Kocha Mkuu wa Yanga amesema wanatakiwa kujiandaa vizuri kuelekea mchezo wao dhidi ya Azam kwasababu kila timu inapocheza na Yanga inajipanga vizuri kwa lengo la kuwafunga mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara.
Yanga itapambana na Azam FC October 16 wakati huo Azam ikiwa kwenye wakati mbaya ambapo imecheza mechi nne bila kupata ushindi. Kati ya hizo, imefungwa mechi tatu na kutoka sare mara moja.
“Tunatakiwa kujiandaa vizuri kwasababu kila timu inajiandaa kwa asilimia 100 au zaidi, kila mtu anataka kuwafunga mabingwa watetezi hilo tunalifahamu na tunatarajia hilo kwenye kila mechi,” hayo ni maneno ya kocha Mkuu wa Yanga Hans van Pluijm akijibu swali kuhusu mechi yao ijayo dhidi ya Azam FC.
Leo October 12, Pluijm amekiongoza kikosi chake kupata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar wakati Azam imechezea kipigo ugenini dhidi ya Stand United ya Shinyanga.