Mchezaji ambae ameshatupia magoli 10 kwenye mechi zake tatu zilizopita ana kila sababu ya kuwa na furaha kwa wakati huu. Robert akiwa na wachezaji wenzake wa Bayern Munich wamekusanyika pamoja kwenye festival moja ya beer huko Ujerumani inayoitwa Oktoberfest.
Jana usiku Bayern ilishinda 5-0 baada ya kuifunga Dinamo Zagreb kwenye mechi ya Champions League. Kwenye festival hii wachezaji hujiachia na glass kubwa iliyojaa bia wakiwa na wapenzi wao.