Ulikuwa ni mchezo wa kirafiki, lakini huenda kocha wa England Gareth Southgate hakufurahishwa na kikosi chake kushindwa kulinda ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Spain.
Kiungo wa Real Madrid Isco alifunga bao dakika ya 96 na kuisawazishia timu yake baada ya Iago Aspas kufunga bao la kwanza dakika ya 89 ikiwa ni mchezo wake wa kwanza kuitumikia timu ya taifa ya Spain.
Magoli kutoka kwa Adam Lallana na Jamie Vardy yaliwapa faida Three Lions kuwa mbele lakini baada ya filimbi ya mwisho matokeo yalisomeka England 2-2 Spain.