
Wadau wa soka la Bongo walikusanyika usiku wa Julai 16 kwa ajili ya kushuhudia ugawaji wa tuzo mbalimbali kwa wachezaji, makocha na vilabu vilivyofanya vizuri katika ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2015/16.
Tuzo hizo zilikwenda kwa walengwa na hatimaye kukamilisha zoezi hilo ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu baada ya kuchelewa kutokana na sababu za hapa na pale.
Kuna matukio mengi yalijiri katika ugawaji wa tuzo hizo, lakini hapa nakupa picha kadhaa ushuhudie mambo muhimu yalivyokuwa.
















