Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

JUMA ABDUL MCHEZAJI BORA VPL 2015/16

$
0
0

IMG_0389

Usiku wa Jumapili Julai 16 zimetolewa tuzo kwa timu, wachezaji na makocha kutokana na kufanya vizuri kwenye ligi kuu Tanzania bara katika msimu wa 2015/16 ambao ulimalizika mwezi Mei kwa Yanga kuibuka mabingwa wa ligi hiyo na kutwaa taji lao kwa mara ya 26 katika historia.

Tuzo hizo ni mabingwa, makamu bingwa, mshindi wa tatu, mshindi wa nne, timu yenye nidhamu, mfungaji bora, mchezaji bora wa Ligi, kipa bora, kocha bora, mchezaji bora chipukizi, mchezaji bora wa kigeni, goli bora la msimu na mwamuzi bora.

Tuzo zilitolewa kwa washindi kama ifuatavyo;

  1. Mshindi wa nne: Tanzania Prisons

IMG_0308

2. Mshindi wa tatu: Simba SC

IMG_0310

3. Mshindi wa pili: Azam FC

IMG_0313

4. Bingwa wa ligi kuu 215/16: Yanga SC

IMG_0318

5. Mfungaji bora wa msimu wa 2015-16: Amis Tambwe-alifunga magoli 21 magoli mawili mbele ya mpinzani wake Hamisi Kiiza aliyefunga magoli 19

IMG_03236. Timu yenye nidhamu: Mtibwa Sugar

IMG_0333

  1. Mwamuzi bora ni Ngole Mwangole

IMG_0336

Walioingia katika kinyang’anyiro hicho ni Anthony Kayombo, Ngole Mwangole na Rajab Mrope.

  1. Goli bora la msimu: tuzo imekwenda kwa Ibrahimu Ajib (Simba)

IMG_0357

Ajib alikuwa akipambana na Amis Tambwe (Yanga) katika kuwania tuzo ya goli bora la msimu 2015-16.

  1. Golikipa bora ni Aishi Manula (Azam FC)

IMG_0356

Majina yaliyopendekezwa kuwania tuzo hiyo ni Aishi Manula (Azam)Beno Kakolanya (Tanzania Prisons) na Deogratius Munishi (Yanga).

  1. Kocha bora wapo Hans Van Pluijm (Yanga)

IMG_0344

Waliokuwa wakipambana kuwania tuzo ya kocha bora wa msimu uliopita ni Hans Van Pluijm (Yanga), Mecky Maxime (Mtibwa Sugar) na Salum Mayanga (Tanzania Prisons).

  1. Mchezaji bora wa kigeni ni Thabani Kamusoko (Yanga)

IMG_0363

Waliongia kwenye orodha ya tuzo ya mchezaji bora wa kigeni ni Donald Ngoma (Yanga), Thabani Kamusoko (Yanga) na Vincent Agban (Simba).

  1. Mchezaji bora chipukizi ni Mohamed Hussein (Simba)

IMG_0381

Waliokuwa wakiwania tuzo hiyo ni Farid Mussa (Azam), Mohamed Hussein (Simba), Mzamiru Yasin (Mtibwa Sugar) na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar).

  1. Mchezaji bora wa Ligi ni Juma Abdul (Yanga)

IMG_0389

Waliopendekezwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi walikuwa ni Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Juma Abdul (Yanga) na Mohamed Hussein (Simba).

IMG_0427


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>