Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

KIMWAGA AING’ARISHA SIMBA

$
0
0
Mshambuliaji wa Simba aliyesajiliwa kwa mkopo toka klabu ya Azam FC Joseph Kimwaga akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya Stand United

Mshambuliaji wa Simba aliyesajiliwa kwa mkopo toka klabu ya Azam FC Joseph Kimwaga akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya Stand United

Mshambuliaji mpya wa Simba aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka klabu ya Azam FC leo ameing’arisha Simba baada ya kuifungia goli pekee kwenye mchezo wa leo dhidi ya Stand United ya mjini Shinyanga kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa.

Kimwaga aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Said Ndemla alifunga goli hilo muda mfupi baada ya kuingia baada ya kuichambua safu ya ulinzi ya Stand kisha kubaki yeye na nyavu na kufunga goli hilo kwa urahisi.

Mfungaji wa goli la Simba Joseph Kimwaga akishangilia na wachezaji wenzake wa Simba SC

Mfungaji wa goli la Simba Joseph Kimwaga akishangilia na wachezaji wenzake wa Simba SC

Licha ya Simba kutawala mchezo kwa asilimia nyingi lakini bado walishindwa kupachika mipira kambani kutokana na nafasi nyingi walizotengeneza. 

Stand United walicheza vizuri na kuwazuia washambuliaji wa Simba kitu ambacho kiliongeza presha kubwa kwa wekundu hao ambao walilala kwa bao 2-0 kwenye mchezo uliopita dhidi ya watani zao Yanga.

Hassan Kessy (kulia) akimtoka mchezaji wa Stand United kwenye mchezo wao uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa

Hassan Kessy (kulia) akimtoka mchezaji wa Stand United kwenye mchezo wao uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa

Kimwaga aliisumbua safu ya ulinzi ya Stand United tofauti na mchezaji Boniphace Maganga ambaye leo alianza kama mshambuliaji wa kati wa Simba kutokana na kukosekana kwa Hamisi Kiiza na nahodha wa timu hiyo Mussa Mgosi ambao wamekuwa wakianzishwa kama washambuliaji kwenye kikosi hicho.

Kocha mkuu wa Stand Leiwig leo hakuwepo kwenye benchi la timu yake kutokana na kutumikia adhabu ya kufungiwa mechi mbili.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>