa nafasi ya Owen kutokana na uwepo wake.

Kwa upande wa michezo ya Marekani, ili kupandisha thamani ya soko la kisasa (mishahara na pesa za usajili), wanaegemea zaidi kwenye historia, hali ambayo inaendana na masuala ya kisheria kwa upande wao. Mfumo wa michezo wa USA haujawa mmoja (haujaunganishwa), na wachezaji ndio wanatakiwa kuendesha soko la mpira. Lakini bahati mbaya kwa sasa timu kama Real Madrid, Manchester City, PSG na nyinginezo zenye matumizi makubwa ya fedha kwenye usali zimekuwa zikiendesha soko la usajili wa wachezaji.

Wakati huo Sir Alex Ferguson akiwa kocha wa Man United na Arsene Wenger wa Arsenal walijipembua na kusema kwamba wao wasingejihusisha na aina hiyo ya soko la usajili ambalo limekosa uhalisia wa thamani ya wachezaji.

Ni namna gani wakala mkongwe wa wachezaji nchini Marekani Scott Boras angepambana na aina hii ya uhamisho? Kutokana na namna ambavyo Boras anavyofahamika kuwa na misimamo yake mikali ambayo inapingana na  ile iliyoko vilabu vya Italy na Uhispania ambapo marais wa vilabu ndio huamua juu ya masuala yote ya uhamisho wa wachezaji bila kuwafahamisha makocha, na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa upande wa Abramovich na Chelsea yake tangu aliposhika hatamu kwenye klabu hiyo. Walau kwa sasa anaonekana kupunguza lakini kwa kiasi kikubwa alikuwa akiwasajilia makocha wachezaji bila ridhaa zao. Kwa mfano wakati kocha Carlo Ancelotti alipokuwa Chelsea alimsajilia wachezaji kama Fernando Torres na Shevchenko na hatimaye wachezaji hao kutofanya vizuri.

Siku hizi mawakala wanapambana kwa kiasi kikubwa kwa ajili ya kujiingizia kipato kikubwa, itakuwaje kama vilabu mbalimbali vitaamua kufuata mfumo wa Kiamerika kwamba mchezaji anapaswa kumlipa wakala? Ni sajili chache za aina hiyo zingefanyika kwa sababu wachezaji wangekuwa wanaogopa kuingia gharama kubwa, Kwanini klabu imlipe wakala kuvunja mkataba huku mchezaji akiwa halipi chochote.?

Kwa mfano Ronaldo na Kaka, hawa ni wachezaji wawili waliogharimu pesa nyingi zaidi duniani kwenye uhamisho wakati huo. Ronaldo aligharimu paundi mil 80 na Kaka paundi mil 56. Kwanini? Ngoja tuangalie kwa ufupi tu takwimu hii:

Kulikuwa hakuna tofauti kubwa mbali na bei waliyonunuliwa na umri walionao japokuwa Ronaldo alikuwa na uwino mzuri wa magoli kuliko Kaka. Sasa je, hiyo tofauti ya paundi mil 24 ni kwa sababu ya umri? hakika si kweli na pengine kuna vigezo vya ziada ambavyo vilisababisha Real Madrid kuweka tofauti ya paundi mil 24 kwa wachezaji wenye tofauti ya miaka 3.

Sasa hapa pengine kuna sababu za ziada ambazo mameneja, wamiliki na waangalizi huzitupia jicho kupanga thamani ya mchezaji.

1) Hadhi ya kikosi

Hapa maana yake ni kwamba mchezaji hawezi kutenganishwa na timu.

Mchezaji huyu ni muhimu sana katika kikosi cha kwanza cha timu.

Mchezaji huyu ana thamani kubwa sana kwenye kikosi cha timu husika

Mchezaji huyu ni ‘backup’ ya kikosi cha kwanza

2) Umri

16-20

21-25

26-30

31-35

36+

Kwa kuzingatia thamani ya mchezaji kulingana na umri, inawezekana kudhibiti ada za uhamisho wa wachezaji? Kwamba mchezaji mwenye umri mdogo thamani yake inakuwa kubwa zaidi, kwa mfano kuanzia miaka 21-25, vivyo hivyo na kwenye suala la hadhi ya kikosi…timu ama kikosi chenye hadhi kubwa basi lazima thamani yake iwe kubwa zaidi.

3) Kipaji

Wachezaji wote wawe wamecheza michezo ya Ligi isiyopungua 20

Aina A- Opta Statistics itambue kwamba wachezaji wameperform kwa walau 10% ya maeneo yao wanayocheza.

Aina B- Opta Statistics itambue kama mchezaji yuko kwenye walau 25% ya wchezaji wanaocheza vizuri kwenye nafasi zao

Aina C- Opta Statistics itambue kama mchezaji yuko kwenye 40% ya wachezaji wanaocheza vizuri kwenye nafasi zao.

Aina D- Opta Statistics zitambue kama mcheza yupo kwenye top 60%  ya wachezaji wanaocheza vizuri kwenye nafasi zao.

Namna hii ya kujua ku-regulate takwimu za soka inaweza isiwe sahihi kwa asilimia kubwa. Kwa mfano, namna gani unaweza kumjua kipa bora?Buffon, De Gea, Petr Cech ama Manuel Neuer anaweza kucheza klabu kama Sunderland na kuruhusu magoli kama Vito Mannone au Jordan Pickford. Tunawezaji kuwatambua mawinga bora?wapigaji wazuri wa pasi za mwisho? Sio lazima sana ila mchango wa mchezaji kwenye mchezo husika ni muhimu. Hili ni eneo ambalo wataalamu wa masuala ya soka na watafiti wanaweza kukubaliana na Opta. Kwenye mpira wa baseball kuna formula nyingi za kufanyia kazi ili kutambua mchango halisi wa mchezaji na hivyo ndivyo Opta inavyoweza kufanya kama ambavyo saber-metrics hufanya.

