Wakiwa na kikosi chao cha kizazi cha dhahabu, Uholanzi waliisumbua Spain, timu inayotajwa kuwa bora katika historia ya timu za taifa, mpaka kufikia extra time katika fainali ya kombe la dunia mwaka 2010. Mwaka 2014, walifika mpaka nusu fainali na kucheza dhidi ya Argentina na mikwaju ya penati ikawahukumu, wakaenda kwenye mchezo wa kutafuta mshindi wa 3 na wakamuadhibu mwenyeji Brazil. 2016, hawatokuwemo hata kwenye michuano ya Euro.
Kutanuliwa kwa ukubwa wa michuano kulitegemewa kufanya jambo hilo lisiwezekane. Zamani mfumo wa Euro ulikuwa viongozi wa makundi 16 walikuwa wanafuzu moja kwa moja wakati washindi wa pili ilibidi wacheze kwenye mechi za play off ili kupata nafasi. Hivi sasa mfumo mpya timu 24 zinafuzu moja kwa moja – washindi wa kwanza na wa pili wa kundi, wakati mshindi wa 3 anaenda kucheza mechi za play off. Uholanzi wenyewe wamemaliza mechi za kufuzu wakishika nafasi ya 4 kwenye kundi lao hivyo hawatopata hata nafasi ya kuingilia mlango wa uani kwenye michuano ijayo ya Euro mwakani.
Nini kimeisibu timu hii – hizi ni sababu 3 kuu.
1. Kundi A Lilikuwa na Timu nzuri sana
Hakuna anayedhani kwamba Czech Republic, Turkey na Iceland ni timu ambazo zinaweza kuviadhibu vigogo. Inategemeaa na kundi lipi wanawekwa, yoyote kati hizo timu angeweza kumaliza katika nafasi ya pili na kufuzu mojakwa moja bila kupitia play off. Lakini wote wakapangwa pamoja, wakaongezewa na Uholanzi, kumaanisha kwamba moja ya timu hizo nzuri angeikosa michuano ijayo ya Euro kwa kukosa nafasi katika top3 ya kundi.
Hakuna aliyefikiria timu hiyo ingeweza kuwa Uholanzi, lakini timu zote zilikuwa nzuri, zote zina mastaa wao ambao wapo kwenye kundi la wachezaji wenye miaka ya 20+. Iceland wamekuwa wakiboreka taratibu katika miaka ya hivi karibuni na kwa bahati kidogo tu wakaikosa michuano ya kombe la dunia, wakati Czech na Uturuki wanachukulia poa na viwango vya UEFA baada ya kupitia kipindi cha mpito baada ya vizazi vyao vya dhahabu kuanza kupotea. Timu hizi zote mbili sasa zimemaliza kipindi cha mpito na sasa wana wachezaji makinda ambao wanapewa nafasi na sasa wanaelekea katika kilele cha viwango vyao.
Angalia vizuri vikosi vya timu zote tatu (Turkey, Czech Republic, Iceland) — vikosi vyao vinaundwa kwa kiasi kikubwa na wana wachezaji wenye umri wa miaka 20-25.
Wote walikuwa na utayari wa kupambana na kuwashinda hata vigogo, na UEFA wakawapanga pamoja. Hili lilikuwa jambo baya kwa Uholanzi kuwekwa nao kwenye kundi moja.
2. Mastaa wakubwa wa Uholanzi wanaelekea uzeeni
Arjen Robben, Wesley Sneijder, Robin van Persie, Klaas-Jan Huntelaar na Nigel de Jong wote wanaelekea mwisho wa maisha yao ya kucheza sokala ushindani. Robben hakucheza mechi vs Uturuki kutokana na majeruhi, de Jong amekuwa akitemwa na wengineo umri umezidi kuwaondo mchezoni. Hililinatokea sana katika timu za taifa – wakati kizazi cha dhahabu kinaanza kuzeeka na wanashindwa kupata namna nzuri ya kuingiza kizazi kipya huku wakipunguza cha zamani.
Kwa upande wa Uholanzi wanafanya kazi nzuri kuingiza vipaji vipya katika timu yao, lakini kuna pengo kubwa la vipaji vya kizazi kinachoondoka na kile kipya.
3. Udhaifu wa mbinu katika safu ya kiungo
Katika miaka ya 1970s, wadachi walicheza soka lilowavutia watu wengi sana. Wakiongozwa na Johan Cruyff mbele, walikuwa wakipiga pasi na kuhamisha mpira vizuri mno. Wakati Wadachi hao hao wakiwa na kizazi chao kipya walipofika mpaka fainali ya Kombe la dunia wakicheza staili ya kibabe, wakiongozwa na viungo watata De Jong na Mark Van Bommel, walisemwa sana kwa aina ya soka walilokuwa wakicheza – Cruyff akisema wanautukanisha utamaduni wa soka la kiholanzi ili kushinda kombe.
