Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

VIDEO: Rekodi 5 zilizowekwa baada ya ushindi wa England vs Scotland

$
0
0

england-vs-scotland

Kocha wa England Gareth Southgate baada ya kupewa mkataba wa kudumu kama kukinoa kikosi cha Simba watatu, usiku wa November 11 alikongoza kupata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Scotland katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2018.

Daniel Sturridge alianza kuipatia bao England dakika ya 24 akiitendea haki krosi ya Kyle Walker kabla ya mchezaji mwenzake wa Liverpool Adam Lallana kupachika bao la pili dakika tano baadaye.

Bao la Gary Cahill dakika ya 61 liliihakikishia ushindi England na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuvuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi.

Ushindi huo umeiweka England kwenye nafasi ya kwanza ya kundi F.

group-f

Rekodi zilizowekwa

  • Daniel Sturridge amefunga mara nne katika mechi sita za hivi karibuni alizoichezea England kwenye uwanja wa Wembley.
  • Magoli saba kati ya nane yaliyopita yalifungwa na England dhidi ya Scotland yamefungwa kwa vichwa na yote yamefungwa na wachezaji saba tofauti – Danny Welbeck, Rickie Lambert, Alex Oxlade-Chamberlain, Wayne Rooney, Daniel Sturridge, Adam Lallana na Gary Cahill.
  • England hawajapotza katika mechi 33 za kuwania kufuzu kombe la Dunia  (wameshinda mara 25 na kutoka sare mara 8) tangu walipochezea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Ukraine October 2009.
  • Scotland wameruhusu magoli kutokana na mashuti yote matatu yaliyolenga goli.
  • England wamefunga magoli matatu au zaidi kwenye mechi tatu mfululizo dhidi ya Scotland kwa mara ya kwanza.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>