4) Kigezo cha ligi

Kama ilivyo kwa kesi ya Kiatu cha Dhahabu Barani Ulaya (Tuzo ya Mfungaji Bora Ulaya), tunaweza kuchukua kigezo cha kipaji kujumuisha na kigezo cha ubora wa ligi.  Swansea kwa mfano, inaweza ikawa haina shauku ama mshawasho wa kulipa kiasi cha paundi mil 12 kumnunua mchezaji wa Kibrazil ambaye anacheza soka kwenye ligi ya Uholanzi

5) Nafasi zenye soko kubwa

Viungo washambuliaji, wa kati na pembeni na washambuliaji wana soko kubwa sana kwenye soka. Suala la kuwapa kisogo au kutowatahmini mabeki si zuri kwani soka ni mchezo unaohusisha timu nzima na thamani ya wachezaji wote lazima iwe sawa. Nafasi za mabeki zimekuwa hazipewi kipaumbele sana katika soko la wachezaji. Tumeshuhudia mabeki wachache sana wakipewa thamani kubwa kwenye soko la usajili, kwa mfano: David Luiz, Dani Alves, Allesandro Nesta, Rio Ferdinand Carvalho bila ya kusahau beki aliyesajiliwa na Man United hivi karibuni Eric Baily

6)Uwezo wa kuendana na kasi ya ligi (Adaptability)

Kuna wachezaji kutoka baadhi ya mataifa huwa wanapata shida sana kuendana na kasi ya ligi ya England. Wachezaji wengi kutoka Amerika Kusini wamekuwa wakipata wakati mgumu kuendana na soka la Kiingereza lakini hilo sasa ni juu ya mameneja kuwapa mbinu wachezaji hao ili kuendana na kasi ya ligi na sio kuwaacha wahangaike wenyewe. Kumekuwa na tatizo la Wabrazil wengi kushindwa kufanya vizuri kunako ligi ya England kwa mfano Robinho, Jo, Elano na Paulinho, wote hawa wameshindwa. Ni wachache tu kama Fernando na Fernandinho wa Man City ndio ambao wamjitahidi kufanya vyema.

7) Kushuka thamani

Hili ni eneo ambalo makocha wengi wanakuwa na makini sana. Licha ya kwamba kuna baadhi huwa wanaingia choo cha kike. Kwa mfano kuna makocha kadhaa ambao wamewahi kulipa pesa nyingi kuliko thamani ya wachezaji. Kwa mfano Mark Hughes na Benitez imeshwahi kuwatokea kwa wachezaji kama Roque Santa Cruz, Gareth Barry, Robbie Keane, vile vile Chelsea imewahi kuwatokea kwa Shevchenko ambaye alinunuliwa kwa pesa nyingi (paundi mil 30) wakati umri ukiwa umeenda (miaka 30), wakati Makelele alisajiliwa kwa paundi mil 16 akiwa na umri huo huo.

Lakini kuna baadhi ya mameneja ambao wako na walikuwa makini sana kwenye suala la ununuzi wa wachezaji. Kwa mfano Arsene Wenger na kocha wa zamani wa Man United Sir Alex Ferguson ni mameneja ambao ni wagumu sana kutoa pesa nyingi kwa mchezaji ambaye wanahisi hafiki thamani husika. Arsene Wenger kwa miaka kadhaa alikuwa akiuza wachezaji ambao ubora wao unakaribia kuisha kwa thamani ya juu ili apate faida kubwa. Kwa mfano Robin Van Persie, Thierry Henry na wengine wengi.

8) Haki ya Matangazo (Image Rights)

Hili pia ni suala muhimu sana kwenye usajili wa wachezaji. Vilabu vingi vimekuwa vikitoa pesa nyingi kwa ajili ya usajili wa wachezaji na kunufaika na mauzo ya jezi. Kwa mfano timu kama Real Madrid imefanya hivyo kwa wachezaji kama James Rodriguez, Gareth Bale na Cristiano Ronaldo. Wametumia mamilioni ya euro kuwasajili lakini zote zimerudi kupitia mauzo ya jezi na haki nyingine zinazotokana na usajili wa mchezaji.

9) Hadhi ya Mchezaji/Wachezaji kwenye timu (Ukubwa wa jina la mchezaji)

Hii ni pale klabu inapokuwa inanufaika na na Nyanja zote za kibiashara kama vile ongezekao la mauzo ya tiketi, mikataba minono ya haki za matangazo ya urushaji matangazo, pre-season tour na kadhalika. Kwa sasa tunaweza kusema wachezaji kama Lionel Messi,  Cristiano Ronaldo pengine na Neymar ndio wana impact kubwa kwenye Nyanja hii kwani popote vilabu vyao vinapokwenda mathalan kwenye pre-season tour watu wengi hununua jezi za timu,vile vile kwenye suala la watu kuingia uwanjani kwa sababu ya kuwaangalia wao ni kigezo kingine cha ongezeko la mauzo ya tiketi. Kwa sasa Messi, Ronaldo na Neymar ndio wachezai wanaoongoza kwa kiasi kikubwa kwenye masuala ya mikataba ya kibishara.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>