Matumaini ya Argentina kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 bado yapo mashakani lakini Leo Messi ameonekana kupambana kuhakikisha timu yake inakwenda Russia.
Akiwa amerejea kutoka kustaafu soka, nyota huyo wa Barcelona alifunga bao la kwanza dakika ya 10 kwa mkwaju wa mbali wa free Kick.
Kikosi cha Argentina chini ya Bauza kilichapwa bao 3-0 na Brazil weekend iliyopita lakini kilikuwa kikiongoza 2-0 baada ya dakika 30 kilikuwa kikihitaji ushindi kwa kila namna mbele ya Colombia usiku wa jana.
Messi, 29, alipiga kwa ufundi mpira wa free kick dakika ya 10 na kufungua nyavu za Colombia huku mlinda mlango wa Arsenal David Ospina akishindwa kufanya lolote.
Angalia hii video namna Messi alivyopiga funga goli kabla ya ku-assist bao la pili.