Van Bommel alistaafu na hakupatikana mbadala wake sahihi, lakini de Jong akaendelea kuwepo na kuunda safu ya kiungo iliyojazwa na viungo washambuliaji na mawinga. Majeruhi na kutokuwa kwenye fomu kumemuondoa kikosini. Louis van Gaal alikuwa akimchezesha nyuma ya safu ya kiungo ya mtindo wa ‘Diamond’ katika kombe la dunia 2014, lakini Guus Hiddink – ambaye alitimuliwa miezi kadhaa iliyopita na Boss mpya Danny Blind waliamua kutumia mfumo wa kuweka wachezaji wachache kwenye safu ya kiungo, wakicheza mfumo wa 4-3-3 au 4-2-3-1 wakati wote wa mechi za kufuzu. Hawakuwa na wachezaji sahihi na hivyo wamefeli.
Katika mechi ya Wadachi dhidi ya Uturuki, Sneijder — kiungo mchezeshaji ambaye ameshavuka kilele cha kiwango chake alicheza sana katika ulinzi – akilindwa na Daley Blind na Davy Klaassen. Blind ni aina ya wanasoka viraka – ambaye amecheza kwa muda mrefu kwenye ulinzi wa beki wa kushoto, lakini anaweza kama beki wa kati au kiungo. Klaassen ni kiungo mshambuliaji. Wote wawili hawajawahi kucheza kwa muda mrefu kwenye safu ya kiungo ya wachezaji wawili, kwa sababu sio viungo wa kati halisi. Mpaka kufikia sasa kwenye maisha yake ya soka, Sneijder sio mchezaji wa kumuamini tena labda mpaka umpange na viungo wawili mahiri wa ukabaji. Kwa aina ya viungo ya Blind na Klaassen lazima upate madhara hata kama timu itacheza na Messi mbele yao.
Katika mechi dhidi ya Uturuki, kocha Danny Blind alianzisha kikosi dhaifu, na ilichukua dakika 7 tu kw Uturuki kutumia madhaifu ya kikosi cha wadachi.
Beki wa kati Left Stefan de Vrij alipotea kabisa kwenye hili goli – hakufanya majukumu yake kama ilivyotakiwa – lakini halikuwa kosa lake moja kwa moja. Sehemu ya kati ya kiungo cha Wadachi kiliwafelisha wenzao. **************************
Namna ya kujipanga kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la dunia 2018.
Jambo la kwanza ni uteuzi wa viungo wa kweli. De Jong ameanza kuchoka, wakati Jordy lasie na Vurnon Anita hawana lolote la maana kucheza viungo wa ulinzi, lakini bora wao kuliko viungo waliocheza katika mechi 4 zilizopita za Uholanzi.
Jambo lingine ni kuwaondo wachezaji wakongwe waliochoka. Wakati Van Persie, Sneijder na Huntelaar pamoja na De Jong wanaweza kusaidia timu kushinda mechi mwaka 2015, hawatokuwa na uwezo huo 2018. Ni muda wa kuingiza damu changa kwenye kikosi na kuwaacha wafeli mara kadhaa lakini matumaini ni kwamba watakuwa wana utayari wa kupambana pindi zitakapoanza mechi za kufuzu kombe la dunia 2018.
Tatizo la Uholanzi litadumu kwa muda mrefu?
Labda inaweza isiwe hivyo, ingawa inategemea na namna unavyoweza kuchukulia neno tatizo.
Kwa sasa wanapitia matatizo ya kawaida ambayo yanakuja na suala la kumalizika kwa kizazi cha dhahabu. Aidha Danny Blind atabaki au kufukzwa na mbadala mpya, bado wataendelea kupata taabu mpaka kwenye fainali za Kombe la dunia lakini watakuwa vyema zaidi katika Euro 2020.
Van der Wiel ndio mchezaji mwenye unri mkubwa zaidi katika safu ya ulinzi ya Wadachi akiwa na miaka 27. De Vrij, ambaye anatajwa kuwa bora zaidi kati safu yao ya ulinzi, ana miaka 23. Memphis Depay anaibuka kuwa staa akiwa na umri wa miaka 21. Hii inaonesha wana vipaji. vichanga ambavyo vikilelewa vizuri watakuwa na uwezo wa kushinda katika michuano mikubwa ijayo.
Vilevile bado wana utajiri wa wachezaji wachanga wanaokuzw vizuri kwenye vilabu vya Ajax na PSV wakipata nafasi katika vikosi vya kwanza vinavyocheza katika ligi kuu yao na Champions League/UEFA Cup.