Mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski ilibidi apatiwe matibabu baada ya kupigwa na flare (fataki) lililotupwa na mashabiki wake wa nyumbani na kulipuka karibu yake wakati wa mchezo wa kutafuta nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Romania.
Mchezaji huyo wa Bayern Munich hakupata majeraha lakini alipata mstuko kutokana na tukio hilo lililofanyika mapema kipindi cha pili na kulazimisha mchezo kusimama kwa dakika kadhaa.
Mechi hiyo iliyopigwa mjini Bucharest ilishuhudia fataki zikitupwa uwanjani mwishoni mwa kipindi cha kwanza.
Poland waliibuka na ushindi wa bao 3-0 kwenye pambano hilo la Kundi E.
Mshambuliaji wa Rennes Kamil Grosicki alifunga bao la kuongoza na kuiweka Poland mbele dakika ya 11 baada ya mchezo kuanza, magoli mengine yalifungwa na Lewandowski dakika ya 82 na dakika ya 90 kwa mkwaju wa penati.
Poland ambayo bao haijapoteza mchezo, inaonoza kundi ikiwa na pointi 10 baada ya kucheza mechi nne. Montenegro yenye pointi saba inaendelea kusalia nafasi ya pili licha ya kupokea kichapo cha bao 3-2 kutoka kwa Armenia.