Kwa wiki nne mfululizo tumekuwa tukikuwekea hapa baadhi ya Makala kuhusiana na simu ya Huawei Y360 inayouzwa kwa ushirikiano kati ya makampuni nguli ya mawasiliano nchini, Tigo na Huawei.
Sababu kubwa ya kuweka Makala hizo, tulikuwa tukifuatilia aina mpya ya kufanya matangazo ambayo inatumika. Makampuni haya yamekua yakitumia kurasa za Facebook, Twitter, Blogs na mitandao mingine mingi kuwafikia watu wengi zaidi.
Mpaka sasa Huawei Y360 kupitia njia hii imewafikia watu wengi zaidi? Jibu ni ndiyo. Katika ufuatiliaji wetu, tumegundua kuwa idadi ya watumiaji wa Huawei Y360 imeongezeka sana baada ya makampuni haya kutumia mitandao hii.
Tulipouliza wengi wa wateja wake, majibu yalikua kupita mitandao waliweza kupata ushauri wa kitaalamu ambao wengi wa wataalamu hao walishauri kunununa simu za mkononi za Huawei Y360. Faida walizoelezwa ni hizi;
Moja simu hizi zinauzwa kwenye maduka ya Tigo hivyo mnunuzi anakuwa na uhakika kuwa ananunua simu original zikiwa na waranti yam waka mmoja. Mbili bei yake ni nafuu ambayo ni Shilingi 160,000 pekee. Tatu kila mteja anayenunua, anarudishiwa pesa yote aliyonunulia kama vifurushi.
Hivyo basi kama makampuni makubwa yanatumia mitandao, nawe kama mfanyabiashara mdogo mdogo ni wakati sasa wa kuwaza kutumia njia hii kuwafikia watu wengi zaidi.