
Wachezaji wa Yanga Malimi Busungu (katikati), Amis Tambwe (kushoto) na Haji Mwinyi (kulia) wakishangilia goli lililofungwa na Malimi Busungu wakati Yanga ikicheza dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri mijini Morogoro
Timu ya Yanga imeendeleza ubabe kwenye ligi kuu Tanzania bara baada ya leo kuitandika timu ya Mtibwa Sugar kwa goli 2-0 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Bao la kwanza la Yanga lilifungwa dakika ya 58 kipindi cha pili mfungaji akiwa ni Malimi Busungu baada ya baada ya beki wa Mtibwa Andrew Vicent kumrudishia mpira golikipa wake Said Mohamed lakini Busungu akainasa pasi hiyo na kupachika bao.

Donald Ngoma wa Yanga (kulia) akijaribu kuwatoka wachezaji wa Mtibwa Sugar wakati wa mchezo wao uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri
Wakati mpira ukitarajiwa kumalizika wakati wowote, Yanga waliandika goli la pili lililofungwa na mshambuliaji Donald Ngoma kufuatia golikipa Said Mohamed kutema shuti ambalo lilipigwa na Simon Msuva.